2709; Uvivu na uzembe.
Hawa ni maadui wakubwa wawili ambao ndiyo kikwazo kinachowazuia wote ambao hawajafanikiwa.
Kwa kila ambaye hajafanikiwa, unapochunguza lazima unakuta maadui hao wawili wapo.
Uvivu ni pale mtu unapojua nini unachopaswa kukifanya, ila hukifanyi.
Unaweza kujipa sababu lukuki kwa nini hufanyi.
Lakini ukweli ni kwamba una uvivu.
Utajilaghai hujawa tayari, umechoka, utalaumu wengine na mengi utakavyo.
Lakini ukweli usiopindisha ni kwamba kama hufanyi unachopaswa kufanya huo ni uvivu.
Uzembe ni pale unapofanya chini ya kiwango unachopaswa kufanya.
Unapofanya kitu kwa mazoea na kuiga wengine.
Unaposhindwa kujitofautisha na kwenda hatua ya ziada.
Unapopata mafanikio kidogo na kuridhika nayo, ukiona umeshamaliza kila kitu.
Unakua uko bize kweli kweli, lakini hakuna cha maana unachokamilisha kwenye mengi unayohangaika nayo.
Uvivu na uzembe ni maadui wakubwa unaopaswa kupambana nao kila siku la sivyo watakuzidi nguvu na kukuzuia kufanikiwa.
Hatua za kuchukua;
Ukatae uvivu kabisa kwenye maisha yako, fanya kila unachopaswa kufanya bila ya kujipa sababu.
Kataa kabisa uzembe, kila wakati jisikume kufanya kwa ubora zaidi ya ulivyokuwa unafanya.
Tafakari;
Uvivu na uzembe ni maneno makali na yanayoumiza. Hivyo watu huwa hawapendi kujiambia wala kuwaambia wengine.
Lakini ndiyo ukweli, ambao mara zote huwa unaumiza.
Hujafika unakotaka kufika, sababu ni uvivu na uzembe ambao umekuwa nao.
Kama hutakuwa tayari kukiri hayo na kubadilika, utaendelea kuhangaika bila ya manufaa yoyote.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining