#SheriaYaLeo (219/366); Waweke kwenye hali ya kudhani.
Ili kuwafanya wengine wakufuatilie na hivyo kuweza kuwashawishi, unapaswa kuwaweka kwenye hali ya kudhani.
Usiwape uhakika kwa kujua kila kitu kuhusu wewe.
Kwani watu wakishakijua kitu na kuwa na uhakika nacho huwa wanakizoea, wanakichoka na kuacha kukifuatilia.
Watu huwa wanachoshwa haraka sana na kitu ambacho wameshakijua na kukielewa.
Pale wanapokuwa na uhakika na kujua kila kitu kuhusu wewe, wanakupuuza na kutokukufuatilia kwa karibu.
Watu wakishakupuuza ni vigumu sana kushawishika na wewe.
Hakikisha kuna vitu ambavyo watu hawajui au kupata uhakika kuhusu wewe.
Pia endelea kubadilika kadiri unavyokwenda na kuwaweka watu kwenye hali ya kutokuwa na uhakika ni nini utakwenda kufanya.
Watu wanapokosa uhakika kuhusu wewe wanajikuta wakilazimika kukufuatilia kwa karibu zaidi.
Ni kupitia kukufuatilia huko ndiyo wanashawishika zaidi na wewe.
Mara zote kuwa na vitu ambavyo vinawashangaza watu, ambavyo hawakuwa wanajua kuhusu wewe.
Hilo litakujengea ushawishi mkubwa.
Sheria ya leo; Ili kunasa umakini wa watu, unapaswa kuwaweka kwenye hali ya kudhani. Usiwape watu nafasi ya kujua kila kitu kuhusu wewe na kuwa na uhakika. Mara zote badilika na kuwa na vitu vinavyowashangaza, hayo yatawafanya waendelee kukufuatilia na washawishike zaidi na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji