#SheriaYaLeo (312/366); Furahia mafanikio ya wengine.
Ni rahisi kwetu binadamu kupata wivu pale wengine wanapofanikiwa kuliko sisi.
Na pale watu hao tunaowaonea wivu wanapopatwa na matatizo, huwa tunafurahia.
Tunafurahia kuwaona wakiwa kwenye matatizo na maumivu mbalimbali.
Lakini hilo halina faida yoyote kwetu, zaidi tu ya kutufanya tushindwe kufanikiwa kama watu hao.
Itakuwa na faida kubwa kwetu kama tutaweza kwenda kinyume na mazoea hayo.
Tuwe tunayafurahia mafanikio ya wengine.
Yaani pale wengine wanapokuwa wamepiga hatua fulani, badala tu ya kuwapongeza, tunafurahia kabisa ndani yetu.
Hili la kuyafurahia mafanikio ya wengine lina manufaa makubwa kwetu.
Pamoja na kuwafanya watu hao kujisikia vizuri, lakini pia linatuweka kwenye urahisi wa sisi kufanikiwa pia.
Hii siyo kawaida kwetu binadamu, hivyo ni lazima ujifunze na kufanya mazoezi ha kulifanya hilo mara kwa mara mpaka liwe zoezi la kawaida kwako.
Furahia mafanikio ya wengine kutoka ndani ya moyo wako kweli.
Itaimarisha mahusiano yako na wao na itakupa msukumo wa wewe kufanikiwa pia.
Sheria ya leo; Jifunze kuifanya furaha ya wengine kuwa yako. Kwa kufanya hivyo inakusaidia kujenga mahusiano mazuri na kukupa msukumo wa kufanikiwa pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
Asante nafurahia mafanikio ya wengine waliofanikiwa kila siku na furaha ya wengine ni furaha yangu pia
LikeLike