3006; Haifanyiki.
Rafiki yangu mpendwa,
Asili ina kanuni ya visababishi na matokeo.
Kanuni hiyo inasema kwa kila matokeo unayoyaona, kuna visababishi vyake.
Hivyo basi, kama kuna matokeo ulitegemea kuyaona ila hayaonekani, ni kwamba hakuna visababishi.
Waswahili wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa.
Mambo hayatokei tu kwa bahati au ajali, bali huwa yanasababishwa.
Na hapo ndipo nataka kuzungumza vizuri na wewe, ili uweze kukaa upande sawa.
Umekuwa unajifanganya sana na pia umekuwa unadanganywa na wengine juu ya hatua wanazochukua.
Unajiambia umefanya kila kitu lakini matokeo hayaji kama ulivyotegemea.
Watu unaojihusisha nao wanakuambia wamefanya kila kitu ila hawapati matokeo.
Jibu moja rahisi kabisa ni hili; hujafanya na hawajafanya.
Wala usitake kuumiza kichwa kwamba kwa nini umefanya au wamefanya na matokeo hayaji.
Jua bila ya shaka yoyote kwamba chochote kilichopaswa kufanyika ili kuzalisha matokeo, hakijafanyika.
Matokeo yanazalishwa na hatua ambazo zimechukuliwa.
Ukienda kwenye shamba na kukuta mahindi yamestawi vizuri, huhitaji hata mtu akuambia nini kimetokea.
Unajua kabisa kuna mbegu za mahindi zilipandwa hapo, zikapata maji, mbolea na kupaliliwa vizuri.
Na kama kuna shamba la pembeni ambalo halina mahindi ya aina hiyo, unajua kabisa kwamba kuna vitu havijafanyika. Labda mbegu hazikupandwa, au maji hayakupatikana au mbolea au hayakupaliliwa.
Kama hakuna matokeo, kuna sababu hizi nne;
Moja ni kitu hakijafanyika kabisa.
Mbili ni kitu hakijafanyika kwa wingi.
Tatu ni kitu hakijafanyika kwa usahihi.
Na nne ni kitu hakijafanyika kwa msimamo.
Kitu chochote kikifanyika kwa wingi, usahihi na msimamo, lazima kitazalisha matokeo yanayotegemewa.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye fedha.
Fedha ni matokeo, ili uzipate lazima kuwe na visababishi.
Lazima ufanye mambo ambayo yanavuta fedha kuja kwako.
Na lazima uyafanye kwa wingi, usahihi na msimamo ndiyo matokeo yaweze kuonekana, yaani fedha ziweze kuja kwako.
Changamoto kubwa kwenye maisha na inayowazuia watu wengi wasifanikiwe ni kutaka matokeo bila ya visababishi.
Watu wanahangaika sana kutafuta njia za mkato za kupata kile wanachotaka bila ya kuweka juhudi.
Hakuna kitu kama hicho, asili haina njia za mkato. Lazima uweke visababishi ndiyo upate matokeo. Na siyo tu kuweka mara moja, bali kuweka kwa wingi, usahihi na msimamo.
Tuchukulie mfano kwenye mauzo, watu wamekuwa wanalalamika kwamba wanaweka juhudi sana lakini mauzo hayapatikani.
Kwamba wanapiga simu sana na kukutana na wateja, ila hawakubali kununua.
Mpaka sasa tayari unalijua jibu, kuna kitu hakifanyiki.
Labda juhudi hizo haziwekwi kwa wingi na kama zinawekwa kwa wingi basi siyo kwa usahihi na kwa msimamo.
Ukianzia hapo utaweza kuona nini hakifanyiki na ukiwezesha kifanyike matokeo yatakuja.
Asili inajiendesha kwa kanuni zake yenyewe.
Kama hutazijua na kuzifuata kanuni hizo, utahangaika sana lakini hutapata matokeo unayotarajia kupata.
Kama matokeo hayapatikani, jua kuna vitu havifanyiki.
Jua ni vitu gani na uvifanye ili uweze kuzalisha matokeo unayoyataka.
Tusijidanganye wala kukubali kudanganywa kirahisi.
Matokeo yanatengenezwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante kocha.
Nitafanya kwa usahihi, wingi na kwa msimamo. Ili nipate matokeo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,nitajitahidi kuweka nguvu kwenye mchakato ili niweze kupata matokeo,bidii,kujituma na kufanya kwa usahihi ili niweze kupata mafanikio.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitafanya kwa msimamo na usahihi bila kuacha hata siku moja katika biashara yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ahsnate kocha, nitahakikisha nafanya vitu vinavyohitajika kwaajili ya kufanya mauzo zaidi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kufanya Kwa usahihi Kwa wingi na msimamo ndiyo chanzo Cha mafanikio.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wingi, usahihi na msimamo.
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Kanuni za mafanikio.
Fanya kwa usahihi.
Kwa wingi
Na kwa msimamo
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asili Haidanganyi matokeo yanatengenezwa
Asante
LikeLike
Hakika, hakuna kutafuta mchawi.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri. Ni kweli kabisa kuwa jambo lolote likifanyika kwa usahihi matokeo yaliyotarajiwa ni lazima.
LikeLike
Ni lazima.
LikeLike
Asante Kocha,
Sitajidanganganya nitafanya kwa usahihi, wingi na kwa msimamo ndiyo nitarajie matokeo chanya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mmmh! Nikweli sijafanya Kwa usahihi
LikeLike
Fanya kwa usahihi.
LikeLike
Wingi, Usahihi na Msimamo
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Kama hakuna matokeo, kuna sababu hizi nne;
Moja ni kitu hakijafanyika kabisa.
Mbili ni kitu hakijafanyika kwa wingi.
Tatu ni kitu hakijafanyika kwa usahihi.
Na nne ni kitu hakijafanyika kwa msimamo.
Kitu chochote kikifanyika kwa wingi, usahihi na msimamo, lazima kitazalisha matokeo yanayotegemewa.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Ukweli ndiyo huo.
LikeLike
ukiona ujapata unakitaka
hakijafanyika kabisa,
fanya kwa wingi,
fanya kwa msimamo na
fanya kwa usahihi
nimeichukua kocha asante
LikeLike
Fanya.
LikeLike
Sipati ninachotaka kwa sababu sifanyi kwa usahihi, au naweka juhudi kidogo, mimi ni mzembe nahitaji kujibadili
LikeLike
Fanya.
LikeLike
Kama hakuna matokeo, kuna sababu hizi nne;
Moja ni kitu hakijafanyika kabisa.
Mbili ni kitu hakijafanyika kwa wingi.
Tatu ni kitu hakijafanyika kwa usahihi.
Na nne ni kitu hakijafanyika kwa msimamo.
Kitu chochote kikifanyika kwa wingi, usahihi na msimamo, lazima kitazalisha matokeo
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Matokeo yanatengenezwa kwa kufuata mchakato. Kwenye biashara yangu juhudi nyingi tumekuwa tunaweka, ila tumekuwa tunakose kwenye kuwafuatilia wateja kwenye ahadi, hili ni jambo ambalo naenda kuliwekea mkazo kuanzia wiki ijayo.
Pia nitakuwa nasikiliza simu za mauzo za msakaji wangu ili kujua nini kinaendelea na kuto amrejesho kwake wa nini aboreshe ili tuweze kuongeza mauzo kwenye biashara
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kweli kabisa. Bila visa banishing hakuna matokeo. Huwezi kuvuna mahali ambapo hukupanda.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kama hakuna matokeo, kuna sababu hizi nne;
Moja ni kitu hakijafanyika kabisa.
Mbili ni kitu hakijafanyika kwa wingi.
Tatu ni kitu hakijafanyika kwa usahihi.
Na nne ni kitu hakijafanyika kwa msimamo.
Kitu chochote kikifanyika kwa wingi, usahihi na msimamo, lazima kitazalisha matokeo yanayotegemewa.
LikeLike
Tunapoona matokeo hayaji, tuanzie hapa.
LikeLike
Itoshe tu kusema MATOKEO YANATENEZWA “Asante sana kocha.
LikeLike
Hakika, kama matokeo hayapo, hayajatengenezwa.
LikeLike
Kama Hakuna matokeo jibu Ni moja tu Kuna vitu havifanyiki, na Kama vikifanyika havifanyiki kwa wingi na kwa msimamo.
Asante Sana kocha kwa makala
LikeLike
Matokeo hayadanganyi.
LikeLike