#SheriaYaLeo (339/366); Ulimwengu upo ndani yako.

Kama unataka kuelewa ukubwa na ukuu wa ulimwengu usio na ukomo, anza kwa kuangalia ubongo wako.
Ndani ya ubongo wako kuna miunganiko ya seli zaidi ya milioni bilioni moja.

Kama ingebidi uhesabu miunganiko hiyo, mmoja kwa kila sekunde, ingekuchukua miaka milioni 32 kukamilisha.

Ukiangalia ukubwa wa muunganiko wa seli za ubongo wako unaweza kuelewa jinsi ulimwengu usivyo na ukomo.
Unaweza kuona jinsi ambavyo ubongo wetu ulivyo na uwezo usio na ukomo.

Yote unayoyaona ya kukushangaza kwenye ulimwengu, jua yapo pia ndani yako.
Ukiweza kutumia vizuri uwezo wa ubongo na akili yako, utaweza kufanya makubwa sana.

Sheria ya leo; Ukuu wa ulimwengu tayari upo ndani yetu, ni kuujua na kuutumia kwa manufaa.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji