2821; Kila mtu anafanya.

Sababu ya hovyo kabisa ya kufanya kitu ni kila mtu kuwa anakifanya.
Sisi binadamu kama viumbe wa kimamii huwa tunapenda sana kufuata mkumbo.

Lakini tuanze tu kwa kuuangalia ukweli ulivyo.
Watu wengi kwenye jamii hawafanikiwi.
Kwa kuwa wale tunaojihusisha nao wana ushawishi mkubwa kwetu, tunapaswa kuwaepuka sana wale ambao hawapigi hatua.

Kila mtu anafanya pia ni kigezo kizuri cha kukataa au kuacha kufanya kitu.
Mambo ya kufanya ni mengi na muda wa kuyafanya ni mchache.
Kuweka muda wako kwenye mambo yanayofanywa na kila mtu ni kuchagua kuupoteza.

Wengi huwa hawafanikiwi, kwa sababu wanakimbilia urahisi.
Hivyo unapoona kitu kinakimbiliwa na wengi, jua kabisa ni kitu rahisi na wewe kujihusisha nacho ni kupoteza muda wako.

Hata kama kuweka vipaumbele ni kugumu kwako, anza kwa hili la kuangalia wingi wa watu.
Unapoona wengi wanakimbilia kitu, usiungane nao kukimbilia kukifanya.
Badala yake fanya kilicho tofauti.

Hatua ya kuchukua;
Jua hasa kile unachotaka na njia ya kupita ili kukipata.
Epuka kufuata mkumbo au kuiga kile kinachofanywa na kila mtu.
Muda na nguvu zako ni rasilimali zenye uhaba, vitumie vizuri ili usivipoteze.

Tafakari;
Watu wengi hawana mafanikio makubwa.
Hivyo wajibu wako mkubwa ni kuwaepuka watu wengi.
Usifuate mkumbo au kuiga kile kinachofanywa na wengi.
Hakina thamani kubwa ya kukufikisha wewe kwenye mafanikio makubwa.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed