2990; Usalama na Uhuru.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu huwa tuna mahitaji mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali za maisha yetu.
Hitaji la chini na la msingi kabisa huwa ni usalama.
Huwa tunapenda kuwa na uhakika kwamba maisha yetu yanaweza kuendelea bila ya kikwazo chochote.
Hitaji la juu kabisa ni uhuru.
Huwa tunapenda kuwa huru, kuyaendesha maisha yetu kwa namna tunavyotaka sisi wenyewe.
Lakini kwa bahati mbaya sana, usalama na uhuru ni vitu ambavyo huwa haviendi pamoja.
Ni asili ya maisha kwamba ukitaka kuwa salama kabisa huwezi kuwa huru na ukitaka uhuru kamili, lazima uwe tayari kupoteza usalama.
Uhuru unahusisha kuchukua hatua za hatari, ambazo zina nafasi kubwa ya kushindwa na zinaondoa uhakika wa usalama.
Kwa kuwa uhuru unahusisha hatari, hatari hizo zinaondoa hali ya usalama.
Usalama unahusisha kuwapa wengine jukumu la kuchukua hatua za hatari ambazo hazikuathiri wewe moja kwa moja.
Japo utakuwa salama, lakini manufaa utakayopata ni madogo sana ukilinganisha na wale wanaochukua hatua za hatari.
Usalama ni kuwapa wengine jukumu la kuyaendesha maisha yako, ambapo mafanikio yako siyo kipaumbele kikubwa kwao.
Kuna usalama kwenye kuendesha biashara ndogo, ambayo upo mwenyewe na wewe ndiyo kila kitu. Huna wafanyakazi wa kukusumbua na unawahudumia wateja wako wachache vizuri.
Usalama huo unakuwa kikwazo kwako kukua zaidi kibiashara na kuingiza kipato kikubwa.
Uhuru wa kibiashara unatokana na kukuza biashara kwa viwango vya juu, ambalo linahusisha kuwa na watu wengi, ambao pia wanakuja na changamoto zao. Hilo linakuwa na hatari mbalimbali ambazo zinapunguza sana usalama.
Tukirudi kwenye uhalisia, akili zetu huwa zinakimbilia zaidi kwenye usalama. Ndivyo asili ilivyotujenga ili kuhakikisha tunaendeleza maisha yetu.
Lakini uhalisia ni kwamba hakuna usalama wa asilimia 100. Kila kitu kina hatari zake.
Chochote tunachoweza kuona kina usalama, ukichunguza kwa makini, utagundua bado kina hatari ndani yake.
Watu hudhani ajira ni njia salama ya kuingiza kipato, lakini ajira zina hatari ya mtu kupoteza, tena kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.
Kadhalika biashara ndogo, hatari ya kushindwa bado ipo, licha ya mtu kudhibiti kila kitu peke yake.
Hivyo basi, tunapaswa kuacha kujidanganya na usalama na kwenda kwenye uhuru moja kwa moja.
Tupambanie zaidi uhuru badala ya kuhangaika na usalama.
Tukazane kupata udhibiti badala ya kuwapa wengine udhibiti huo.
Uzuri ni kwamba, ukiwa na uhuru mkubwa, unakuwa na kiwango kizuri cha usalama pia, japo siyo kwa asilimia 100, kwa sababu hatari haziepukiki.
Ni lazima ujue na kukubali kwamba maisha ya mafanikio yameambatana na hatari mara zote.
Kama huwezi kuvumilia hatari yoyote, huwezi pia kuyavumilia mafanikio makubwa.
Lakini sasa, hata usipofanikiwa, bado unakuwa kwenye hatari, tena wakati mwingine hatari ambayo ni kubwa zaidi.
Tukishajihakikishia chakula, mavazi na malazi, kinachofuata kinapaswa kuwa ni kupambana kujijengea uhuru mkubwa.
Japo hilo litatuweka kwenye hatari, lakini hakuna kisichokuwa na hatari kwenye maisha.
Kitendo tu cha kuwa hai, ni hatari ya kifo, unatembea na hatari ya kifo muda wote.
Hivyo tunapaswa kuacha kuhangaika sana na usalama na badala yake tuhangaike zaidi na uhuru.
Badala ya kukazana kuwa salama, kazana kuwa huru.
Usalama ni kulinda goli usifungwe, maana yake huwezi kupata ushindi, lakini pia una hatari ya kufungwa.
Uhuru ni kushambulia ili ufunge goli, unakuwa kwenye hatari ya kufungwa, lakini pia una nafasi ya kushinda.
Uhuru utakuweka salama, lakini usalama hauwezi kukuweka huru.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
sitalinda goli ili nisifungwe(usalama),,,nitapambania kufunga goli huku nikiwa na hatari ya kufungwa (uhuru).
usalama unakupa comfort zone ambayo n hatari
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitapambana kuwa huru,huo ndiyo usalama tosha kwangu..
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Uhuru utakuweka salama lakini usalama hauwezi kukuweka huru.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Ili nifanikiwe natakiwa kushambulia zaidi,kuliko kulinda goli.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Asante kocha,ntajitahidi kuwa na uhuru ili nishambulie na kufunga goli sio usalama ambao siwezi kuwa na uhuru.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Uhuru utaniweka salama, lakini usalama hautaniweka huru. Uhuru utaniweka huru na salama pia.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Uhuru ni kitu chenye gharama kubwa sana kulikoni tunavyofikiria
LikeLike
Na bila kulipa gharama hiyo kubwa hatuwezi kuupata.
LikeLike
Asante sana Kocha upambanie uhuru
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Uhuru utaniweka salama, lakini usalama hautaniweka huru.
LikeLike
Sahihi
LikeLike
Ahsante sana kocha nitahakikisha nautafuta uhuru bila kuogopa Usalama utakuaje.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni lazima ujue na kukubali kwamba maisha ya mafanikio yameambatana na hatari mara zote.
Kama huwezi kuvumilia hatari yoyote, huwezi pia kuyavumilia mafanikio makubwa.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Asante Kocha,
Nakazana kuwa huru na sio kutafuta usalama
Nakazana kufunga magoli maana uwezekano wa kushinda ni mkubwa na sio kulinda goli ili nisifunge maana hata nikilinda vipi uwezekano wa kufungwa ni mkubwa.
Natafuta uhuru kwaani uhuru utaniweka salama lakini usalama hautaniweka huru.
Asante
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Uhuru utakuweka salama, lakini usalama hauwezi kukuweka huru.
Kwenye maisha tunapaswa kushambulia muda wote na siyo kulinda
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nipo tayari kuchukua hatua zenye hatari Ili kuwa huru! SIOGOPI kushambulia!
LikeLike
Shambulia sana.
LikeLike
Ukilinda goli unakaribisha adui golini kwako na hivyo kuna uwezekano wa kufungwa kwa urahisi.
LikeLike
Kweli, unaposhambulia, unafanya adui ndiyo ajilinde, hivyo hawezi kukushambulia sana.
LikeLike
Ni lazima ujue na kukubali kwamba maisha ya mafanikio yameambatana na hatari mara zote.
Kama huwezi kuvumilia hatari yoyote, huwezi pia kuyavumilia mafanikio makubwa.
Lakini sasa, hata usipofanikiwa, bado unakuwa kwenye hatari, tena wakati mwingine hatari ambayo ni kubwa zaidi.
Ahsante Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna chenye usalama 100% Duniani, chochote tunachofanya kina hatari ndani yake badala ya kutafuta usalama tutafute uhuru mkubwa
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muhimu kushambulia ili kufunga siyo kujilinda,Asante Kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Usalama ndio unahubiriwa na chaguo la kundi kubwa, lakini tunafahamu wazi ya kwamba uhuru ndio njia ya kutufikisha kule tunakolenga kwenda.
nachagua uhuru!
LikeLike
Wanaotaka kuwatawala watu wanawaahidi usalama, ili wachukue uhuru wao.
LikeLike
Mumbe ni bora kuwa huru kuliko kulinda usalama ni bora kushambulia kuliko kulinda goli maana una hatari ya kufungwa tu
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kwa kuwa uhuru na usalama haviendi pamoja, ni heri kuwa huru kuliko kuwa salama. Kuna usalama katika uhuru lakini hakuna uhuru katikaq usalama
LikeLike
Hakika
LikeLike
anza na usalama, kisha uhuru
LikeLike
We mzee hii haiko sawa. Komaa na UHURU kuliko USALAMA. UHURU utakupa usalama japo sio asilimia 100 Ila USALAA hautakupa UHURU abadani.
LikeLike
Imekaa kinyume.
LikeLike
Asante Sana Kocha kwa makala ya leo. ‘UHURU UTAKUWEKA SALAMA LAKINI USALAMA HAUTAKUWEKA HURU..’
Nadhani woga ndiyo inatupeleka kwenye kupambania usalama.
Nitaweka mbele maslahi ya Uhuru badala ya Usalama.
LikeLike
👍
LikeLike
Asante Kocha ni heri nipambane nifikie uhuru wa maisha kuliko usalama.
LikeLike
Ukiwa huru unakuwa salama zaidi.
LikeLike