2985; Usipoteze hiyo kazi ambayo umeshaweka.
Rafiki yangu mpendwa,
Tofauti ya kufanikiwa na kushindwa siyo akili wala juhudi zinazowekwa.
Wanaofanikiwa na wanaoshindwa hawatofautiani sana kiakili.
Na juhudi wanazokuwa nazo pia hazitofautiani sana.
Tofauti kubwa ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa inaanzia kwenye msimamo.
Wanaofanikiwa wanapeleka juhudi zao kwenye jambo moja kwa muda mrefu.
Wakati wanaoshindwa wanahamisha hamisha juhudi zao kwenye mambo mengi.
Hivyo hata kama watu hao wawili watafanya kazi au biashara kwa muda sawa, tofauti yao kubwa itaanzia kwenye msimamo wa ufanyaji.
Anayefanikiwa anakuwa amekusanya juhudi zake zote kwenye kitu kimoja kwa muda wote na hivyo anaweza kuleta matokeo ya tofauti.
Wakati anayeshindwa anakuwa ametawanya juhudi zake kwenye mambo mengi na kuishia kupata matokeo ambayo ni hafifu.
Ili kujikumbusha hili na kuacha kuwa kikwazo chako mwenyewe kwenye mafanikio, kila mara unapaswa kujikumbusha kwamba hupaswi kupoteza kazi ambayo tayari umeshaiweka.
Kila unapotaka kuacha kile ambacho umekuwa unafanya na kuanza kitu kipya, jikumbushe kuna kazi ambayo umeshaiwekeza kwenye hicho unachotaka kuacha.
Swali ni je upo tayari kupoteza kazi yote hiyo na kwenda kuanza upya?
Kama ni maji ya kisima umekuwa unapampu, kisha ukaona yanachelewa kutoka na kuamua kuachana nayo, tambua kuna maji yako njiani kuja.
Je upo tayari kuyapoteza maji hayo yarudi chini kwa wewe kuacha na kwenda kwenye mambo mengine?
Kama ni maji unachemsha na unaona kama yanachelewa kuchemka hivyo kutaka kuachana nayo, swali ni je upo tayari kupoteza moto wote ambao tayari umeshaenda kwenye maji hayo?
Kwa sababu kwa kuacha yatapoa na yakipoa utahitajika kuanza upya kuyachemsha.
Kama unaweka juhudi na huoni matokeo, siyo kwamba juhudi hizo zimepotea, bali bado zinajikusanya ndiyo ziweze kuzalisha matokeo makubwa.
Wajibu wako ni kuendelea kuweka juhudi hizo ili ziendelee kukusanyika na kukupa matokeo makubwa sana.
Pale unapokata tamaa na kuacha kufanya, unakuwa umepoteza juhudi zote za nyuma unazokuwa umeweka.
Usikubali kupoteza juhudi zote ambazo umeshaweka mpaka sasa.
Endelea na mapambano, mambo makubwa na mazuri yapo mbele yetu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuwa na msimamo kwenye kitu kimoja ili kupata matokeo bora.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ahsante sana kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kama unaweka juhudi na huoni matokeo, siyo kwamba juhudi hizo zimepotea, bali bado zinajikusanya ndiyo ziweze kuzalisha matokeo makubwa.
LikeLike
Tusipoteze hizo juhudi kwa haraka zetu za kutaka matokeo ya hapo kwa hapo.
LikeLike
Asante Kocha kwa kweli sipo tayari kupoteza kile nilichoanza, zinakuja fursa nyingi za kutaka kunitoa kwenye focus lakini kwangu ni msimamo ndio unanipa matokeo hata kama yatachelewa, nitakaa kwenye mchakato wa kufikisha maono ya TLG ♥
LikeLike
Safi sana, kaa humo, kuna mengi makubwa na mazuri.
LikeLike
Juhudi na akili nitaweka ila nitatoboa kwa kuwa na msimamo katika kile ambacho nimeshaanza kukifanya ili mradi ni sahihi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nimeamua kusimama na jambo moja kwanza mpaka nione matokeo na si kuhangaika na mambo mengi ambayo yatanupa matokei hafifu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni sawa hatupaswi kukata tamaa mapema ni kuvumilia hadi tupate matokeo tusirukeruke
LikeLike
Matokeo mazuri yanakuja, ni swala la muda tu.
LikeLike
Nguvu zangu haziwezi kupotea Bure…nitang’ang’ania Hadi mwisho.
LikeLike
Tuendelee kuweka hizi juhudi, hazipotei.
LikeLike
….hata nikiwa katika mwendo mkali nitakuwa nina FOCUS kwenye kile nilichoamua kukifanya.
LikeLike
Kasi na fokasi ni mapacha muhimu kwenda nao ili kufanya makubwa.
LikeLike
Kufanikiwa kunaletwa ma kudumu katika jabo kwa ubora.
LikeLike
Uwekezaji na muda vinahitajika.
LikeLike
Msimamo ni muhimu sana kwenye maisha.
LikeLike
Hakuna lolote kubwa linalozaliwa bila msimamo.
LikeLike
Nitaendelea kufanya ninachofanya mpaka nione matokeo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Siko tayari kupotezea nguvu niliyoiwekeza
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hakuna juhudi zinazokwenda Bure, tukae kwenye mchakato
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato haina mbadala.
LikeLike
Usikubali kupoteza kile ulichoanzisha, thamini nguvu ulizotumia kujenga kile ulichonacho.
LikeLike
Kila nguvu uliyokwishaweka ni uwekezaji mkubwa, usikubali kupoteza.
LikeLike
Ni sahihi kupoteza juhudi na jitihada za nyuma hupoteza zaidi
LikeLike
Nitaendeleabkuweka juhudi kwenye kile ninachofanya, bila kurudi nyuma
LikeLike
Pamoja na changamoto ninazokutana nazo, nitaendelea kuipambania brand yangu ya Beatus animal feed,na njia pekee ni kuwa na msimamo kwa kukaa kwenye mchakato,sitakuwa tayari kuacha kazi ambayo nimeisha ianzisha.
LikeLike
Hata Kama sioni matokeo kwa Sasa kwa chochote ninachofanya, sitakubali kuishia njiani.
LikeLike
Nitang’ang’ana hadi nione matokeo kwa sababu najua kuwa nikikata tamaa itabidi nianze upya
LikeLike
Vizuri, usipoteze kazi ambayo umeshaiweka.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimeshajua tofauti ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
kwa kuwa nataka kufanikiwa nitakuwa na MSIMAMO katika kufanya jambo moja kwa muda mrefu bila kuhamisha hamisha hamisha juhudi kwenye mambo mengi.
Nitakaa kwenye MCHAKATO WA KUFANYA JAMBO KWA MSIMAMO NA KWA KURUDIA RUDIA NA KWA MUDA MREFU BILA KUACHA.
LikeLike
TUKAE KWENYE MCHAKATO.
LikeLike