#SheriaYaLeo (265/366); Wafanye wakuambie siri zao.
Kwenye mchezo wa madaraka, lengo lako ni kuwa na udhibiti mkubwa wa matukio yajayo.
Lakini tatizo kubwa litakalokukabili ni watu kutokuaa tayari kukuambia siri zao.
Watu wanapokuwa na udhibiti kwenye kile wanachosema, huwa wanaficha yake maeneo muhimu au ambayo wana udhaifu mkubwa.
Hilo linafanya iwe vigumu kwako kujua nini kitakachoendelea au wamepanga kufanya nini.
Hilo linakuweka kwenye giza na kukukosesha udhibiti wa yale yajayo.
Njia pekee ya kuvuka hilo ni kutafuta njia ambayo itawafanya watu wakuambie siri zao.
Unatakiwa uweze kufanya hivyo bila ya watu kukushtukia kwamba unachukua siri zao.
Njia bora ya kukamilisha hilo ni kuwa muulizaji wa maswali na kusikiliza kwa makini.
Kadiri unavyomfanya mtu mwingine aongee zaidi ndivyo unavyomweka kwenye nafasi ya kukuambia siri zake.
Hilo unapaswa kulifanya kwa makini ili watu waone mnafanya mazungumzo ya kawaida na wasijue lengo lako ni kuwafanya wakuambie siri zao.
Lazima uwe tayari kujikandamiza mwenyewe kwenye hayo mazungumzo ili kumpa mwingine sehemu kubwa ya kuongea.
Ni kupitia kuongea sana ndiyo wengi wanajikuta wamekuambia siri zao bila hata ya kujua kwamba wamefanya hivyo.
Sheria ya leo; Kwenye mazungumzo yako na watu wengine, wafanye wao waongee zaidi na watakueleza mambo mengi usiyojua kuhusu wao na hilo litakupa fursa kubwa ya kuwa na ushawishi kwa watu hao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
Asanteee
LikeLike