2947; Shinikizo na muda.
Rafiki yangu mpendwa,
Tangu enzi na enzi, watu wamekuwa wakitafuta njia rahisi ya kupata mafanikio makubwa.
Kwa miaka mingi ya nyuma, watu walitafuta sana njia ya kubadili madini ya kawaida kama risasi (lead) kuwa dhahabu.
Iliaminika ipo njia ya kufanya hivyo (alchemy) na watu waliambiwa kwa kupata jiwe dogo na mchanganyiko fulani, basi wangeweza kutengeneza utajiri mkubwa.
Watu wengi sana waliamini hicho ni kitu kinachowezekana na hivyo kunasa kwenye huo utapeli.
Hata watu waliokuwa na uelewa mkubwa, wanasayansi kama Newton, nao walinasa kwenye hilo na kutumia muda mwingi kutafiti jambo hilo.
Kwa miaka mingi watu walidanganyika kwenye hilo lakini hakuna aliyefanikiwa.
Na mpaka leo, bado watu wanaendelea kutapeliwa kwa kunaswa kwenye tamaa ya kupata mafanikio makubwa kwa haraka.
Angalia kila aina ya utapeli ambao watu wananaswa nao na utaona mtego ni mmoja, kupata mafanikio makubwa kwa haraka.
Ukweli ni kwamba, mafanikio makubwa yanaweza kupatikana, ila siyo kwa haraka.
Ni kweli kwamba madini ya kawaida yanaweza kugeuzwa kuwa madini ya thamani kubwa, ila siyo kwa haraka.
Kwa mfano, almasi, madini yenye thamani kubwa, huwa yanatokana na makaa ya mawe, ambayo thamani yake ni ndogo tu.
Lakini mchakato mzima wa kugeuza makaa ya mawe kuwa almasi, unahusisha shinikizo kubwa na muda mrefu. Makaa hayo ya mawe yanakaa kwenye mkandamizo mkubwa, miaka na miaka na hilo linapelekea yageuke kuwa almasi, ambayo ni imara na yenye thamani kubwa.
Tunachojifunza hapa ni mafanikio yoyote makubwa ambayo mtu anayataka yanawezekana, kama atajiweka kwenye shinikizo kubwa na kwa muda mrefu.
Inampasa mtu kuweka umakini wake wote kwenye kitu kimoja na kwa muda mrefu ndiyo aweze kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti kwenye kitu hicho.
Na hivyo ndiyo vitu viwili muhimu ambavyo wengi hawapo tayari kuviweka.
Ndiyo maana utapeli unaendelea kuwepo.
Kwa sababu wengi wanaamini kuna njia ya mkato ya kupata mafanikio makubwa.
Kubali kwamba hiyo njia haijawahi kuwepo na wala haitakuja kuwepo.
Chochote unachotaka kufikia, lazima uweke shinikizo kubwa na kwa muda mrefu.
Ni kitu gani umekuwa unakitaka sana lakini kimekuwa hakitokei?
Hebu weka shinikizo kubwa na muda mrefu na uone kama mambo hayatakuwa vile unavyotaka.
Kama ambavyo almasi inatokana na makaa ya mawe yaliyowekwa kwenye shinikizo kwa muda mrefu, ndivyo mafanikio makubwa yanaweza kupatikana kwa yeyote anayejiweka kwenye shinikizo kwa muda mrefu.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Najiweka kwenye shinikizo kubwa kwa Muda mrefu.
LikeLike
🔥🔥
Dhahabu yenyewe inapitishwa kwenye moto ili iwe safi.
Hicho kikombe hakikwepeki.
LikeLike
Ni sahihi kabisa Kocha Muda
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ahsante sana Kocha.
Naweka shinikizo zaidi kwa muda mrefu kuufikia ubilionea mwaka 2030.
Naweka muda katika kujifunza, kujenga biashara, kujenga mfumo wa biashara, kukuza team ya mauzo na kukuza mauzo zaidi.
Lazima nitoboe, hakuna Cha Kunizuia
#NidhamUpendo
LikeLike
Safi,
Pambana.
LikeLike
Asante kocha,kwa makara ya leo.
LikeLike
Najigeuza almasi kutoka kwenye risasi kupitia mchakato wa kila siku kwa miaka kumi mfulilizo bila kuacha.
LikeLike
Safi.
Pambana
LikeLike