2952; Hili basi linaenda wapi?
Rafiki yangu mpendwa,
Pata picha una safari yako ya kwenda eneo fulani.
Unafika stendi ya mabasi na kukata tiketi ya safari yako na kuelekezwa basi unalopaswa kupanda.
Unakwenda kwenye basi na muda siyo mrefu dereva anawasha gari kuondoka.
Kujihakikishia safari yako, unamuuliza dereva swali; “hili basi linaenda wapi?”
Dereva anakuangalia kwa umakini na kukujibu; “kusema kweli sijui basi linakokwenda.”
Kwa akili timamu, kitu cha kwanza utakachotaka kufanya ni kushuka kwenye basi hilo kabla hujaendelea kupotea.
Kabla hujataka kujua imekuwaje dereva kutojua mwelekeo wa safari, utataka kwanza usiendelee kupotea.
Na kwa hayo utakuwa sahihi.
Sasa tutoke kwenye mfano na tuje kwenye uhalisia na kumhoji dereva wewe.
Hiyo biashara unayoendesha, inaelekea wapi?
Ni maono yapi makubwa uliyonayo kwenye biashara unayofanya au nyingine yoyote.
Unajiona wapi kila baada ya muda fulani?
Kama huwezi kujijibu hayo maswali kwa uhakika, upo kwenye njia ambayo hujui kama ni sahihi au la.
Na huko ni kupoteza muda mwingi sana.
Ni lazima ujue kwa hakika kabisa hiyo biashara yako inaenda wapi.
Lazima ujue kila baada ya muda fulani itakuwa imefikia hatua fulani.
Yajue hayo yote kwa uhakika kabisa kwako na kaa kwenye njia sahihi ya kufika kule unakotaka kufika.
Biashara yako inaenda wapi na kila baada ya muda inakuwa wapi ndiyo kitu cha kuanza nacho kwenye safari yako.
Maana hayo ndiyo yataamua kila kinachopaswa kufanyika na kutokufanyika kwenye biashara hiyo.
Haina haja ya kuwa na mbio kama haupo kwenye njia sahihi.
Maono, malengo, mikakati na hatua za kuchukua ni sehemu muhimu ya safari yako ya kibiashara.
Hupaswi kufanya lolote kwa kubahatisha, bali unapaswa kuwa na mipango na mikakati unayofuata ili kufikia malengo na maono.
Unakosa shauku na hamasa au unahangaika na usumbufu usio na tija kwako ni matokeo ya kutokujua ni wapi kazi au biashara watu wanafanya zinaelekea.
Tumia biashara kama chombo cha kukufikisha kwenye yale maono makubwa uliyonayo kwenye maisha yako.
Na usikubali kuyumbishwa na chochote katika kuyapambania maono hayo unayokuwa nayo.
Watu wengi wapo kwenye biashara ambazo hawajui zinaelekea wapi hasa.
Hawawezi kupima ni hatua gani ambazo biashara hiyo inapiga kadiri inavyokwenda.
Hayo ndiyo yanayosababisha watu kukosa msukumo mkubwa wa kuzipambania biashara zao.
Hawajui ni matokeo gani ya kuvuna na kwa wakati gani kutoka kwenye biashara zao.
Hilo linawafanya wanabaki kuwa watumwa wa hizo biashara, kila wakati wakiwa wametingwa sana na uendeshaji wa biashara ambao unawategemea kwa asilimia 100.
Kama ambavyo utashuka haraka kwenye basi ambalo hujui linaenda wapi, ndivyo unavyopaswa kujitafakari haraka na kujua biashara yako inaelekea wapi.
Yajue wazi maono na mikakati iliyopo.
Kisha kaa kwenye mchakato sahihi wenye matokeo ya kila hatua unayotaka kufikia kupitia biashara hiyo.
Ukiamshwa usingizini na kuulizwa biashara yako inaenda wapi, unapaswa kuweza kujibu swali hilo kwa haraka na uhakika mkubwa.
Kama hutaweza kujibu hilo swali, unazurura tu na biashara yako, hakuna unakokwenda.
Usikubali kupoteza muda.
Jua kwa hakika unakokwenda ili ujisukume kupambana kwa kila namna kufika huko.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Haina haja ya kuwa na mbio kama haupo kwenye njia sahihi.
Kabla hujaendelea kufanya jiulize, je uko njia sahihi?
LikeLike
Ukiamshwa usingizini na kuulizwa biashara yako inaenda wapi, unapaswa kuweza kujibu swali hilo kwa haraka na uhakika mkubwa.
LikeLike
Asante sana kocha upo sahihi sana lazima ujue safari yako inaelekea wapi ndio usafiri
LikeLike
Asante kocha njia sahihi haipotezi napaswa kujua biashara yangu inaelekea wapi? Ndio nitumie njia hiyo kuhakikisha nafika Kule ninakohitaji kufika .Asante sana kwa maarifa haya
LikeLike
Muhimu kujua kazi au biashara tunazofanya zinakwenda wapi, maana ni kama chombo cha kutupeleka kwenye maono na malengo yetu. Asante kocha
LikeLike
Asante sana kocha ,bora dereva kipofu anayefahamu wapi gari linakwenda kuliko dereva anayeona na hajui wapi anaelekea.
LikeLike
Ili biashara idumu lazima iwe na msingi imara na kuendelea kujifunza juu ya biashara hiyo
LikeLike
Nitajua kwa uhakika ninako kwenda ili nipambanie kwa nguvu zangu zote
LikeLike
Ninafaham kwa uhakika wapi ninaelekea kisha nikipanda bas nafaham niendako
LikeLike
Biashara yangu inaelekea wapi?
LikeLike
Lazima kujua haswa kule tujapotaka kwenda kibiashara na maisha.Asante sana kocha.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa makala hii muhimu. Biashara yangu inakwenda wapi. Hakika AMSHA UWEZO inaenda kutengeneza media empire kuhusu UWEZO HALISI WA MWANADAMU na MAFANIKIO ANAYOSTAHILI
LikeLike
Najua ninakokwenda, katika kujenga biashara kubwa kutoka chini kabisa ambapo inanitegemea Kwa asilimia kubwa, na kuwa biashara inayoweza kujiendesha yenyewe, biashara inayokwenda kutatua matatizo/maumivu ya wateja, biashara inayokwenda kutatua tatizo la ajira kwenye jamii yetu na kuboresha maisha ya kila anaejihusisha nayo, biashara inayokwenda kukua na kuzaa kampuni kubwa ya kutoa huduma Bora kabisa kimataifa, biashara inayokwenda kunipa uhuru Kamili Wa kifedha na Uhuru Wa muda.
Biashara inayokwenda kunipa ubilionea na kufikia hatua ambayo pesa Wala muda haitakuwa kikwazo Tena kwangu.
Biashara inabaki kuwa mchezo ninaoufurahia kucheza, siyo kwaajili ya pesa Tena Bali kama mchezo tuu.
Hakuna kingine muhimu Lazima nitoboe au nife nikiupambania maono haya makubwa.
LikeLike
Safi sana, kaa humu kwa msimamo.
LikeLike
Unaweza kukimbia Kasi sana lakini kama haiko uelekeo sahihi ni kujilisha upepo bure.
LikeLike
Kuendelea kukimbia bila kujua uendeko ni hatari zaidi Bora kushuka TU kwenye Hilo gari.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri.
LikeLike
Basi langu linaenda kwenye Mji uitwao Uhuru wa Kifedha. Vituo navyotakiwa kupitia ni Uwekezaji, Timu imara na mchakato wa mauzo kufikia Ubilionea. Ni safari ndefu na ya gharama na hatari kubwa lakini nimejiandaa vyema kuipita. Nitakazana mpk nifike au nitakufa nikiwa njiani Ila sitarudi Nyuma.
Dereva ni Kocha wangu na abiria ni mie mwenyewe na Basi letu linaitwa Kisima Cha Maarifa
LikeLike
Ni muhimu kujua unapokwenda ili kupata unachokata
LikeLike
Nina hakika na kule ambako biashara yangu ineanda.
LikeLike
Focus ni kitu muhimu ili kutoyumbushiwa na changamoto za njiani , Asante kocha kwa Makala bora
LikeLike
Sikubali kuyumbishwa na chochote katika kuyapambania maono yangu.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Ili niweze kuifurahia safari ni lazima niwe na uhakika nipo kwenye gari sahihi la ninakotaka kufika
LikeLike
Ahsante sana kocha kwa tafakari hii, hakika hakuna haja ya kuwa na mbio wakati sipo kwenye njia sahihi na pia ni wakati sahihi wa kujitathmini kama gari nlilopanda litanifikisha kule niendako
LikeLike
Hii inafanana na ukweli niliowahi shuhudia dereva akiruka toka kwenye gari na kuwaacha abiria kwenye gari. Hio ilitosha kutuambia kwamba gari sasa halina mweleo na hivyo kuendelea kuwepo kwa gari ni kuongeza hatari juu ya hatari
LikeLike
Duh, hatari sana.
LikeLike
Kwa kweli swali hili ni muhimu sana kujiuliza mara kwa mara ili uweze kuchukua hatua stahik pale unapogundua kuwa unaelekea kupotea.
LikeLike
Unaweza kujikuta unapotea huku ukiwa hujui.
LikeLike
Inanipasa nijue vizuri niendako kabla ya kuchukua Hatua yoyote. Asante sana Kocha.
LikeLike
Ni kweli tuna muda mwingi lakini tunatumia kwa mambo yasiyoleta tija kwenye malengo yako pia tulenge kufanya mambo mavhache kwa muda mrefu
LikeLike
Tuache kupotea ili tuokoe muda.
LikeLike
_ ninapaswa kuwa na maono makubwa
_kila wakati .ninapaswa kujua kwa uhakika kabisa matokeo ninayokwenda kupata
_mara zote ninapaswa kila wakati kuwa ktk mchakato
wa kuelekea ktk maono yangu
LikeLike
Sisi Ni namba moja au namba mbili katika kitu chochote tutakachofanya
LikeLike
Vizuri.
LikeLike