3027; Watu wa aina yako.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna vitatu muhimu sana nilivyojifunza wakati naanza kwenye hii safari ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Kimoja ni kutoka kwa aliyekuwa maandishi na mnenaji Jim Rhon ambaye alisema; maisha yako ni wastani wa maisha ya watu watano wanaokuzunguka. Akimaanisha unakuwa kama wale unaotumia nao muda wako mwingi.
Cha pili ni kutoka kwa aliyekuwa mwasisi wa tasnia ya uandishi wa maendeleo binafsi, Napoleon Hill ambaye alisema ili ufanikiwe, unahitaji kuzungukwa na watu wanaokusukuma kuyaelekea mafanikio yako. Alieleza kila mmoja anatakiwa kuwa na kikundi cha watu ambao wanamjua kwa undani mafanikio anayoyataka na kumwajibisha ili aweze kuyafikia. Alikiita kikundi hicho Master Mind Group.
Cha tatu ni umuhimu wa kuwa na mtu mmoja kwenye maisha yako ambaye hatapokea uongo unaojidanganya nao mwenyewe. Mtu huyo anakuwajibisha ipasavyo bila ya huruma ili uweze kufikia makubwa kwenye maisha yako. Hili nilijifunza kwa Dan Pena, mmoja wa makocha bora kabisa kwenye eneo la maendeleo binafsi. Hivyo kila mtu anapaswa kuwa na mtu wa kumwongoza, kupitia kumfundisha na kumwajibisha kwenye maeneo muhimu ya maisha yake. Kama ambavyo wachezaji na timu zenye mafanikio zina makocha, ndivyo pia ilivyo kwa watu wanaoyataka mafanikio makubwa.
Rafiki, ni kwa kuchanganya vitu hivyo vitatu ndiyo tulipata wazo la kujenga jamii ya tofauti kabisa, jamii yenye watu wa aina zetu, watu wenye kiu ya mafanikio makubwa. Watu ambao siyo tu wasemaji, bali watendaji, wanaojifunza na kuchukua hatua ili kuyapata mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Jamii hii tukaiita KISIMA CHA MAARIFA, mwanzoni kikiwa mtandaoni pekee, lakini baadaye kikatoka mtandaoni na kuja kwenye maisha halisi kupitia klabu za KISIMA CHA MAARIFA za mikoa.
Kama ilivyo kwa jambo lolote jipya, watu hulipokea kwa shauku kubwa wakitegemea litakuwa jambo rahisi lisilohusisha kazi.
Hivyo mwanzo tukawa na klabu nyingi sana na zenye watu wengi.
Lakini kadiri tulivyokwenda, watu wakaanza kupungua kwenye klabu, hasa pale uwajibishwaji ulipoanza.
Watu walidhani klabu ni sehemu za kubembelezana na kuliwazana.
Lakini zilipoanza kufanya kazi yake halisi ya kuwabana na kuwawajibisha watu, wengi wakaanza kukimbia.
Pamoja na changamoto hiyo kubwa, bado maono ya kujenga hiyo jamii ya tofauti hayajakufa na hayatakufa kamwe, hata kama watu wote watakimbia.
Nitaendelea kuyasimamia maono haya kwa sababu kupitia kujifunza na pia kwa kuangalia baadhi ya jamii za watu waliopiga hatua, kama watu wa asili ya Asia hapa Tanzania, nimejifunza kitu kimoja kikubwa sana; WATU WENYE KIU YA MAFANIKIO MAKUBWA WANAHITAJIANA SANA.
Safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni safari ngumu na yenye kila aina ya vikwazo. Watu wengi kwenye jamii hawapo tayari kukabiliana na ugumu na vikwazo hivyo. Pale wanapokutana navyo, wanakata tamaa na kuiacha safari.
Mtu mwenye kiu ya mafanikio makubwa, akizungukwa na watu wote ambao wamekata tamaa, ni rahisi sana na yeye kukata tamaa.
Bila ya kuzungukwa na watu sahihi, ni vigumu sana kwa mtu kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.
Kwa kuzungukwa na watu wa kawaida na waliokata tamaa, ni rahisi kwa mtu kukata tamaa, kwa sababu tumeona watu wanaokuzunguka wana ushawishi mkubwa kwako.
Kwa kukosa watu wanaoelewa kile wanachofanya, watu wanakosa ushauri sahihi wa hatua gani wachukue.
Na kwa kukosa mtu wa kuwawajibisha bila ya kuwaonea huruma, watu wanajidanganya sana wao wenyewe.
Chukulia lengo kubwa tulilonalo la kufika kwenye ubilionea. Mwambie mtu yeyote kwenye jamii unataka kuwa bilionea na cha kwanza atakucheka. Na hata kama hatakucheka, kwa kutokutaka kukuumiza, ataenda kukusema vibaya kwa wengine kwamba huenda umechanganyikiwa na unajidanganya tu bure.
Haya ni mambo ambayo tayari umeshayasikia sana na huenda umeshajifunza kutokusema lengo lako hilo kubwa mbele ya wengine.
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, ambao tunapenda kuona tunakubalika na watu wengine ndiyo tujisikie vizuri na kujitoa kweli kwenye kile tunachofanya.
Hilo linatufanya tufanane na watu wanaotuzunguka, ili watukubali na tujione tupo ndani ya jamii fulani.
Hakuna kitu kinachotuumiza sisi binadamu kama kujiona tumetengwa au tupo peke yetu.
Ndiyo maana tunaishia kufanana na wanaotuzunguka.
Watu waliofanikiwa sana, baada ya kugundua hili awali kwenye maisha yao, waliondoka kwenye jamii zao na kwenda maeneo mengine ambayo yanawakutanisha na aina ya watu wenye kiu ya mafanikio makubwa.
Duniani kuna nchi ambazo watu wenye kiu kubwa ya mafanikio ni rafiki zaidi kwao, mfano karne ya 18 na 19 watu wengi kutoka bara la Ulaya walihamia Marekani na huko wakapata fursa ya kufanya makubwa.
Na hata ndani ya nchi, kuna maeneo ambayo yanawapa watu fursa za kufanikiwa kuliko maeneo mengine.
Ndiyo maana watu wamekuwa wanaondoka vijijini na kwenda mijini ambapo hawafahamiki na penye watu waliofanya makubwa ili kupata msukumo wa kufanya makubwa pia.
Kwenye nchi zetu ambazo bado zinaendelea, ili kupata mafanikio makubwa siyo tu unahitaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine, bali unahitaji sana kuzungukwa na watu sahihi na kupata mwongozo sahihi.
Unahitaji watu wanaokuelewa kwa ndoto kubwa ulizonazo na kisha kukuongoza na kukuwajibisha kuzifikia ndoto hizo.
Kwa kuwa lengo letu kubwa la kufikia ubilionea linahusisha njia kuu mbili; biashara na uwekezaji, unahitaji sana watu ambao wanayaelewa maeneo hayo kwa kina, kupitia ufanyaji.
Na hapa ndipo tumeboresha zaidi klabu za KISIMA CHA MAARIFA kwa kuzigeuza kuwa bodi ya wakurugenzi kwenye kila biashara ya kila mwanachama.
Kwa sasa klabu ya KISIMA CHA MAARIFA itakuwa na nguvu kubwa ya kumwajibisha kila mwanachama pale anapochukua hatua zisizo sahihi kwenye biashara yako.
Yote hiyo ni kuhakikisha kwamba watu hawajidanganyi kwenye hii safari, wanajitoa kweli na kufanya yale wanayopaswa kufanya ili kupata matokeo wanayopaswa kupatikana.
Wakati tupo kwenye hatua za awali kabisa kwenye hili, kuna makundi ya aina tatu za watu ambao hawatatoboa kwenye hili.
Kundi la kwanza ni wale ambao wameona tangu mwanzo kwamba kitu hiki hawapo tayari nacho, hawapo tayari kuingiliwa kwenye namna wanavyoendesha biashara zao. Hawa tutawapoteza kwa haraka sana.
Kundi la pili ni wale ambao wanadhani hiki ni kitu rahisi, wamepokea kwa wepesi na kuona itakuwa raha tu. Hawa hawajajua maumivu makubwa yanayokuja na hili ambayo yapo mbele yao. Kwa sababu ya mategemeo tofauti, watu hawa watakata tamaa na kukimbia pale mambo yanapoanza kuwa magumu. Pale watakapohitajika kulala njaa wakati wanaiona fedha ipo kwenye biashara.
Na kundi la tatu ni wale wenye ubinafsi, wale wanaotaka kufanya mambo yao wenyewe bila ya kushirikiana na wengine, wale ambao wanaona wataenda kasi zaidi wakiwa peke yako kuliko wakiambatana na wengine. Ambao wanaona kushirikiana na wengine ni usumbufu kwao au watajua mambo yao ambayo hawataki yajulikane. Hawa nafasi wataikosa mara moja kwa sababu kwa sasa tunajenga jamii na siyo mtu mmoja mmoja.
Njia pekee ya kutoboa kwenye ngazi hii mpya tunayoiendea ni kujua ni hatua ngumu mno kwenye maisha yako, hatua itakayokuumiza sana kwenye kukuwajibisha lakini kujitoa kafara kukabiliana na kila kinachokuja ili kuweza kufikia malengo makubwa uliyonayo.
Ni kuwa tayari kuambatana na wengine hata kama hilo linachelewesha safari yako.
Kwa sababu ipo kauli inayosema, kama unataka kwenda kasi nenda peke yako ila kama unataka kwenda mbali, ambatana na wengine.
Sasa kwa kuambatana na watu sahihi, kutapunguza kasi yako, lakini kutakupa nguvu kubwa ya kufika mbali zaidi.
Wale wanaoruhusu aina yoyote ya wasiwasi kuwatawala juu ya hatua hizi mpya hakuna namna watatoboa.
Kitu kimoja ambacho hatutakifanya ni kulegeza viwango tulivyojiwekea ili kwenda na wengi iwezekanavyo.
Viwango vitabaki juu na vitaendelea kwenda juu ili kujenga jumuia ya tofauti sana.
Tupo hapa kwa ajili ya kujenga jamii ya tofauti kabisa, jamii ambayo haitaishia kwetu tu, bali itakwenda vizazi na vizazi.
Nimetoa kafara ya kila kitu kwenye maisha yangu ili kujenga jamii hii.
Na sitakubali kuyaharibu maisha yangu kwa sababu ya watu ambao hawajajitoa kweli kwenye hili.
Tutakwenda kwa viwango hivi na kuendelea kuvikuza zaidi bila ya kujali ni watu wangapi tunawapoteza.
Najua fika kuna watu wapo tayari kulipa tu ada ila waendelee na mambo yao wenyewe, na ningependa nizipate sana hizo fedha kwa sababu nina uhitaji nazo, lakini sitaliruhusu hilo.
Ni upo ndani ya hii jamii kwa miguu miwili ndani au unakaa nje kabisa.
Kuwa vuguvugu, mguu mmoja ndani na mguu mmoja nje haina nafasi hata kidogo.
Nimalize kwa kuwakaribisha wale ambao wamechagua kujitesa hasa kwa ajili ya kujenga jamii hii na wamejitoa kwa kila namna.
Na pia niwaage wale ambao wanaona hawawezi kujitesa kwa ajili ya hili, wanaona mafanikio ambayo wameshayapata yanawatosha au wakienda kwa namna yao watafika wanakotaka kufika.
Ukweli ni hakuna njia moja sahihi kwenye jambo lolote lile, njia zipo nyingi, hii yetu ni moja tu kati ya hizo nyingi.
Haiwezi kumfaa kila mtu, hivyo usijisikie vibaya kama unaona haikufai.
Achana nayo mara moja ili uweze kuwahi kwenye njia iliyo sahihi kwako.
Niweke wazi kwamba sitegemei kila aliye kwenye njia hii awe mkamilifu kwa kila jambo.
Ukamilifu siyo kitu ninachokiangalia, kwa sababu najua ni kitu ambacho hakipo.
Ninachoangalia zaidi ni nia njema na ya kweli kutoka ndani ya mtu kukaa kwenye hii njia.
Na inapodhihirika kwamba kukaa kwenye hii njia ni kitu ambacho ni mzigo kwako au unafanya tu kuwafurahisha wengine, tutakusaidia kuamua haraka, kwa kukuondoa kwenye hii jamii.
Ndani ya jamii ya KISIMA CHA MAARIFA na BILIONEA MAFUNZONI, hakuna mwenye kinga ya kudumu kwamba hawezi kuondoka.
Kinga pekee ya kudumu ni kukaa kwenye mchakato.
Hukai kwenye mchakato, unakwenda na maji, bila ya kujali umekuwepo kwa muda gani au umejitoa kwa kiasi gani.
Hii ni nidhamu ya hali ya juu sana ambayo tunahitaji kuijenga na kutoruhusu kitu chochote kile kiingilie au kuilegeza ili kupata watu wengi zaidi.
Nimekuwa nikisema KISIMA CHA MAARIFA ni jeshi, kitu cha kwanza muhimu kwenye jeshi lolote lile ni NIDHAMU YA HALI YA HUU SANA KWENYE KUAMUA NA KUCHUKUA HATUA.
Tukae humo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Muhimu kwenye jeshi ni nidhamu.
LikeLike
Hakuna kitu kirahisi kwenye maisha,ili niweze kufikia ndoto na malengo makunwa niliyo nayo kwenye maisha inanipasa kuwa na nidhamu kubwa isiyoyumbishwa na chochote na kukaa kwenye mchakato sahihi.
Asante kocha.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato bila kuyumbishwa na chochote.
LikeLike
Bila NIDHAMU hakuna kikubwa kinachoweza kufanyika.
LikeLike
Ahsante sana kocha🔥👏✅
LikeLike
✌️
LikeLike
Nimekusikiliza na kusoma ukurasa huu kwa umakini sana. Nashukuru nimeelewa muhimu ni mchakato
LikeLike
Karibu tukae kwenye mchakato kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
Nidhamu,uadilifu na kujituma ndiyo msingi mkuuu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kunahitajika kwanza kujitoa kujikana mwenyewe kuwa na nidhamu kali ya kuamua na kufanya na pia kuweka ubinafsi pembeni na kutembea na kundi huku tukielekezana kwa pamoja na kwa ubora zaidi mungu akulinde kocha tuendelee kupata madini ya kutufikisha kwenye ubilionea na ni lazima tutoboe
LikeLike
Hakika, kutoboa ni lazima, tukae tu kwenye mchakato.
LikeLike
Nitahakikisha nazungukwa na watu sahihi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nidhamu ya Hali ya juu sana kwenye kuamua na kuchukua hatua
Asante sana
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Ni kujitoa kafara kweli kweli.
LikeLike
Hakuna kujionea huruma, ni kufika kule tunakotaka ndiyo muhimu zaidi.
LikeLike
Skin in the game,dawa ni kukaa kwenye mchakato. Asante kocha. 🙂
LikeLike
Mchakato haukwepeki.
LikeLike
Nimeusikiza kwa makini walaka, pia nimeusoma kwa makini na nitaendelea kuisikiliza na kuisikiliza Tena na Tena. Kwa kifupi kabisa ninasema KAMA UNATAKA KWENDA KASI BASI NENDA PEKE YAKO . NA KAMA UNATAKA KWENDA MBALI AMBATANA NA WENGI
Asante kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana naweka kazi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitahakikisha nazungukwa na watu sahihi muda wote.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante Kocha nakaa kwenye mchakato.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nimetoa kafara ya kila kitu kwenye maisha yangu ili kujenga jamii hii.
Na sitakubali kuyaharibu maisha yangu kwa sababu ya watu ambao hawajajitoa kweli kwenye hili.
LikeLike
Huo ndiyo mstari niliouchora.
LikeLike
naamua kuteseka ili kujennga jamii iliyo bora kwa kila namna
PIA NAJUA KISIMA CHA MAARIFA NI JESHI na kitu cha kwanza nidhamu kali sana
KWENYE KUAMUA NA KUCHUKUA
( TUPO PAMOJA KOCHA)
LikeLike
Kaa kwenye mchakato kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
Asante kocha,nilikusikiliza vzr jana,nikarudia kuisikiliza tena,na leo nimesoma tena,kabla ya hapo jana siku ya ijmaa nilikuwa najiuliza na kujadiliana na mwanakisima Sebastian kaluguru namna tunavyotakiwa kupambana,ulivyokuja kueleza kama vile tulikuwa ndotoni,muhimu ni NIDHAMU KALI YA KUAMUA NA KUFANYA na kuendelea kukaa kwenye mchakato, mafanikio siyo rahisi, vinginevyo mabilionea wangekuwa wengi.asante.
LikeLike
Umefanya vyema.
Tukae kwenye mchakato kwa msimamo bila kuyumba.
LikeLike
Nalichukukia Kama tangazo au waraka wa Amiri jeshi mkuu kwenye Kambi ya Jeshi. Makabu live ukipenda umeze au uteme hakuna atakayejali. Ukweli Ni mchungu ukisemwa hadharani, nimekuelewa na nakushuru Sana Kocha sikati tamaa jitahidi.
LikeLike
Vizuri sana, tupambane, maana hii vita ni kali na watu wanaanza kulega lega.
LikeLike
Kinga ya kudumu ya kubaki kwenye KISIMA cha Maarifa ni kukaa kwenye mchakato
Nahitaji Kuwa na Nidhamu ya hali ya juu ya kuamua na kufanya.
Asante
LikeLike
NIDHAMU YA HALI YA JUU YA KUAMUA NA KUFANYA.
KUKAA KWENYE MCHAKATO KWA MSIMAMO BILA KUYUMBA.
Tukae humo, hakuna namna tutashindwa kutoboa.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato ndiyo jawabu la mambo yote
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nami nimeamua kwa dhati kabisa kuwa sehemu ya jamii ya tofauti.Nitaendelea kukaa kwenye mchakato ili kuhakikisha jamii hii inafikiwa.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Ahsante Kocha.
Nimekuelewa vizuri sana.
Dawa Ni Kukaa Kwenye Mchakato Bila Kuyumbishwa Na Chochote.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, ambao tunapenda kuona tunakubalika na watu wengine ndiyo tujisikie vizuri na kujitoa kweli kwenye kile tunachofanya.
Maneno ya kweli
LikeLike
Tuyazingatie.
LikeLike
Nimesoma nimeelewa nabakia njia kuu ambayo ni mchakato
LikeLike
Huonekani kwenye mchakato.
LikeLike