3030; Unafanya ambavyo hawafanyi.
Rafiki yangu mpendwa,
Imezoeleka kwamba, kama unataka kufanikiwa, angalia yale ambayo waliofanikiwa wanayafanya kisha na wewe uyafanye.
Kwamba mafanikio huwa yanaacha alama, kama utaangalia waliyofanya waliofanikiwa na wewe ukayafanya, utafanikiwa sana.
Ni kweli kwamba mafanikio huwa yanaacha alama.
Lakini kwenye kufanya yale ambayo waliofanikiwa wanayafanya, kuna ugumu mkubwa.
Hiyo ni kwa sababu tayari kila mtu ametingwa na mambo mengi ya kufanya.
Kila mtu, hata ambaye hajafanikiwa, tayari siku yake nzima imejaa mambo mbalimbali ya kufanya.
Hivyo kudhani mtu atapata nafasi ya kuweka yale ambayo waliofanikiwa wanayafanya ni kujidanganya.
Njia bora ya kujifunza kwa waliofanikiwa siyo kwa kuangalia wanayofanya kisha kuyaiga, badala yake ni kuangalia yale ambayo hawayafanyi kisha kuacha kuyafanya pia.
Kwa kuwa tumeona tayari kila mtu ametingwa na mambo mengi, njia ya kupunguza mambo ya kufanya ina nguvu kubwa.
Kwa kuondoa mambo mengi unayofanya ambayo hayana tija, unabaki na uwanja mpana wa kuweza kufanyia kazi yale yaliyo muhimu zaidi na yanayokupeleka kwenye mafanikio makubwa zaidi.
Watu wamekuwa wakilalamika kwamba hawana muda wa kufanya mambo muhimu.
Lakini ukiangalia siku zao nzima, tayari wametingwa na mengi wanayofanya.
Hiyo ina maana kwamba, ukipunguza mambo mengi unayofanya kwa sasa na kubaki na machache muhimu, utaweza kupata muda wa kufanya mengine muhimu unayotaka kufanya.
Muda wa kufanya chochote muhimu kabisa unachotaka kufanya upo, unachohitaji ni kuacha kufanya baadhi ya vitu unavyofanya sasa ambavyo siyo muhimu zaidi, ili ubaki na muda wa kufanya yaliyo muhimu.
Kuna zoezi moja rahisi sana kwako kufanya kama unataka kupunguza mambo mengi unayoyafanya.
Fungua ukurasa mpya kwenye kijitabu chako kisha ugawe sehemu mbili.
Upande wa kushoto orodhesha mambo yote ambayo umeyafanya ndani ya siku saba zilizopita. Andika yote kabisa bila kuacha hata moja.
Upande wa kulia andika malengo yako makubwa unayoyafanyia kazi.
Kisha chora mstari kutoka kwenye kila ulichofanya kwenda kwenye lengo ambalo kinatimiza.
Kwa vitu ambavyo vimekosa mstari unaoenda kwenye lengo, ndiyo unavyopaswa kuacha kuvifanya mara moja.
Hivyo ndiyo vitu vinavyokufanya utingwe sana wakati hakuna mafanikio makubwa unayoyapata.
Tayari kuna mambo mengi sana unayoyafanya ambayo hayana mchango wowote kwako kufanikiwa.
Anza kwa kuyatambua na kuacha kuyafanya mara moja ili utoe mwanya wa kufanya vizuri yale yaliyo muhimu na yenye tija.
Wakati wote ambao upo hai, unao muda wa kutosha kufanya chochote muhimu unachopaswa kufanya.
Pa kuanzia ni kuacha kufanya mengi unayofanya sasa, yasiyokuwa na tija.
Na kila unapowaangalia wale waliofanikiwa kuliko wewe, usijiulize nini wanafanya ambacho wewe hufanyi, bali jiulize ni vitu gani wewe unavyofanya ila wao hawafanyi?
Kujiuliza swali hilo kunakupa fursa ya kuyatambua yale yasiyo muhimu na kuachana nayo ili kuweza kuhangaika na yaliyo na umuhimu kubwa.
Punguza sana mambo unayofanya ili akili yako iweze kukaa kwa umakini kwenye yale yaliyo muhimu zaidi kufanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Namna bora ya kupata muda wa kufanya yale yaliyo muhimu kwangu ni kuacha kufanya yale yasiyo muhimu kwangu.
LikeLike
Angalia yale ambayo waliofanikiwa hawafanyi na wewe uache kufanya.
LikeLike
Asante sana. Nitapunguza kwa kiwango kikubwa sana kwasababu mambo mengi ndio yamekuwa sababu ya mimi kushindwa.
LikeLike
Napunguza mambo mengi ninyofanya ambayo hayana mchango kwenye kufikia malengo na ndoto kubwa nilizonazo,na kufokas kwenye mambo machache na ya muhimu.
Asante kocha
LikeLike
Asante kocha,nitapunguza mambo yasiyo muhimu nayananipotezea mda,na kufanya ya muhimu.
LikeLike
Matendo yaendane na malengo.
LikeLike
Nitakuwa mwangalifu kwenye matumizi ya muda kwa kuacha yale yote yasiyo na umuhiimu kwangu
LikeLike
Angalia waliofanikiwa na acha yale unayofanya lakini wao hawafanyi
LikeLike
Kama hakinipeleki kwenye ndoto yangu bas naachana nacho
LikeLike
Ukitaka kupata muda wa kufanya vitu muhimu punguza muda wa kufanya mambo yasiyokuwa na umuhimu wala tija.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Muda tayari upo, ni matumizi tu ndiyo mabaya.
LikeLike
Naacha kufanya yasiyo muhimu, Yale ambayo waliofanikiwa hawafanyi hii inanisaidia kuondoa usumbufu wote Ili kupata muda Wa kufanya Yale yaliyo muhimu kwangu, ambayo yananipeleka katika lengo.
Hakuna kingine muhimu.
LikeLike
Fokasi.
LikeLike
Mbo yote ambayo hayahusiani na kijenga biashara, sitayafanya kamwe
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Sio kuwaangalia wale wenye mafanikio wanafanya Bali ni kuwaangalia Yale wasiofanya na Wewe usifanyanye.
Asante
LikeLike
Tunafanya mengi sana yasiyokuwa na tija.
LikeLike
Asante sana Kocha
Ni kweli nilikuwa naamini ktk kufanya yale ambayo waliofanikiwa wanafanya kumbe inatakiwa kujiuliza ni vitu gani ninavyo fanya ambavyo wao hawavifanyi ili niachane navyo kabisa.
LikeLike
Vile unavyofanya ambavyo waliofanikiwa zaidi hawafanyi ndiyo vinakukwamisha sana.
LikeLike
Ili nipate muda wa kufanya yale muhimu na tija naacha yote yasiyo na tija kwenye biashara na maisha kwa ujumla.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitapunguza mambo yasiyo na tija ili nipate nafasi ya kufanya machache ya muhimu kwa umakini mkubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
1.Unafanya ambavyo hawafanyi.
2.Na kila unapowaangalia wale waliofanikiwa kuliko wewe, usijiulize nini wanafanya ambacho wewe hufanyi, bali jiulize ni vitu gani wewe unavyofanya ila wao hawafanyi?
LikeLike
Mengi tunayohangaika nayo hayana tija.
LikeLike
Njia Bora ya kufanikiwa ,ni kuangalia Yale wasiyoyafanya
wale waliofanikiwa Kisha nawe yaepuke usiyafanye na hapo nawe utafanikiwa.
Asante kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajitafuta kwa kuachana na yote yasiyo muhimu ili nipate nafasi ya kuhangaika na yaliyo muhimu sana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wakati wote ambao upo hai, unao muda wa kutosha kufanya chochote muhimu unachopaswa kufanya.
Pa kuanzia ni kuacha kufanya mengi unayofanya sasa, yasiyokuwa na tija.
Ahsante Kocha.
Nimekuelewa vizuri.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitaachaana na mambo ambayo hayana muhimu na kupambania yale yenye umuhimu mara zote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Njia Bora ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa Ni kwa kuyaangalia mambo yale ambayo hawayafanyi na mimi kuacha kuyafanya.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitanguza sana mambo ninayofanya ili akili yangu iweze kukaa kwa umakini kwenye yale yaliyo muhimu zaidi kufanya kuelekea kwenye Ubilionea
LikeLike
Fokasi kwenye machache.
LikeLike
Kweli. Wengi tunfanya memngi yasiyochangia kwenye maendeleo yetu wala ya wengine. Tuyaache hayo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha,Nitaachana na yote ambayo hayana umuhimu kwangu na kuanza kuendelea na ya msingi kwangu kufanya
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kufuata nyayo za waliofanikiwa.
LikeLike
Kwa kutokufanya ambayo hawafanyi.
LikeLike