#SheriaYaLeo (275/366); Sheria ya msingi ya asili ya binadamu.
Sisi binadamu wote huwa tuna asili ya aina moja.
Kwa ujumla sisi binadamu wote ni viumbe wa kihisia, ambao huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia.
Lakini sheria ya msingi kabisa ya asili ya binadamu imekuwa ni kukataa asili yake.
Huwa tunajiona sisi ni wa tofauti ukilinganisha na wengine.
Tunaona wengine ndiyo wenye matatizo ila siyo sisi.
Tunaona wengine ndiyo wanaofanya maamuzi yao kwa hisia, wakati sisi tukijiona tukiwa tunafanya maamuzi kwa mantiki.
Ukweli ni kwamba sisi binadamu wote tuna asili moja na hivyo tunafanana kwa mambo mengi.
Sisi binadamu wote ni viumbe wa kihisia, ambapo huwa tunafanya maamuzi yetu kwa kusukumwa na hisia na siyo mantiki.
Hivyo ndivyo asili ya binadamu imekuwa kwa muda mrefu na tutaendelea kuwa hivyo.
Badala yakuona wengine ndiyo wenye shida ila siyo wewe, tambua wote tuna asili moja na hivyo tunafanana kwenye mengi.
Usiikatae asili yako kwa sababu ya madhaifu yake. Bali ikubali ili uweze kuitumia vizuri.
Sheria ya leo; Kubali asili yako kama binadamu ambayo unafanana na wengine. Acha kujiona wewe kama wa tofauti au uko juu sana ya wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
Ni kweli kocha nakubali Mimi ni ni binadamu pia nafanana mambo mengi na wenzangu sitajiona kuwa Mimi niko juu zaidi yao badala yake nitaheshimu kila ninae kukutana nae.
LikeLike