#SheriaYaLeo (337/366); Tukio ambalo huenda lisingetokea.
Huwa tunayachukulia maisha kikawaida na kwa mazoea.
Lakini tukitafakari kwa kina, ni tukio ambalo huenda lisingetokea.
Tangu kuanza kwa maisha hapa duniani, mabilioni ya miaka iliyopita, kila tukio limekuwa linatokea kwa namna ambayo haiwezi kuelezeka.
Hata wakati sisi binadamu tunajitenga na wanyama wengine na kuwa jamii ya tofauti, ilitokea kama nafasi tu, ambayo hakuna anayeweza kusema ilitegemea.
Na ukija kwako mwenyewe, kukutana kwa wazazi wako mpaka wewe kupatikana, ni mambo ambayo huenda yasingetokea.
Vipi kama mmoja wa wazazi wako angekutana na mtu mwingine? Je ungepatikana?
Na vipi kama siku waliyojamiiana ukapatikana mmoja angekuwa anaumwa na hilo lisingefanyika, je ungepatikana?
Ukiifikiria dunia kwa mapana yake, unajionea wazi jinsi ambavyo kila kilichopo duniani kimetokea kama bahati tu.
Kila kitu ni tukio ambalo lisingewezekana.
Hiyo inatupa sababu nyingine kubwa ya kuthamini kila kitu na kushukuru kwa kila jambo.
Maana kwa nafasi kubwa sana, ni mambo ambayo huenda yasingetokea.
Sheria ya leo; Kila kitu kilichopo hapa duniani kina thamani kubwa sana, kwa sababu chimbuko lake ni la bahati ya kipekee sana. Ni tukio ambalo huenda lisingetokea, lakini kwa sababu tusizozielewa limetokea. Tunapaswa kuthamini na kushukuru kwa kila jambo.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji