#SheriaYaLeo (214/366); Sanaa ya ushawishi.
Lengo la hotuba ya ushawishi ni kutengeneza hali ya mtu kukubaliana na hoja bila ya kuihoji.
Hotuba ya aina hiyo huwa inawavuruga watu, kuondoa mapingamizi yao na kuwafanya wawe rahisi kushawishika.
Hotuba hiyo huwa inakuwa na maneno yanayojirudia rudia, yenye msisitizo na yanayogusa hisia.
Lengo ni kumfanya anayesikiliza ashawishike haraka bila hata ya kuhoji.
Hotuba hiyo pia inakuwa na maneno ya moja kwa moja na ya kuamrisha badala ya kupendekeza.
Haina maneno kama Nadhani… Nafikiri… Napendekeza….
Badala yake inakuwa na maelezo ya moja kwa moja.
Tumia sanaa hii ya ushawishi ili uweze kutoa maelezo ambayo yanakuwa na ushawishi mkubwa kwa watu unaowalenga.
Sheria ya leo; Chagua vizuri aina ya maneno unayotumia kwenye maelezo yako. Ondoa maneno ya mapendekezo na weka maneno ya moja kwa moja na ya kuamrisha.
Hayo yanakuwa na ushawishi zaidi maana yanamfanya mtu awe na imani fulani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji