3009; Umasikini na uaminifu.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye makala ya ukurasa wa 3008 uliopita niliandika;
‘Hakuna kitu kama masikini mwenye furaha,
Au masikini mwaminifu.
Furaha na uaminifu haviwezi kukaa pamoja na umasikini.’
Kila mtu alikubaliana na upande kwamba hakuna masikini mwenye furaha.
Na hilo liko wazi kwamba huwezi kuwa na furaha kama huna uhakika wa wapi utapata fedha ya kula kesho, au unakosa mahitaji mengine muhimu.
Lakini baadhi ya watu hawakukubaliana na upande kwamba hakuna masikini mwaminifu. Waliona kuna masikini ambao wapo vizuri tu kwenye eneo la uaminifu.
Na mimi nalikataa hilo kata kata.
Hakuna masikini ambaye ni mwaminifu.
Kwa kuanza, kitendo tu cha kuwa masikini kinamweka mtu kwenye hali ya kukosa uaminifu.
Masikini ni rahisi kushawishika kudanganya au kudokoa ili kupata kitu fulani anachoshindwa kupata kwa sababu ya umasikini wake.
Kwa mfano kama una njaa na huna fedha ya kupata chakula, ni rahisi kwako kuhalalisha kudanganya ili upate chakula.
Ni wachache sana ambao wapo tayari kusimamia ukweli kwenye hali za aina hiyo.
Jambo la pili na kubwa kabisa ni umasikini ni matokeo ya kufanya au kutokufanya vitu fulani.
Ndani ya kila mmoja wetu tayari upo uwezo mkubwa wa kupata chochote ambacho anataka.
Kama mtu ni masikini, kuna namna ameshindwa kutumia uwezo mkubwa ambao tayari anao.
Je unadhani ni uaminifu kushindwa kutumia kitu ambacho tayari kipo ndani yako?
Jibu ni hapana, kama unashindwa kutumia vizuri kitu chenye manufaa ambacho unacho, unakosa uaminifu kwako mwenyewe na hata kwa wengine pia.
Tatu na mwisho tunakubaliana umasikini ni dhambi kubwa sana kwenye maisha, ambayo tunapaswa kupambana nayo ili kuitokomeza kabisa kwenye maisha yetu.
Je unadhani dhambi inaweza kuwa na uaminifu?
Jibu ni hapana, dhambi na uaminifu haviwezi kwenda pamoja.
Unakuwa na dhambi pale unapokosa uaminifu.
Hivyo kitendo tu cha kuwa masikini, tayari unakuwa umekosa uaminifu.
Umasikini ni mbaya,
Umasikini ni dhambi,
Umasikini ni kukubali kuishi maisha ambayo siyo ya hadhi yako.
Hatupaswi kuuremba na kuubembeleza umasikini kwa namna yoyote ile.
Ni adui tunayepaswa kumpa kila aina ya jina baya na kumshambulia kisawasawa.
Maana yeye mwenyewe anapopata nafasi anatushambulia kikatili.
Kuutetea umasikini kwa namna yoyote ile ni kuukaribisha na kuukumbatia kwenye maisha yako, kitu ambacho kinafanya uendelee kuwa masikini.
Umasikini ni adui ambaye hastahili huruma yoyote kutoka kwako.
Unapaswa kumshambulia kwa silaha yoyote unayoweza kuwa nayo.
Hata kama unaanzia kwenye umasikini, usikubali kwamba wewe ni masikini.
Kamwe usijiite masikini, bali jiite tajiri uliye kwenye matengenezo.
Uchukie na kuukataa umasikini na mambo mengine yote yanayohusiana nao.
Umasikini ni adui ambaye hahitaji huruma wala utetezi wako, bali mpe adhabu anayostahili.
Umasikini unatesa na kudhalilisha, hupaswi kuuonea huruma kwa namna yoyote ile.
Ushambulie na kuuangusha ili kuweza kujenga maisha bora kwako.
Nimalizie kwa kusema kwamba kama inabidi ushawishiwe kwamba umasikini ni mbaya na haustahili utetezi wowote, basi itakuwa vigumu sana kwako kutoka kwenye umasikini huo.
Hatua ya kwanza kwenye vita yoyote ni kumpa adui jina baya, ili uweze kumshambulia bila kujali.
Kwenye mapambano yako na umasikini, upe majina yote mabaya na ushambulie bila ya huruma.
Achana na jamii inayoonekana kutetea umasikini na masikini kwa nguvu kubwa.
Huo ni mkakati wa kuwafanya masikini wajisikie vizuri na kuendelea kubaki kwenye umasikini wao, kitu kinachowafanya watawalike kirahisi kwenye jamii.
Wewe ukatae na uchukie umasikini, usiutetee kwa namna yoyote ile.
Adui mtesi hahitaji huruma yako, ni wa kuangushwa na kuvunjwavunjwa.
Umasikini hauendani na furaha,
Umasikini hauendani na uaminifu,
Tuupinge, kuukataa na kuushambulia umasikini kwa kila namna bila ya kuuonea huruma.
Maana wenyewe ukipata nafasi, unatutesa sana bila ya huruma yoyote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
umaskini unadhalilisha,hakuna namna ya kuutetea umaskini kuonekana mzuri au kuuonea huruma.
Ni vigumu maskini kuwa mwaminifu.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Umaskini kweli ni dhambi na ili tuachane na dhambi hiyo ni kupambana nao kama tunavyopamba na shetani
LikeLike
Kabisa yani.
LikeLike
Asante Kocha kila siku nitaupinga umasikini
LikeLike
Tusiulazie damu.
LikeLike
Umasiini ni dhambi. Mimi ni tajiri,
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Umasikini haujawahi kuwa mzuri wala hautakaa kuwa mzuri, kinachoongelewa ni hadithi tuu za kuwafariji walio amua kukaa katika umasikini.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Umaskini unadhalilisha,umaskini unakosesha raha,nimechagua kupambana na adui umaskini bila kumuonea huruma mana yeye hana huruma hata kidogo anaposhambulia anashambulia kwelikweli.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ninaukataa umaskini na wadau wake na wapambe wake wote.
LikeLike
Umasikini ni mbaya na una dhalilisha sana
LikeLike
Sinaga urafiki na hili jitu umasikini.
LikeLike
Umaskini ni dhambi kubwa, nauchukia, unanyima furaha na unakosesha uaminifu.
LikeLike
Umaskini ni uovu.
LikeLike
Tusihuonee huruma umaskini wenyewe hauna huruma kwetu
Asante
LikeLike
Ahsante sana kocha, nauchukia sana umasikini na siku zote nitaushambulia kwa nguvu zangu zote
LikeLike
Umasikini ni laana.
LikeLike
Umasikini hauendani na furaha,
Umasikini hauendani na uaminifu,
Tuupinge, kuukataa na kuushambulia umasikini kwa kila namna bila ya kuuonea huruma.
Maana wenyewe ukipata nafasi, unatutesa sana bila ya huruma yoyote.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Nitapambana na kuushambulia umaskini kwa kila silaha niliyonayo!
LikeLike
Asante Kocha nitajitahidi kuupinga Umaskini kwa nguvu zote
LikeLike
Ndiyo, umaskini ni adui ambaye tunapaswa kumshambulia vibaya. Hata hivyo si kweli kwamba maskini wote si waaminifu. Wapo maskini waamonifu na wasio waaminigi. Hali kadhalika wapo matajiri waaminkfu na wasio waaminifu. Japo ninkweli kwamba ni rahisi kwa maskini kushawishika kufanya mambo yasiyo ya uaminifu.
Ukowa na Yesu unaweza kuwa mwaminifu katika hali yoyote ile, ya utajiri au umaskini.
LikeLike
ahsante kocha , hatua ya kwanza ya kumshambulia adui ni kumpa majina mabaya
LikeLike