3008; Shughuli muhimu zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna shughuli nyingi sana unazojihusisha nazo kwenye maisha yako ya kila siku.
Lakini shughuli iliyo muhimu zaidi kuliko zote ni ile ya kujiingizia kipato.
Hiyo ndiyo shughuli muhimu kwa sababu ndiyo msingi mkuu wa maisha yako.
Kuingiza kipato ndiyo msingi wa kuyaendesha maisha yako.
Ndiyo kunakuwezesha kula, kuvaa, kuwa na malazi na kuweza kutunza familia.
Ukikosa kipato, mambo mengi sana kwenye maisha yako yanavurugika na unakosa umakini mzuri.
Cha kushangaza sasa, shughuli hii muhimu sana kwenye maisha ya kila mtu, watu wamekuwa hawaipi uzito wa kutosha.
Watu wengi wamekuwa wanaichukulia kawaida tu na matokeo yake ni kuingiza kipato cha kawaida na maisha yao kuwa magumu.
Halafu kuna wale ambao wanaipuuza kabisa shughuli hiyo, kwa kujidanganya kwamba fedha siyo kila kitu, kwamba kuna mambo mengine muhimu kwenye maisha kuliko fedha.
Watu hawa hujifariji na mengine wanayojihusisha nayo ambayo hayaingizi fedha. Na maisha yao huwa magumu sana.
Ni dhambi kubwa sana na kutokujitendea haki pale unapojidanganya kwamba fedha siyo muhimu kwako wakati bado hujawa na uhakika wa kipato.
Kama hujafika hatua ya kifedha ambapo maisha yako yote yaliyobakia unaweza kuyaendesha vizuri hata kama hafanyi kazi ya kukuingizia kipato moja kwa moja, basi kipaumbele cha kwanza kwako kinapaswa kuwa kuingiza fedha.
Usijidanganye kwa kitu kingine nje ya hapo, usiwe na unafiki wowote.
Weka kipaumbele chako kwa usahihi na kifanyie kazi.
Fedha inagusa kila eneo la maisha yako, hivyo kama haijawa na utulivu, maisha yako hayawezi kuwa na utulivu.
Na kujidanganya kwamba unajenga utulivu wa maisha nje ya fedha ni kuzidi kujipoteza.
Ukweli ni kwamba, usipoingiza kipato cha uhakika na usipojijengea utajiri na uhuru wa kifedha, unajiweka kwenye hatari ya kupoteza vitu vyote muhimu kwenye maisha yako.
Lengo lako kuu kwenye maisha ni kuwa tajiri (kuweza kununua chochote unachotaka) na kufikia uhuru wa kifedha (kuweza kuishi vizuri hata kama hafanyi kazi moja kwa moja).
Lengo lolote jingine kabla ya kufikia haya makuu ni kujidanganya na kujipoteza.
Na shughuli muhimu zaidi kwenye maisha ni ile inayokufikisha kwenye lengo hilo kuu, ambayo ni kuingiza kipato.
Shughuli hiyo kuu kwenye biashara inahusisha mauzo, ambayo ndiyo njia pekee ya kuingiza fedha kwenye biashara.
Hiyo inaturudisha kwenye msingi huo mkuu kwamba kuuza ndiyo shughuli kuu kwenye maisha.
Ni kupitia kuuza ndiyo utaweza kujenga maisha yoyote unayoyataka.
Kama kuna kitu hakipo sawa kwenye maisha yako, unaweza kukiweka sawa kwa kuuza zaidi.
Hili linatufikisha wapi basi, MAUZO NDIYO SHUGHULI KUU KWENYE MAISHA YAKO.
Kwa kuwa njia kuu kwetu kuingiza kipato ni kupitia kuuza vitu mbalimbali, mauzo yanakuwa ndiyo shughuli kuu kwenye maisha yetu.
Na hivyo tunawajibika kuwa wauzaji wazuri sana.
Ni muhimu uwe na njia sahihi ya kujipima kwenye shughuli hii kuu na kupiga hatua kubwa zaidi kadiri unavyokwenda.
Lazima uweze kupima pale ulipo sasa na kule unakopaswa kufika ili kupata utajiri na uhuru wa kifedha.
Hakuna kitu kama masikini mwenye furaha,
Au masikini mwaminifu.
Furaha na uaminifu haviwezi kukaa pamoja na umasikini.
Ni kujidanganya tu na kujipa moyo.
Na zaidi kuficha huzuni na maovu nyuma ya hilo.
Ni wajibu wako namba moja kuwa tajiri na kufikia uhuru wa kifedha.
Na shughuli muhimu zaidi kwako ni ile ya kuingiza fedha, ambayo ni mauzo.
Ninachotaka kusema mabibi na mabwana ni hiki, uza zaidi.
Utauza zaidi kwa kuwafikia watu wengi zaidi na kuwashawishi zaidi.
Utauza zaidi na zaidi kwa kuwahudumia watu wako zaidi na kuwafuatilia zaidi.
Una changamoto yoyote kwenye maisha yako, rudi kwenye mauzo ili kuweza kuitatua.
Usichanganye vipaumbele.
Kama hujafikia utajiri na uhuru wa kifedha, hilo ndiyo linapaswa kuwa kipaumbele namba moja kwako, mengine yote yanaweza na yanapaswa kusubiri.
Weka vipaumbele vyako sawa na usiwasikilize wanaokushauri kinyume na hilo, wana ajenda zisizo sahihi na maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Sitowasikiliza wale wote wanaonishauri nifanye yale Yaliyo tofauti na kujenga utajiri na kufikia uhuru wa kifedha kwani waanajenda zao ovu dhidi yangu
LikeLike
Tuwaepuke kama ukoma.
LikeLike
Ni kweli umasikini haujawahi kuleta furaha furaha inaletwa na kukakilisha yale ya msingi kabisa na ni muhimu kupambana na mauzo ili tuweze kufikia lengo la ubilionea kwa kufanya yafuatayo
1.kuwafikia walengwa wengi
2.kuwapa thamani kubwa
3.kuwashawishi wengi na
4.kuwahudumia kwa ubora kabisa na
Mwisho kuwafuatilia na kurudia mchakato kwa msimamo
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Nitauza zaidi ili kufikia uhuru wa kifedha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuuza/kushawishi ndiyo nguzo kuu ya Mimi kuufikia utajiri ili kuufikia Uhuru wa kipato (fedha).
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Mauzo ndiyo shughuli kuu kwenye maisha, kupitia MAUZO tunaweza kuwa kile tunachotaka.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha ni kuuza tu mengine yote mbwembwe
LikeLike
Tuuze.
LikeLike
Kuuza ndio kupaombele namba moja kwenye maisha yangu, mengine yote ni kujiangusha kwenye kuufikia ubilionea.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mauzo ndiyo mpango mkuu kuufanyia kazi na kipaumbele kikuu kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha.Kila mtu yupo kwenye mauzo.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kweli, kama unadhani fedha hainunua furaha ni kwa sababu hujui duka liko wapi – Dan Pena.
LikeLike
Na Mwana FA akaongezea kama pesa hainunui furaha, umasikini unanunua nini?
LikeLike
Kabla ya kufikia utajiri na uhuru Wa kifedha, mengine yote yanaweza kusubiri.
Kipaumbele kuuza zaidi…
Asante Kocha.
LikeLike
Tusijichanganye na mengine.
LikeLike
Mauzo ndio kipaumbele Cha kwanza kwenye maisha kama una changamoto yoyote inakusumbua fanya mauzo
Asante
LikeLike
Uza. U.Z.A.
LikeLike
Kilicho muhimu Ni kuuza zaidi, mengine yote yanategemea mauzo.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Tuuze, ila siyo sura.
LikeLike
Ni kweli inahitajika kupambana na umasikini na kutotafuta furaha isiyo ya kinafiki kwenye pesa.
LikeLike
Hakika, tusijidanganye.
LikeLike
kuuza ndio nyenzo muhimu ili kufikia utajiri na uhuru wa kifedha
shukrani kocha
LikeLike
Tukae humo
LikeLike
Asante kocha,kuuza ndo njia ya kupata utajiri na kuwa na uhuru wa kifedha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Fedha ndo kila kitu.
LikeLike
Tuzisake kwa uhakika.
LikeLike
Ni kuuza tu. kukusanya fedha Ili Kujenga hakuna la kujivunia kwenye umaskini zaid ya kukuzalilisha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Utauza zaidi kwa kuwafikia watu wengi zaidi na kuwashawishi zaidi.
Utauza zaidi na zaidi kwa kuwahudumia watu wako zaidi na kuwafuatilia zaidi.
Una changamoto yoyote kwenye maisha yako, rudi kwenye mauzo ili kuweza kuitatua.
Ahsante sana Kocha.
Nitauza Zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Fedha ndiyo kitu muhimu zaidi kwangu, ili kupata fedha zaidi natakiwa kuuza zaidi, ili kuuza zaidi natakiwa kuwafikia watu zaidi, ili kuwafikia watu zaidi natakiwa kuwa na timu imara na adilifu. Tumu na mauzo zaidi ndiyo shughuli kuu hakuna kikingine.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Hakika hakika kakika kocha. Nguvu moja
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kweli kabisa, kuyngiza kipato ndiyo shughuli muhimu kuliko zote kwa kila mmoja. Shughuli zingine zaidi ya hii ni mbwembwe tu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kazi kubwa na muhimu kwangu kwa sasa ni kufikiria kuingiza kipata kupitia kuuza,nipo kazi karibia miaka 19,na kwenye biashara mwaka mmoja na nusu,najua nini ni nini
LikeLike
Kwa kuwa njia kuu kwetu kuingiza kipato ni kupitia kuuza vitu mbalimbali, mauzo yanakuwa ndiyo shughuli kuu kwenye maisha yetu.
LikeLike
Ni kweli kabisa kuwa shughuli iliyo muhimu zaidi kuliko zote ni ya kuingiza kipato.
Na njia ya uhakika ya kuingiza kipato ni kuwa na biashara na kuuza ndiyo shughuli kuu kwenye maisha.
Kwa hiyo basi Mauzo ndiyo shughuli kuu kwenye maisha yako.
Asante
LikeLike