#SheriaYaLeo (252/366); Tumia vizuri machafuko.

Fikiria akili yako kama jeshi.
Jeshi linapaswa kuweza kuendana na ugumu na machafuko yanayoendelea kwa kutumia njia isiyotabirika.

Kama ilivyo kwenye vita vya msitumi, adui hatumii mkakati wote mazoea, badala yake kila wakati anakuwa kwenye mwendo.
Hali hiyo inafanya kuwa vigumu sana kumshambulia adui huyo.
Hiyo ni kwa sababu kila wakati anakuwa anabadilika.

Ushindi kwenye vita vya msituni huwa unatokana na kuwa kwenye mwendo wakati wote.
Pale adui anapopanga kushambulia eneo fulani ambapo jeshi hilo lilikuwepo, wanakuta limeshamaha.

Kuwa kwenye mwendo ambao hautabiriki, inafanya mashambulizi kuwa magumu.

Hivyo ndivyo fikra zako zinapaswa kuwa, zisigande kwenye kitu kimoja ulichozoea. Badala yake fikra zako ziwe tayari kubadilika kulingana na mambo yanavyobadilika.

Kuwa kwenye mwendo muda wote, kunawafanya maadui wakose cha kushambulia.
Unasababisha machafuko ambayo unayatumia vizuri kupata kile unachota kwenye maisha yako.

Sheria ya leo; Yakabili matatizo na changamoto kwa kutumia njia mpya ya kufikiri na kutumia vizuri hali ilivyo. Mara zote kuwa tayari kubadilika na kuendana na hali ilivyo, hilo litakupa fursa ya kufanya vizuri na kutumia machafuko kwa manufaa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu.
UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji