3024; Kazi itakayokulipa vizuri wakati wote.
Rafiki yangu mpendwa,
Ukitaka upotee na kukosa kabisa mafanikio kwenye hizi zama tunazoishi, sikiliza na fanyia kazi kila aina ya ushauri unaopewa na kila mtu.
Kumekuwa na ushauri mwingi kinzani ambao umekuwa unatolewa na watu wengi kwenye mambo mbalimbali.
Na sehemu kubwa ya ushauri huo huwa ni nini kinalipa au hakilipi.
Watu wanaotoa ushauri huo huwa wanajiamini sana wakati hawana uzoefu au matokeo yoyote kwenye hayo wanayoshauri.
Kwa bahati mbaya sana washauri hao huwa ni mawakala wazuri wa kueneza hali mbaya na kujenga hofu kubwa ndani ya watu.
Huwezi kuwasikiliza watu hao wanavyoshauri kwa kujiamini na ukabaki salama.
Lazima wataacha wasiwasi mkubwa ndani yako ambao utaathiri sana kile unachofanya.
Kila wakati watu hao huwa wanakuwa na habari njema na habari mbaya.
Lakini huwa wanaweka mkazo zaidi kwenye habari hasi ili kuwafanya watu wajawe na hofu na kuchukua hatua fulani wanazozotaka ili wanufaike.
Tutaangalia mifano miwili kuelewa vizuri hii dhana.
Mfano wa kwanza ni kwenye teknolojia.
Kuna watu huwa wanatumia mabadiliko yanayoendelea kwenye teknolojia kutafuta njia za kuwajaza watu hofu ili wajinufaishe nao.
Kila kunapokuwa na teknolojia mpya ambayo wengi hawajaielewa, watu hao huwa wa kwanza kuonyesha ni jinsi gani wale ambao hawajaanza kutumia teknolojia hiyo mpya watakavyopoteza.
Watu wale wale ambao mwaka juzi walikuwa wanakuambia Bitcoin (fedha za kidijitali) ndiyo kila kitu na kama huzimiliki utakufa masikini.
Ndiyo hao hao ambao mwaka jana walikuwa wanakuamboa NFT (umiliki wa picha kidijitali) ndiyo kila kitu na kama huna umiliki huo wewe ni masikini mkubwa.
Na ndiyo hao hao ambao mwaka huu wanakuambia chatGPT (lugha ya kuwasiliana na kompyuta) ndiyo kila kitu na itachukua kazi zote ambazo watu wanafanya.
Ukiwafuatilia watu hao mara zote utajawa hofu na kuona tayari umeshapoteza.
Tukiangalia mfano wa pili ambao ni kwenye mambo ya kawaida.
Watu wale wale ambao mwaka juzi walikuambia ufugaji wa kware ndiyo kila kitu na kama huwafugi utakufa masikini.
Ndiyo hao hao mwaka jana wakakuambia ufugaji wa sungura ndiyo habari ya mjini na kama huna sungura hujui unachofanya.
Na ndiyo watu hao hao mwaka huu wanakuambia ufugaji wa bata ndiyo habari yenyewe, mwingine kote unajichelewesha.
Ukiangalia mambo ni yale yale, kupeana hofu kwa mambo yanayobadilika badilika.
Leo nataka nikutoe hofu zote ambazo umekuwa unajazwa kuhusu kuachwa nyuma kama hukimbizani na kila kitu kinachobadilika.
Nataka nikuambie kazi itakayokulipa vizuri wakati wote na ambayo haitakutaka ukimbizane na kila aina ya manadiliko yanayoendelea.
Kazi hiyo ni mauzo.
Ukijifunza na ukawa muuzaji mzuri na aliyebobea, utakuwa na fursa zitakazokulipa vizuri kwa kipindi chote cha uhai wako.
Ukiwa muuzaji mzuri, haijalishi ni teknolojia gani imekuja, wewe utaendelea kuingiza kipato kikubwa zaidi.
Wauzaji bora hawana hofu ya kitu chochote kuathiri kipato chao, kwa sababu wanajua mauzo yatathaminiwa wakati wote.
Haijalishi ni mabadiliko gani yanayoendelea kiteknolojia, mauzo yataendelea kuwa fursa kubwa kwa sababu bado watu wanahitaji kushawishiwa kuchukua hatua sahihi.
Haijalishi ni ufugaji gani unaolipa zaidi, mauzo yataendelea kulipa kwa sababu hivyo vinavyofugwa vitahitaji watu washawishiwe ndiyo waweze kuvitumia.
Jifunze na uwe muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea na hutakuwa na hofu juu ya mabadiliko mbalimbali yanayoendelea.
Sisemi hutahitaji kubadilika, mabadiliko ni lazima.
Ninachosema ni hutahitaji kuhofia chochote kinaweza kuathiri sana kipato chako, kwa sababu ujuzi unaokuwa nao ni wenye nguvu ya kukulipa kwenye nyakati zote.
Kuwa muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea na hakuna kitakachoweza kuathiri kipato chako kwa kiwango kikubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitakuwa muuzaji bora siku zote
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nitakuwa muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea ili kutotetereka na mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kweli mafanikio yako kwenye kuwa muuzaji Bora
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kwa kweli kuwa muuzaji bora kabisa utafanikisha mengi na makubwa, kwenye suala la mafanikio mauzo ni kipaumbele cha kwanza.
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
Ni kweli Kocha dunia haina matatizo kama tutajifunza kuwa wauzaji bora. Mimi Isaack ni muuzaji bors kuwahi kutokea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wauzaji bora hawana hofu ya kitu chochote kuathiri kipato chao, kwa sababu wanajua mauzo yatathaminiwa wakati wote.
Ahsante sana Kocha.
Nimekuelewa vizuri sana.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Nimechagua kujifunza kila siku ili niwe muuzaji bora kuwahi kutokea na kuepuka kabisa kukimbizana na fursa zinazoibuka kila mara
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ninataka kujifunza kila siku ili niwe muuzaji bora na mbobevu kutokea duniani ili niache a kabisa kukimbizana na fursa mlipuko za kila mara.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Sihitaji kuwa na hofu Kwa yale yanayoendelea kwenye maisha, ambayo yanaoneka kama fursa mpya ya kupata kipato. Wengi wanaendesha biashara ya kuwahamasisha watu wameijua vyema mbinu ya kutumia hofu kupata umakini WA wengine. Hivyo Usikubali mbinu hii ikayumbisha maisha Yako Kwa kudandia Kila fursa mpya ukizani utakuwa mpya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ahsante sanaa kocha Dr makirita amani kwa makala na uzi mkali Sanaa wa Leo. Hapa nimejifunza kuwa na msimamo katika kujifunza Kwa kina juu ya mauzo na kuwa muuzaji mbobezi
Nitahakikisha najifunza Kila siku bila kuacha kuhusu mauzo na kuwa muuzaji Bora Sanaa kuwahi kutokea.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Ujuzi Wa mauzo, njia pekee ya kuniingizia kipato Cha uhakika.
Nabaki kwenye mchakato mambo mazuri yapo mbele
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha kwa somo, ni kweli kabisa kuwa mauzo ni kila kitu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Jifunze kuuza na hutaangaika na chochote kwenye maisha
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Wauzaji bora hawana hofu ya kitu chochote kuathiri kipato chao, kwa sababu wanajua mauzo yatathaminiwa wakati wote.
Asante sana Kocha, nitakuwa Muuzaji bora wa Chumvi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Najifunza mauzo mara kwa mara na nakuwa Muuzaj bora kuwahi kutokea
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kweli kabisa. Mauzo ndiyo mpango mzima
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
hizi story za kitu fulani kinalipa zaidi hizi.Kama haupo makini unapoteza focus sana kwenye kufanya mambo ma kupata matokeo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,ni vyema kujikita kwenye ubora wa mauzo na sio kukimbizana na kila frusa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Muhimu ni kuwa sehemu sahihi,kujifunza jinsi ya kuwa Muuzaji bora wa wakati wote hata kama mabadiliko yanatokea unakuwa ndani ya mchakato
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ntahakikisha nakuwa muuzaji bora kuwahi kutokea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Haijalishi ni mabadiliko gani yanayoendelea kiteknolojia, mauzo yataendelea kuwa fursa kubwa kwa sababu bado watu wanahitaji kushawishiwa kuchukua hatua sahihi
LikeLike
Tuwe bora kwenye mauzo.
LikeLike
Nitakuwa muuzaji mkubwa na mahiri.
LikeLike
Mimi Deogratius Stanslaus Kessy ni muuzaji bora kuwahi kutokea na ninaweza kupata chochote nachotaka kwenye maisha yangu kama nitauza zaidi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ni kweli ukihangaika na mambo mingi hutafanikiwa utaishia tu kuchoka bure
LikeLike
Tuelekeze nguvu zetu sehemu sahihi.
LikeLike
Kweli Mauzo ni jambo la msingi kuzingatia mara zote ili kutohathirika na mabadiliko yanayoweza kutokea
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Jifunze kuwa muuzaji Bora kuwahi kutokea na hutakua
na hutayumbishwa na badiliko lolote , kwa sababu ujuzi
Utakaoupata ni. wenye nguvu ya kukulipa wakati wote
Asante Sana kocha kwa makala hii.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni kweli kabisa.
Kazi itakayonilipa vizuri na kwa muda mrefu ni Mauzo.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Haipingiki kabisa. Nikiweza kuuza Basi nimetoboa. Nataka kufanya mauzo Kama mchezo wangu pendwa wa maisha sio Kama kazi.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mauzo ndiyo itakayokulipa zaidi kuliko mambo yote
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike