3026; Anza upya kila siku.
Rafiki yangu mpendwa,
Mwanzo wa kitu chochote kile huwa ni wa shauku na hamasa kubwa.
Mtu unapokuwa unaanza kufanya kitu, unakuwa na msukumo wa kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo mazuri.
Msukumo na juhudi hizo za awali huwa zinapelekea mtu kupata matokeo mazuri na kumpeleka ngazi za juu.
Mtu anakuwa amepiga hatua fulani kwenye kile anachokuwa anafanya.
Na hapo sasa ndipo hatari kubwa inapomnyemelea mtu.
Mtu anabadilika, anaacha kushambulia kama alivyokuwa anafanya awali, badala yake anaanza kulinda matokeo ambayo ameshayapata.
Ule msukumo na juhudi za awali zinaondoka na nafasi yake kuchukuliwa na mazoea.
Mtu anaanza kufanya kwa mazoea huku akilinda matokeo ambayo ameshayapata yasipotee.
Hali hiyo ya mazoea na kulinda matokeo ya nyuma ndiyo huwa inawaangusha wengi baada ya kupata mafanikio kidogo.
Watu wanakuwa wanapanda vizuri mwanzoni, lakini baadaye wanapata anguko kubwa.
Kuondokana na hali hiyo ya kupanda na kushuka kimafanikio, unapaswa kuwa unaanza upya kila siku.
Kila siku jichukulie kama ndiyo unaanza kufanya chochote unachofanya.
Sahau hatua zozote ambazo umeshapiga na epuka kutaka kulinda matokeo ambayo umeshayapata.
Wewe jione kama ndiyo unaanza upya, hilo litakusukuma uweke juhudi kubwa na za tofauti kitu ambacho kitakupa matokeo makubwa.
Hakuna kitu kinachoharibu mafanikio kama mazoea na kulinda matokeo ya nyuma.
Hiyo inakupa hali ya kuridhika na kuona kama umeshamaliza kila kitu.
Ni katika hali hiyo ya kuridhika ndiyo changamoto na matatizo mbalimbali hujitokeza na kumwangusha mtu vibaya.
Unapokuwa na mtazamo wa kuanza upya kila siku, unakuwa na msukumo wa kufanya tofauti, kitu ambacho kinaondoa mazoea na kukupa matokeo ya tofauti.
Kila siku jichukulie ndiyo unaianza biashara yako.
Pamoja na wateja ambao tayari unao sasa, chukulia wote wamekuacha na huna mteja tena.
Weka juhudi za kutosha kila siku kuzalisha mafanikio mapya.
Mafanikio yoyote ya nyuma yasahau kabisa, kwani hayo yana hatari ya kukuangusha.
Hakuna kitu kinalevya na hatari kama mafanikio.
Mafanikio yana tabia ya kuleta kiburi na mazoea kwa mtu, vitu ambavyo vinakaribisha anguko kubwa.
Chochote unachofanya kwa mazoea na kulinda usipoteze, kinaishia kuwa na changamoto ambazo zitapelekea kupoteza zaidi.
Kila siku jiweke kwenye hali ya hatari ya kupoteza kila ulichonacho na hiyo itakusukuma ufanye kwa ukubwa na utofauti.
Hivi umewahi kugundua kwamba wakati ambao upo bize sana ndiyo pia wakati ambao unafanya makosa machache sana yasiyo na tija?
Ndiyo huwa iko hivyo, unapokuwa umetingwa hasa, huwa huhangaiki na mambo yasiyokuwa na tija na hivyo kupunguza makosa yasiyo na tija pia.
Sahau mafanikio yoyote ambayo umeshayapata huko nyuma na anza upya kila siku.
Kuwa na njaa ya mafanikio mara zote na jisukume sana katika kuchukua hatua mpya kwa yale unayokabiliana nayo.
Usifanye kitu leo kwa sababu ulikifanya jana pia, hata kama utakifanya kama jana, lakini sababu ya kukifanya leo inatakiwa kuwa tofauti na ya jana.
Usilinde sana chochote ambacho umeshakipata, itakuzuia kuchukua hatua mpya na hatari na hivyo kukunyima matokeo mapya na makubwa.
Mara zote shambulia kama ndiyo unaanza, ukiwa na hasira ya kufanya makubwa zaidi.
Jiweke kwenye hatari ya kupoteza makubwa kama utafanya kwa mazoea. Hilo litakusukuma uachane na mazoea na ufanye kwa utofauti ili kutokupoteza kwenye hatari uliyojiweka.
Kukosa hamasa na msukumo huwa ni zao la mazoea, ambayo hujitokeza pale mtu anapolinda matokeo ambayo ameshayapata badala ya kushambulia ili kupata matokeo mapya na bora zaidi.
Kama unataka kuwa na hamasa isiyoisha, kila wakati anza upya.
Sahau matokeo ambayo umeshayapata na jichukulie unaanza upya kabisa.
Ni hali hiyo ya kuanza upya ndiyo inayokuweka kwenye hali ya kujisukuma sana ili kupata matokeo bora zaidi.
Mafanikio yoyote ambayo umeshayafikia, jua unaweza kwenda zaidi ya hapo.
Lakini kilochokufikisha hapo ulipofika sasa, siyo kitakachokupeleka mbele zaidi.
Achana na mazoea yote ya nyuma na kulinda mafanikio hayo ambayo umeshayapata.
Badala yake anza upya kila wakati ili kuwa na njia bora za kupata matokeo ya tofauti.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kila siku ni ya kutafuta ushindi. Umefunga goli Moja hupaswi kurudi nyuma na kulinda goli Bali unapaswa kupeleka mpira kati na kutafuta magoli mengine yatakayoendelea kuimarisha ushindi wetu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Anza upya kila wakati, kila siku nitakuwa nafanya kama ndio natafuta na kuhudumia mteja wa kwanza.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kila siku ni siku ya kuanza upya ili kuwa na hamasa ya kufanya makubwa.Nisikumbatie mafanikio yoyote niliyonayo sasa kwani ni kikwazo kwa mafanikio yangu zaidi mbeleni.Asante.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitaanza upya be kila siku
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitabweteka na mafanikio kidogo niliyo nayo au yatakayokuja bali najifunza kuanza upya kila mara ili niweze kubuni mbinu na njia mpya za kuendesha biashara na maisha yangu.
Asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Usilinde mafanikio uliyonayo,
Bali shambulia kila siku na ondoa mazoea
LikeLike
Mashambulizi yanapaswa kuwa endelevu.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa mtazamo huu sahii.
Leo ni siku yangu mpya na kipekee nakwenda kufanya makubwa zaidi nakataa mazoea nafanya kwa utofauti kupata matokeo bora
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Usifanye kitu leo kwa sababu ulikifanya jana pia, hata kama utakifanya kama jana, lakini sababu ya kukifanya leo inatakiwa kuwa tofauti na ya jana.
Nimekuelewa vizuri sana Kocha.
Ahsante Kocha.
LikeLike
Fanyia kazi.
LikeLike
Kila siku nitatafuta ushindi mpya kwakuanza upya kwenye biashara yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Anza upya kila Wakati ili kuwa na njia bora kukusogeza
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Anza upya kila siku,asante sana kocha kwa makala hii,sitaridhika na yale niliyonayo , nitaendelea kujifunza na kupambana kila siku.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mazoea yoyote yale ni kikwazo kikubwa sana kwenye biashara na maisha yetu kwa ujumla.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nitajitahidi kuanza upya kila siku ili kuwa bora zaidi. Asante sana kocha
LikeLike
Kweli
LikeLike
Nitahakikisha naanza upya na kuacha a na mazoea yanayonipa furaha ya muda badala yake nitaweka malengo makubwa yanayonisukuma nipambane zaidi ili niweze kuyafikia
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kila siku itskuwa mpya kwangu na staancha kufanya kamwe
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Usichukulie mafanikio yako ukiyonayo leo ndio mwisho wa safari yako ya mafanikio.
Kila siku jichukulie kuwa mpya na anza kama huna kitu ambacho umekifanya.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mafanikio kidogo ndio sumu ya mafanikio makubwa
Asante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kila siku yangu nihakikishe nasahau matokeo ambayo nimeshayapata na jichukulie %$naanza upya kabisa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kila siku ni mpya kwangu kufanya mambo ya tofauti bila mazoea, naepuka mazoea yanayoleta anguko.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Naacha kulinda goli na kuanza kushambulia.
LikeLike
Shambulia kwa kasi kubwa.
LikeLike
Unapoongeza maarifa mapya Ni sawa na kuanza upya. Ongeza ubunifu acha Mazoea na ongeza kazi kwenye kazi. Naongeza bidii na kuwa mpya kila siku mpaka watu hawataamini.
LikeLike
Kaa humo.
LikeLike
Kial siku mtaanza upya kwa kujifunza upya na kupiga hatua zaidi kwenye maisha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
mafanikio niliyo nayo sasa ni hatari sana kama ntaogopa kupoteza,itanifanya nishindwe .Nitaanza upya kila siku
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ni kweli ukibweteka na matokeo madogo utajisahau kwa kuona umefika mwisho kumbe ni muhimu kuanza mchakato upya wa kusaka ,kugeuza na kutoa huduma bora
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Naanza upya
LikeLike
Vizuri
LikeLike