3005; Wewe na biashara.
Rafiki yangu mpendwa,
Changamoto nyingi ambazo watu wanakutana nazo kwenye biashara, chanzo chake ni watu kushindwa kujitofautisha na biashara zao.
Kwa sababu wanamiliki biashara, basi wanadhani biashara hizo ni wao na hivyo kufanya chochote wanachojisikia kwenye biashara hizo.
Hizo fikra kwamba wao ndiyo biashara na wanaweza kufanya chochote wanachotaka zimekuwa kikwazo kikubwa sana kwa watu kufanikiwa kwenye biashara.
Kwani watu hufanya maamuzi kwa tamaa zao wenyewe, ambayo huwa na madhara makubwa kwenye biashara.
Eneo ambalo biashara zimekuwa zinaathirika sana ni eneo la fedha.
Wamiliki wa biashara hudhani kwa kuwa biashara ni zao, basi fedha zote zilizopo kwenye biashara ni zao pia na wanaweza kuzitumia watakavyo.
Hapo ndipo matatizo makubwa huanzia na kupelekea biashara kushindwa vibaya sana.
Wewe na biashara yako ni viumbe wawili tofauti kabisa.
Hata serikali, kisheria inatambua biashara kama kitu kinachojitegemea.
Kudhani wewe na biashara yako ni kitu kimoja ni kuibemenda, kuidumaza ishindwe kukua.
Uhusiano wako na biashara ni huu; wewe umeikopesha biashara mtaji na biashara inakulipa mtaji huo kwa faida inayotengenezwa.
Hiyo ina maana kwamba, fedha pekee unayoweza kuitoa kwenye biashara ni faida.
Na hapo ni kama unaweza kukokotoa faida kwa uhakika.
Tofauti na hapo, kama unatoa fedha kwenye biashara kiholela, jua tu hiyo biashara itakufa, hakuna namna itaweza kutoboa.
Biashara yoyote ile inayoendeshwa kwa misingi sahihi, ambayo inauza kitu chenye uhitaji kwa watu, ina nafasi kubwa ya kufanikiwa kama itafanywa kwa umakini, kama taratibu zote za kuendesha biashara zitafuatwa.
Maeneo muhimu ya kuzingatia ili biashara iweze kufanikiwa ni kuzijua namba za biashara na kuzisimamia kwa uhakika. Kuwa na mfuno bora wa kuiendesha biashara. Kujenga timu imara ya kuendesha biashara na kufanya mauzo makubwa.
Fedha ya kwenye biashara inapaswa kuheshimiwa sana na kila mtu, haipaswi kuchukuliwa kiholela, hata na mmiliki wa biashara.
Muda na juhudi za kazi zinapaswa kuwekwa na kila anayehusika kwenye biashara. Watu hawapaswi kufanya vitu vile wanavyojisikia wenyewe.
Unajua kwa nini watu wanaotoka kwenye ajira na kwenda kuanza biashara zao wenyewe huwa wanashindwa sana kibiashara?
Kwa sababu wanashindwa kuhamisha nidhamu ya kwenye ajira kupeleka kwenye biashara.
Wakati kwenye ajira walikuwa wanawahi kazini kila siku bila kuchelewa wala kukosa, kwenye biashara zao wanafika muda wanaotaka na wakiwa na changamoto kidogo hawaendi kabisa.
Wakati watu wakiwa kwenye ajira na hawana fedha, hawawezi kuchukua fedha ya taasisi vile wanavyojisikia wao wenyewe. Lakini kwenye biashara zao, wakiwa na shida kidogo tu ya fedha, wanachukua kwenye biashara bila kujali.
Vifo vya biashara nyingi vinatokana na uyatima wa biashara.
Yaani biashara inakuwa kama mtoto yatima, ambaye hakuna anayemjali.
Kuanzia mmiliki mwenyewe ambaye anafanya kila kitu jinsi anavyojisikia, mpaka kwa wafanyakazi ambao wanatafuta njia ya kupata zaidi kwa kufanya kidogo.
Kama unamiliki biashara na unatoa fedha kwenye biashara hiyo vile unavyojisikia haitaweza kutoboa.
Kama unamiliki biashara na unafungua na kufunga vile unavyojisikia wewe ni tatizo kubwa.
Kama unamiliki biashara yenye wafanyakazi na unawaacha wafanye vile wanavyojisikia wao, kifo cha biashara hiyo hakiepukiki.
Ili biashara ifanikiwe, inapaswa kuheshimiwa sana na kila aliyepo kwenye biashara hiyo, kuanzia mmiliki, wafanyakazi mpaka wateja.
Biashara ambayo haiheshimiwi itakufa tu.
Serikali zimekuwa na njia za kulazimisha watu waziheshimu biashara ili iweze kukusanya kodi yake, lakini watu wamekuwa na njia za kukwepa hilo.
Wanafanya kwa nia njema ya kupungua gharama za biashara, lakini wanaishia kuziumiza biashara kwa sababu hazina mtetezi.
Wanafanya vile wanavyotaka na kujisikia kitu kinachopelekea biashara hizo kufa.
Kwenye programu yetu ya bilionea mafunzoni, mimi Kocha wako nimechagu kuwa mtetezi wa biashara yako, dhidi yako wewe mwenyewe.
Wajibu wangu ni kuhakikisha hiyo biashara yako inaheshimiwa na kila mtu, kwa kuanza na wewe mwenyewe kisha wote wanaohusika.
Ninakuwa mkali sana kwako wewe na kwa wengine wote ambao wanaihujumu biashara kwa kwenda kinyume na misingi sahihi ya kuiendesha biashara.
Nahakikisha misingi yote inazingatiwa na kila aliyepo kwenye biashara.
Bila hivyo, hakuna biashara itakayotoboa.
Ichukulie biashara yako kama ajira kwenye kampuni kubwa kabisa nchini au hata duniani.
Chukulia wewe umeajiriwa pale kama mkurugenzi mkuu (CEO) na wajibu wako ni kuleta matokeo bora.
Kama huleti matokeo bora, bodi ya wakurugenzi itakufukuza muda wowote.
Kama mwajiriwa wa kampuni kubwa, huwezi kufanya mambo vile unavyojisikia wewe, utafuata misingi na taratibu zilizopo.
Huwezi kuamua lini uende na lini usiende kazini.
Huwezi kujichukulia fedha kwenye biashara vile unavyotaka wewe.
Na huwezi kumwajiri mtoto wa shangazi yako kwa sababu hana kazi ya kufanya.
Sijui unaipata picha hapo?
Hivi ndivyo tunavyokwenda kwenye programu yetu ya Bilionea Mafunzoni;
1. Wewe ndiye mkurugenzi mkuu (CEO) wa biashara yako ambaye umeajiriwa na biashara kwa lengo la kuifikisha kwenye ubilionea.
2. Klabu yako ya Bilionea Mafunzoni ndiyo bodi ya wakurugenzi kwenye biashara yako, ambayo inahakikisha biashara inaendeshwa kwa misingi sahihi na malengo yaliyopo yanafanyiwa kazi.
3. Kocha ndiye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kwenye biashara yako, ambaye pamoja na bodi wanayo mamlaka ya kukuwajibisha wewe mkurugenzi mkuu wa biashara kwa yale yanayoendelea.
Huu ni uwajibikaji wa juu kabisa kwenye biashara ambao ukizingatiwa lazima biashara itakuwa na mafanikio makubwa.
Pokea hili kwa mikono miwili na kulifurahia kwa sababu linakuzuia wewe mwenyewe usiwe kikwazo kwa biashara yako.
Na kama unaona ni jambo usiloweza, kwa kuona ni kukubali kuteswa kwa ajili ya biashara yako mwenyewe, basi jua hiyo biashara haina maisha marefu.
Ukiwa na bahati sana utaenda nayo kwa udumavu katika kipindi cha uhai wako.
Lakini baada ya kifo chako, hata kabla ya arobaini yako, shida zitakuwa zimeanza kujitokeza na biashara kukufuata kaburini.
Hicho ni kitu ambacho hatutakiruhusu kwenye programu hii ya Bilionea Mafunzoni.
Tutakuondoa haraka sana kama huwezi kuwa na nidhamu hii ya msingi kabisa inayohitajika ili biashara yako iweze kufanikiwa.
Kuanzia sasa, futa dhana kwamba wewe ni mmiliki wa biashara na unaweza kufanya utakavyo.
Kisha jenga dhana kwamba wewe ni mwajiriwa kwenye biashara kama mkurugenzi mkuu na unapaswa kufuata taratibu zote za kuiendesha biashara hiyo kwa mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha, ni kweli nilikosa uwajibikaji wa kuendesha biashara kwenye misingi sahihi. Sasa mimi ni mwajiriwa wa TLG nitafuata misingi sahihi
LikeLike
Vizuri kwa kujua wapi makosa yamefanyika, sasa ni wakati wa kufanya kwa usahihi.
LikeLike
Mimi na biashara ni viumbe viwili tofauti,napaswa kuindeshesha hii biashara kwa misingi na taratibu zinazopaswa ili kuweza kuikuza biashara hata nikifa biashara yangu isinifuate kaburini bali iendelee kuishi kwa wale nitakaowaacha na kuwanufaisha pia.
Sina haki ya kuchukua fedha au kuendesha biashara vile ninavyojisikia mimi kwani mimi ni mwaajiriwa tu wa kwenye hi biashara na jukumu langu kubwa ni kuhakikisha biashara hii inafika kwenye ubilionea.
Asante sana kocha kwa kuchagua kuwa mgurugenzi wa bodi ya kuniwajibisha ili biashara yangu isife.
LikeLike
Karibu sana, tukae humu.
LikeLike
Asante Kocha,kuanzia sasa mimi ni mwajiriwa kama Ceo wa kampuni ya Digola traders,na nitafuata misingi yote ya ufanyaji kazi. Na nitawajibika kwenye Bodi ya Wakurugenzi.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ni Makala bora sana kweli tunahitaji kuwajibika kwenye maisha kiujumla ili biashara zetu ziweze kwenda kama mifumo mingine ya kampuni kubwa au mashirika makubwa ya kiserikali ili kuwa na uwajibikaji mkubwa. Nitawajibika kwa bodi ya Wakurugenzi.
LikeLike
Vizuri sana
LikeLike
Asante kocha Kwa ujumbe huu
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Mimi na Biashara ni vitu viwili tofauti. Pamoja na Biashara kuwa ni ya kwangu bado nahitajika kuwa na nidhamu ya hali ya juu. Bodi ya Wakuregenzi ya Bilionea mafunzoni itachangia juu ya hili
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha, mpaka sasa hivi sijaweza kujitenga mimi na biashara yangu. Na hili nimekuwa naliona waziwazi, maana naweza kutoa hela ya biashara muda wowote ninapojisikia.
NInabadilika.
LikeLike
Utalazimika kubadilika.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimeliona hilo, Mimi sasa ni mwajiriwa, CEO wa biashara yangu. Nitaiheshimu sana.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Sana kocha kwamakala bola kabisa. Ninaahidi kuyatekeleza kikamilifu maagizo hayo kwa kuhakikisha Mimi na biashara yangu tunaendelea kuwa vitu viwili tofauti kabisa.
Asante
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
hapa ndipo patamu, tumeendesha biashara hizi kwa mazoea kiasi hata unapoajiri bado unaikosea biashara
LikeLike
Kabisa, lazima tubadilike.
LikeLike
Wewe ndiye mkurugenzi mkuu (CEO) wa biashara yako ambaye umeajiriwa na biashara kwa lengo la kuifikisha kwenye ubilionea.
Klabu yako ya Bilionea Mafunzoni ndiyo bodi ya wakurugenzi kwenye biashara yako, ambayo inahakikisha biashara inaendeshwa kwa misingi sahihi na malengo yaliyopo yanafanyiwa kazi.
Kocha ndiye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kwenye biashara yako, ambaye pamoja na bodi wanayo mamlaka ya kukuwajibisha wewe mkurugenzi mkuu wa biashara kwa yale yanayoendelea.
LikeLike
Hivyo ndivyo tutakavyokwenda.
LikeLike
Ahsante Sana kocha (mwenyekiti mkuu wa biashara yangu). Nimefurahi sana kusoma makala hii, hakika ni bahati kubwa Sana kwangu kusoma makala hii.
✅🤗🤗💥
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mkurugenzi wa biashara sio biashara. Mimi nasimama kama Mkurugenzi.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mimi na biashara ni vitu viwili tofauti, natakiwa nijitofautishe na biashara yangu
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mimi ni mwajiriwa wa biashara yangu
Nimeelewa sana kocha
Asante
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mimi ni mwajiriwa wa biashara yangu nimeelewa sana kocha
Asante
LikeLike
Asante sana kocha kwa maelekezo haya. Kazi yangu kama mkurugenzi ni kutii mamlaka zilizopo ambazo ni bodi ya wakurugenzi (clabu) na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (kocha).
LikeLike
Kabisa na hivyo ndivyo biashara itakavyoweza kukua.
LikeLike
Mimi ni Mwajiriwa kwenye biashara yangu, Fedha ya kwenye biashara inapaswa kuheshimiwa na kila mtu na haipaswi kuchukuliwa kiholela hata na mmiliki wa biashara.
kwenye chati ya uongozi wa biashara yangu:-
Mimi ni CEO mwenye malengo ya kuufikia ubilionea
Club ya Bilionea Mafunzoni ndio Bodi ya wakurugrnzi
Kocha ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mimi si biashara yangu,imeniajiri niiheshimu biashara.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Fedha ya kwenye biashara inatakiwa kuheshimiwa na kila mtu, Daina nitahakikisha fedha hii ina heshimiwa.
LikeLike
Safi.
LikeLike
Kuanzia sasa, futa dhana kwamba wewe ni mmiliki wa biashara na unaweza kufanya utakavyo.
Kisha jenga dhana kwamba wewe ni mwajiriwa kwenye biashara kama mkurugenzi mkuu na unapaswa kufuata taratibu zote za kuiendesha biashara hiyo kwa mafanikio makubwa.
Ahsante sana Kocha, kuanzia sasa nabadilika.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wanafamilia na marafiki wakiona una pesa wanajua wanaweza kupewa watakavyo.
LikeLike
Wanadhani zote ni zako, wakati ni mali ya biashara.
LikeLike
Mm ni Mwajiriwa namba moja kwenye biashara, kama Sita weka kazi na nidhamu biashara yangu itakuwa mapema sana
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mimi ni CEO wa biashara yangu,pia nitaendesha biashara hii kwa misingi sahihi ninayojifunza ktk bilionea mafunzoni
LikeLike
Safi
LikeLike
Mimi ni mwajiriwa kama mkurugenzi mkuu wa biashara yangu. Napaswa kufuata kanuni zote za biashara Ili biashara hii ifanikiwe.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimepona Kwa somo la Leo
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha, HII nitaiita 3005/24/023 hii imeniamusha,huwa naieshimu na kuijali sana kazi ya mwajiri wangu kwa sasa karibia miaka 18,kwa kutambua kuwa mimi sasa ni mwajiriwa wa Beatus animal feed ninalo jukumu zito la kutekeleza.
LikeLike
Hamisha heshima ya mwajiri kwenda kwenye biashara na utafanya makubwa sana.
LikeLike
Asante kocha
Mimi ni mwajiriwa nitafuata taratibu zote Kama mkurugenzi sio mmiliki tena wa biashara
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha
Mimi Nitakuwa ni mwajiriwa tu kama Mkurugenzi wa kampuni yangu na nitafuata misingi yote ya kazi iliyowekwa. Nidhamu yangu itakuwa juu Na nitawajibika kwenye Bodi ya Wakurugenzi.
Biashara itajitegemea na kustawi na sintaruhusu ife
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Tunarudi kwenye msingi mkuu NIDHAMU,
ukiongeza na nidhamu kali ya kuamua na kufanya yale tu yanayo kusongeza mbele zaidi ya leo la ubilionea
LikeLike
Nidhamu haikwepeki.
LikeLike
Kuanzia leo mimi ni mwajiriwa wa MaxQuality Consultants
Wajibu wangu ni kwenda kazini kila siku asubuhi na mapema kutekeleza majukumu ya mwajiri ambayo ni kusaka kukamilisha na kuhudumia watu kwenye eneo la uhasibu na Kodi, kufikia wateja 100 kwa mwaka huu, 25 wageuzwe kuwa wateja wa kulipia Tshs 100k, kila mwezi na 75 wawe wateja wa mara moja na walipie Tshs 400k kila mmoja.
Naahidi kulitimiza hili kama CEO
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mimi Ni mwajiriwa wa
TIJARA SUNLAND INVESTMENT ( TSI ), hivyo mtazamo wa kujichukulia Kama mmiliki umekwisha. Nihaheshimu fedha ya biashara. Maana hapo ndipo manufaa ya biashara yangu.
LikeLike
Vizuri, zingatia sana hili.
LikeLike
Asante kocha kwa kujitolea kuwa mtetezi wa biashara zetu. Tumekusikia na hatutakuangusha.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante, hakika mimi siyo biashara yangu ila ni mwajiriwa na muda wowote nikizingua nitafukuzwa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante Sana ,
Mimi na biashara ni viumbe wawili tofauti, hili nalijua siku nyingi lakini sijaweza kulifanya kwa asilimia 100, nachukua hela Dukani wananiandika, nikipata mshahara nalipa. Hitzi ndogondogo najitahidi kulipa lakini nikichukua kubwa nashindwa. Mfano tulichukua na Mr kama millioni tukapeleka kwenye ujenzi, Ile hela tumeshindwa kulipa hata sijui kwanini.
Ila Leo nimejua kwamba Mimi ni mwajiriwa wa biashara kama mkurugenzi, wanaclub ni bodi ya wakurugenzi na kocha ni mwenyekiti wa bodi.
Nitawajibishwa wakati wowote ukaguzi ukipita nikaotekana utendaji wangu mbovu.
Asante Sana kocha
LikeLike
Mwarobaini wa hilo unakuja.
LikeLike
Asante Sana ,
Mimi na biashara ni viumbe wawili tofauti
I Mimi ni mwajiriwa wa biashara kama mkurugenzi, wanaclub ni bodi ya wakurugenzi na kocha ni mwenyekiti wa bodi.
Nitawajibishwa wakati wowote ukaguzi ukipita nikaotekana utendaji wangu mbovu.
Asante Sana kocha
LikeLike
Vizuri sana,
Zingatia haya.
LikeLike
Kwa muda mrefu nimeihujumu biashara na kushindwa kujitofautisha nayo.
Nakwenda Sasa kuweka nidhamu na kujiheshimu biashara, sipo tayari kufukuzwa kazi ya ukurugenzi kama nitashindwa kufanya majukumu yangu na kuheshimu biashara, hivyo nakwenda kujitoa hasa tangu Leo na Kisha kuhakikisha wafanyakazi na hata wateja wanaiga mfano Bora kwangu Kwa kuheshimu sana biashara.
LikeLike
Safi sana.
Tukae humu.
LikeLike
Asante Kocha kwa kunikumbusha. Mimi ni Mwajiriwa wa AMSHAUWEZO CONSULTANTS. Nitahakikisha naiendesha biashara hii kwa misingi sahihi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike