Rafiki yangu mpendwa,
Mimi huwa siyo mfuatiliaji wa habari wala michezo.
Ila siku ya jana tarehe 31/07/2022 nilishangaa kuona kukutana na taarifa za bondia anayeitwa mandonga kila mahali.
Nilipochunguza kujua nini kinaendelea ndiyo nikaujua ukweli, kwamba ni bondia aliyekuwa akitamba kwamba atampiga vibaya mpinzani wake.
Lakini kufika kwenye pambano yeye ndiyo akaishia kupigwa vibaya.
Watu wengi sana wamemdhihaki bondia huyo mandonga kwa tambo alizokuwa nazo na kipigo alichopokea.
Kama kawaida yangu, ninapoona watu wengi wanakubaliana na jambo, huwa najiambia kuna kitu hakipo sawa.
Hivyo kwa mandonga nilijiuliza nini halipo sawa mpaka wengi wawe wanakubaliana kwenye hilo.
Na hapo ndipo nikaona hili, video za mandonga akiwa anatamba kumpiga mpinzani wake hazikusambaa sana kabla ya pambano.
Lakini baada ya pambano ambapo mandonga alipigwa licha ya tambo zake, ndiyo video zake zikaanza kusambaa kwa kasi.

Tunajifunza nini kwenye hilo?
Watu huwa wanasubiri ushindwe ndiyo wa kudhihaki.
Kumbe watu hawapendi pale unapoeleza wazi wazi malengo yako makubwa.
Sasa kwa kuwa hawajui kama utayafikia au la, watakaa kimya.
Pale utakaposhindwa, ndipo sasa wataibuka kutoka walikokuwa wamejificha na kuanza kukudhihaki.
Je ufanye nini?
Uache kusema wazi malengo yako makubwa?
Jibu ni hapana.
Wapuuze wote,
Wewe jiwekee malengo makubwa na kama unasukumwa kuyaweka wazi, fanya hivyo.
Kushindwa ni sehemu ya kila safari ya mafanikio.
Hata watu wakubeze kiasi gani, wewe jifunze kwa kila unalopitia na kukazana kuwa bora zaidi.
Haya, sasa ni wakati wa kutoa tambo kama za mandonga.
Nani anataka kuwa bilionea?
Fungua kiungo; https://t.me/kochadrmakirita na andika NATAKA KUWA BILIONEA.
Halafu njoo tupambane pamoja kama mandonga.
Tutapokea za uso nyingi, tutadhihakiwa na wengi.
Lakini hatutakata tamaa mpaka tumefikia ubilionea.
Rafiki yako.
Kocha Dr Makirita Amani.
https://t.me/kochadrmakirita