2980; Kubali kupitwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Inapokuja kwenye swala la mafanikio, wengi huwa na mtazamo wa kutokukubali kupitwa na chochote.
Lakini huo ni mtazamo ambao unakuwa kikwazo kikubwa kwa wengi kupata mafanikio makubwa.
Tamaa huwafanya wengi kuhangaika na mengi wakidhani watairahisisha safari ya mafanikio, lakini kwa uhalisia wanaishia kuwa wameirefusha safari hiyo.
Elon Musk na Charlie Munger ni mabilionea wawili ambao wote ni watu wa mfano kwangu. Ni watu ambao nimechagua kujifunza kwao kwenye safari yangu ya ubilionea.
Mwaka 2008, kampuni ya Elon Musk inayoitwa Tesla, ambayo inazalisha magari ya umeme ilikuwa kwenye hali mbaya sana kifedha, ilikuwa inakaribia kufilisika.
Elon Musk akihangaika kutafuta fedha kwa watu wengi na moja wa watu hao akawa Charlie Munger.
Musk alipata nafasi ya kuongea na Munger na kumweleza kuhusu kampuni yake na kiasi cha fedha anachohitaji ili kuinusuru na kuifanya iwe kampuni yenye faida.
Munger alimpa Musk sababu nyingi sana za kwa nini kampuni yake itashindwa, na hivyo hakuwa tayari kuweka fedha za kampuni yao ya uwekezaji ambayo anaiongoza pamoja na bilionea mwingine Warren Buffett.
Musk anasema alisikitishwa sana na hilo, akamjibu Munger kwamba ni kweli kuna hatari nyingi za kampuni yake kufa kuliko kupona. Akaendelea kueleza, lakini kama kitu ni muhimu, mtu unakifanya, bila kujali hatari yake.
Waliishia hapo na matokeo yake ni kampuni ya Tesla iliweza kuvuka hatari zote na kuwa yenye thamani kubwa sana kwenye soko la hisa.
Sasa watu wamekuwa wakimcheka Munger kwamba alipitwa na fursa. Kwamba kama angewekeza kwenye kampuni ya Tesla kipindi hicho, angekuwa ameongeza utajiri mkubwa sana kutoka kwenye ukuaji wa kampuni hiyo.
Lakini je, Munger anachukuliaje hali kama hiyo? Anajutia kupitwa na fursa nzuri kama hiyo?
Jibu ni hapana, Munger siyo tu hajutii, bali anafurahia kabisa.
Amekuwa akijinasibu wazi kabisa kwamba hawekezi kwenye maeneo ambayo yeye binafsi hana ujuzi nayo kwa kina.
Na eneo kubwa ambalo yeye na mwendake Buffett hawana uelewa nalo na hivyo kuliepuka ni teknolojia mpya.
Msimamo wao huo umewakosesha fursa nyingi sana za kupata faida kubwa kwenye makampuni yaliyokuwa mapya na ambayo sasa yamekua sana, kama Microsoft, Amazon, Google n.k.
Lakini matokeo yake ni yapi?
Munger na Buffett ni mabilionea wakubwa duniani.
Buffett akiwa amepata nafasi ya kushika namba moja kwenye watu matajiri zaidi duniani kwa kipindi kirefu. Mpaka sasa Buffett yuko kwenye kumi bora ya watu matajiri zaidi.
Kuna mengi sana ya kujifunza kwenye hili tuliloshirikishana hapa, ambapo mengine utashirikisha kwenye maoni hapo chini.
Lakini kubwa kabisa ambalo nataka wote tutoke nalo hapa ni kwamba mafanikio siyo kutokupitwa na chochote. Bali ni kuamua baadhi ya mambo mazuri kabisa yakupite kwa kuwa umechagua baadhi ambayo utakuwa bora zaidi.
Na kwa hayo uliyochagua kuwa bora zaidi yana fursa ya kukupa mafanikio yoyote unayotaka.
Acha kugangaika na kila fursa mpya inayokuja kwako, hasa zile ambazo haziendani na fursa kuu ulizochagua.
Hilo litakupa fursa ya kutumia vyema fursa ambazo tayari umeshazichagua sasa.
Tukumbuke mafanikio yapo kwenye kila eneo, kadiri unavyoweka juhudi na umakini kwenye eneo lolote ulilochagua, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko kuhangaika na kila fursa mpya inayojitokeza, hata kama ni nzuri na ya uhakika kiasi gani.
Hii haimaanishi kwamba utaacha kabisa kufanyia kazi fursa zote mpya. Ila inamaanisha utafanyia kazi fursa mpya kwenye maeneo ambayo tayari umeshayachagua na kupuuza maeneo mengine yote.
Tukubali kupitwa kwenye fursa nyingi nzuri ambazo haziendani na maeneo tuliyochagua ili tupate nafasi nzuri ya kuzama kwenye fursa za maeneo hayo na kupata mafanikio makubwa.
Je ni yapi mengine uliyojifunza kwenye hili la kupitwa? Shirikisha kwenye maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante kocha,
Kwenye mafanikio hakuna kupitwa bali kunakujifunza.
Pia. Tukumbuke kushindwa ni kushinda pia.
Ahsante sana.
LikeLike
Hakika,
Bila ya kuyatambua haya tutakata tamaa mapema sana.
LikeLike
Asante kocha,ntajitahidi kuweka umakini kwenye biashara moja kwanza nasio kutanga tanga nafursa zingine.
LikeLike
Vizuri sana.
Kusanya nguvu ili ziwe na madhara.
LikeLike
Kukubali kupitwa sio ujinga ila ni masmuzi bora ya kunisaidia kutulia na biashara moja au chache kwanza na kuzikuza ,na kisha kuangalia fursa nyingine ambayo nina ujuzi nayo.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri kabisa.
LikeLike
Asante,
Nilichojifunza ni msimamo,kuchagua kitu kimoja na kukifanya kwa muda mrefu sana bila kuyumbishwa.KamaWarren na Charlie Munger walivyokaa kwa muda mrefu kiuwekezaji na kwenye eneo wanaloluelewa
LikeLike
Kwa chochote kile utakachochagua kukifanya na ukaamua kuweka umakini wako wote kwenye kitu hicho ni hakika utafanikiwa
Asante Sana kocha
LikeLike
Kama kitu ni muhimu tusikate tamaa kukifanya pamoja na hatari zilizopo. Lakini pia tusitawaliwe na tamaa tukafanya mambo tusiyoyafahamu kwa uhakika.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa makala hii muhimu sana hasa kwangu.
Nilichojifunza hapa ni kuwa: Musk ni mtu ambaye amefanikiwa sana kwani hakukubali mapingamizi ya wanaoona hawezi kutoboa kupitia kampuni yake Tesla.
Lesson: Hata iwe nani anasema kuhusu kitu ulichochagua, usikubali kabisa kuiacha Imani Yako na kuanza kukimbilia fursa nyingine.
Ahsante sana Kocha 👏👏✍️✍️
LikeLike
Msimamo na kuepuka tamaa ni nguzo muhimu katika mafanikio ya kiuchumi.
LikeLike
Mm kwa upande wangu nmejifunza Kuchagua fursa moja kujifunza na kuchukua hatua mpaka unafikia mafanikio. Kwa upande kwenye uwekezaji, nimechagua kwanza kwa muda wa miaka 5 kuwekeza sana kwenye paper assets, najua Kuna Fursa nyingi kama ardhi na majengo lakini bora nipitwe kwanza na fursa hizo na kuonekana mshamba.
LikeLike
Asante sana kocha,
Nimejifunza kuwa na mcmamo kwenye yale niliyochagua kuyafanya kila kitu kinalipa, niache papara.
LikeLike
Kwetu sisi wafanyabiashara tulio wengi na niseme kwa upande wangu mimi niliathiriwa sana na hiyo kutokupitwa na fursa nimehangaika sana nazo na zingine hata sina ujuzi nazo ila kwa sasa siziangalii hata ninachoangalia ni ile yenye kulenga biashara yangu tu basi na hii ni kwa mabilionea wote
LikeLike
Asante Kocha.
Nilichojifunza kwenye makala hii ni kwamba, mafanikio ni kuacha baadhi ya mambo ambayo yanaonekana ni mazuri kabisa yakupite kwa kuwa umechagua baadhi ambayo utakuwa bora zaidi.
Na uchaguzi huu ni kwa sababu umeamua kufanya mambo ambayo unayajua kwa kina vizuri.
Asante
LikeLike
Sita hangaika na mengi kwenye karne hii kwani kila kitu ni mhimu na ni fursa lakini nimechagua biashara na uwekezaji kama njia ya kunifikisha mwenye uhuru wa kifedha na ubilionea,,,
LikeLike
Matatizo ya kutatua(fursa) ni hayajawahi kuisha, hata vitukuu wetu watayakuta matatizo ya kutatua(fursa) kwa wakati wao, nachagua matatizo machache ya kutatua na niatayatatua hayo kwa Muda mrefu Sana ili nipate nguvu kubwa ya kuyaathiri.
LikeLike
Nitakubali kupitwa na fursa zote ambazo hazipo kwenye mpango wangu!
LikeLike
Ni kweli huwezi kuwekeza kila mahali.
LikeLike
Kuna umuhimu wa kuwa na msimamo wa unacho fanya pamoja na kwamba fursa ni nyingi, hasa biashara ambazo huna ujuzi nazo hizo ndio za kuepuka kabisa, na kuendelea kufanya unazozijua kwa kina.
LikeLike
Ahsante sana kocha nitaachana na fursa ambazo sina ujuzi nazo
LikeLike
Hii imenikumbusha hivi karibuni ambapo mdogo wangu alinishirikisha fursa ya shamba la miti ambalo lilikuwa linauzwa kwa bei poa.Kipindi cha nyuma nilikuwa na ndoto ya kufanya kilimo cha miti kwa hiyo alitumia hilo kunishawishi nichukue shamba hilo.Nilipokumbuka malengo yangu ya sasa nikamweleza hilo haliwezekani kwa sasa.Kwa ni muhimu kukomaa na kile tunachofanya sasa kuliko kuhangaika na kila fursa inayokuja
LikeLike
Nilichoji funza ni kuwa kama kitu hujakielewa usiwekebpesa yako.
LikeLike
Fanyia kazi like unachoamini na komaa nacho Kwa msimamo na mafanikio yatakuja kwko I
Asante
LikeLike
Nakubali kupitwa ili nisitapanye nguvu zangu kitu ambacho kinapelekea kuchelewa kufika mafanikio, ahsante sana kocha
LikeLike
Huwezi kukosa kufanikiwa kwa kupitwa na fursa MOJA. Nia ya kweli inavuka changamoto nyingi.
Wekeza kwenye kitu unachojoua bila kutawanya nguvu.
Asante sana
LikeLike
Nakubali kupitwa kwa sababu siwezi kufanya kila kitu kizuri kinachokuja kwenye maisha.
LikeLike
Tusiwe viranja wa dunia.
LikeLike
Asante sana kocha, nitaendelea kuweka msimamo wangu kwenye biashara kuikuza kuliko kutaka kukimbia na kila fursa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike