#SheriaYaLeo (213/366); Ufanye uwepo wako uwe wa msisimko.

Kwenye dunia ambayo ni ngumu na iliyojaa hali za kukatisha tamaa, watu wanapenda sana kukaa na watu wanaowapa msisimko.

Hilo linarahisisha zoezi la ushawishi kwa sababu watu wanakazana sana kupata nafasi ya kuwa karibu na wewe.

Ili kuwezesha hilo, hakikisha watu hawakuelewi kwa undani na kukuzoea.
Badala yake kunapaswa kuwa na vitu ambavyo watu hawaelewi kuhusu wewe.

Kadiri watu wanavyotaka kujua zaidi kuhusu wewe ndivyo wanavyozidi kukufuatilia na hilo kuwafanya washawishike zaidi na wewe.

Siyo lazima uwe mtakatifu sana ndiyo uweze kukamilisha hilo, kuwa hivyo kunaweza kuwachosha watu haraka.
Unaweza kuwa hatari, mtukutu au usiyetabirika, lengo ni kuwaweka watu kwenye hali ya msisimko ili waendelee kukufuatilia zaidi na iwe rahisi kuwashawishi.

Sheria ya leo; Kamwe usikubali kuwa wa kawaida au kujiwekea ukomo. Fanya uwepo wako uwe wa kusisimua ili watu wavutiwe kukufuatilia na iwe rahisi kuwashawishi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji