3031; Muda wa kutosha kwenye kazi.
Rafiki yangu mpendwa,
Tupo kwenye msimu wa HAPANA, kipindi cha kusema HAPANA kwa mengine yote isipokuwa kujenga biashara zetu kuu na kufanya uwekezaji.
Lengo kuu la kuingia kwenye msimu huu wa HAPANA ni kuondokana na mambo ambayo huwa yanakuwa usumbufu kwetu na kupunguza muda wetu wa kuweka kazi.
Katika kusoma vitabu, nimekutana na barua fupi ambayo Steve Jobs aliandika kwa wafanyakazi wake mwaka 1986.
Barua hiyo imeelezea kwa ufupi dhana hii ya HAPANA ili kupata muda wa kutosha kuweka kazi.
Nitashirikisha hapa jinsi barua hiyo ilivyokuwa inaeleza, ili tuweze kujifunza na kuchukua hatua kuwa bora zaidi.
N E X T
1 7 M a r c h 1 9 8 6
M E M Ο
Kampuni yetu imejengwa kwenye msingi mkuu kwamba watu wazuri wachache wanaweza kuzalisha matokeo bora sana kama hawatasumbuliwa na;
a) kulazimika kushawishi kundi kubwa la watu kuhusu nini ni sahihi, na
b) kama wanaweza kuweka muda wao mwingi kwenye kazi zinazozalisha badala ya kusimamia wengine ambao hawawezi kufanya kazi zao vizuri.
Ili kusimamia msingi huo, napendekeza mambo haya mawili;
1) Kila mtu anahitaji muda wa kufanya kazi bila kusumbuliwa. Mikutano mbalimbali ya nje na ndani inakula muda mwingi wa kazi. Hivyo napendekeza siku ya alhamisi kuwa siku ambayo hakuna mikutano ya aina yoyote ile. Iwe ni siku ya kujifungia na kila mtu kufanya kazi yake kwa ukimya.
2) Tupitie uhitaji wetu wa watu ili kuwa na tahadhari kwenye kuajiri. Niwakumbushe kuna mstari mwembamba sana kwenye kuajiri ambao ukiuvuka unaishia kuwa na watu wengi na hapo kazi yako kubwa inakuwa kuwasimamia badala ya kuzalisha. Tusiruhusu hilo kutokea, ni bora kuwa na watu wachache hata kama itamaanisha kufanya kwa uchache. Tujenge kampuni yetu taratibu na kwa umakini.
Tutajadiliana zaidi juu ya haya kwenye mkutano wa kesho.
Asanteni.
Steve Jobs
Kuna mambo mengi sana ya kuondoka nayo kwenye barua hii fupi ya Steve Jobs.
Lakini kubwa sana ambalo napenda kila mmoja wetu kulifanyia kazi kwenye huu msimu wa HAPANA tuliopo ni kutenga muda wa kutosha wa kufanya kazi bila ya usumbufu.
Ukikagua unavyofanya kazi sasa, utagundua muda mwingi wa kazi unaingiliwa na usumbufu wa kila aina.
Kuanzia simu yako ambayo ina kila aina ya fursa ya usumbufu, ukienda kwa wengine, ni usumbufu kila kona.
Unaweza kutenga masaa 10 ya kufanya kazi kwa siku, ukaishia kufanya kazi ya uhakika kwenye masaa 2 tu.
Unakuwa na siku ndefu na yenye uchovu, lakini hakuna matokeo makubwa unayozalisha.
Hiyo ni kwa sababu masaa 8 katika 10 ya kufanya kazi, umeyatumia kwenye usumbufu.
Na hapa usumbufu tunamaanisha yale yote ambayo hayachangii moja kwa moja kwenye lengo lako kuu.
Hapa ni mapendekezo makubwa ninayokupa ya kutenga na kupangilia muda wako vizuri ili uweze kuzalisha matokeo bora.
1. Tenga masaa 10 ya kazi ya uhakika kwenye kila siku yako.
2. Masaa 2 yatumie kujenga na kupitia mifumo mbalimbali ya kuendesha biashara yako.
3. Masaa 2 yatumie kwenye kujenga timu yako ya biashara, kupitia vikao muhimu na timu yako na hata kwa mtu mmoja mmoja.
4. Masaa 4 kujenga wateja wakubwa kwenye biashara yako ambao watakuwa wa uhakika.
5. Masaa 2 ya kupitia taarifa na ripoti mbalimbali pamoja na kuboresha mikakati inayofanyiwa kazi kwenye biashara.
Hayo ni masaa 10 ya kuweka kwenye kazi kwa uhakika. Kwenye masaa hayo 10 unafanya hayo tu uliyopanga na kutokuruhusu usumbufu wowote, hasa wa simu na mikutano mbalimbali.
Mengine yote unayokuwa unahitaji kufanya, unayafanya kwenye hiyo hiyo siku yako, ila nje ya masaa hayo 10.
Unahitaji muda kwa ajili ya kujifunza, angalau masaa 2 kila siku.
Unahitaji muda kwa ajili ya mikutano ya nje.
Na unahitaji muda kwa mambo binafsi, kama kula, kutoka sehemu moja kwenda nyingine n.k.
Ili siku yako iweze kuwa bora na ukamilishe yote unayotaka kukamilisha, siku yako inabidi isiwe chini ya masaa 16 ya kazi.
Na ndiyo maana unaona msimu wa HAPANA unahitajika sana, maana ukishaondoa masaa 16 ya kazi, unabaki na 8 tu ambayo ndiyo unahitaji kulala humo humo na kuipa familia na watu wa karibu.
Bila ya kusema HAPANA kwenye kila kitu, hayo hayatawezekana.
Na pendekezo kubwa zaidi ninalokupa ni kuchagua siku moja kwenye wiki ambayo hiyo utaifunga yote kabisa kwa ajili ya kutekeleza mipango ya wiki ambayo imeshindwa kukamilika kwa sababu mbalimbali.
Ukishaipangilia wiki yako, hakikisha unakazana kuikamilisha.
Hivyo tenga siku moja ya wiki ambapo utakamilisha yote ambayo yamekwama kukamilishwa.
Siku hiyo inakuwa ni ya kazi ya uhakika kwa masaa yote 16 bila kuruhusu usumbufu wowote ule.
Siku hiyo unakuwa hupatikani kabisa kwa namna yoyote ile.
Haya ni mambo yanayokutaka ujitoe kweli kweli, lakini ambayo matokeo yake ni mazuri sana unapoyafanya kwa msimamo.
Tukae kwenye msimu huu wa HAPANA kwa uhakika ili kuweza kuzalisha matokeo makubwa na bora sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Tukae kwenye msimu wa hapana kwa uhakika.
LikeLike
Hilo halina mjadala.
LikeLike
ahsante kwa kushirikisha barua hii fupi .
Na asante kwa msimu wa hapana,,,ninakwenda kutenga siku mojakwa wiki kuwa siku ya kufanya kujisukuma zaidi nakutipatikana kirahisi bali ya kukua na kujenga biashara na uwekezaji
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa makala bora sana juu ya msimu wa hapana na mpango bora wa uwekezaji wa muda. Ni kweli tunakutana na usumbufu mkubwa wakati wote hasa sisi tulio na biashara ya huduma, kila wakati unaweza kupokea simu, je inakuwaje pale ambapo pamoja na ujenzi wa biashara hizi bado tuna jukumu la kuhudumia wateja hao, je utahesabika kama usumbufu?
LikeLike
Kweli kabisa. Hii imekaaje
LikeLike
Time blocking ndiyo mkombozi pekee, bila hivyo utakuwa zimamoto wakati wote.
LikeLike
Block muda ambao hutapokea mahitaji ya wateja, hasa mapema kwenye siku.
Halafu baada ya hapo kuwa na majukumu ambayo hayaathiriwi na mwingiliano wa simu.
Hakuna dharura kubwa inayotaka uwe unapatikana 24/7.
Hivyo ni kubadili mtazamo na kuwajengea wateja mazoea ya wakati gani unapatikana kwa urahisi.
LikeLike
Asante sana Kocha Kwa mwongozo huu
Nitaufuata
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante dana kocha, nitasema hapana kwenye manbo ambayo siyo ya msingi na nitakaa kwenye mchakato ili kujuza biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha
Ili niweze kutumia muda wangu kwa mambo muhimu na ya msingi napaswa niseme hapana mara nyingi
LikeLike
Hilo halina mjadala.
LikeLike
Haya yote yanawezekana kwa kusema hapana kwa mambo mengine yanayokula muda wetu
Masaa 2 ya kujenga mfumo
Masaa 2 ya kujenga team
Masaa 4 ya kujenga wateja bora
Masaa 2 ya kupitia riport zote
Masaa 2 ya kupata maarifa
Naenda kuiweka kwenye vitendo
LikeLike
Ukienda na ratiba hii kwa msimamo, ukianza saa 10 alfajiri, saa 12 jioni unakuwa umekamilisha mengi.
Na hapo unabaki na muda mwingi wa mambo mengine muhimu.
LikeLike
Nitaendelea kusema HAPANA,asante sana kocha kwa kuendelea kusisitiza hili.
LikeLike
Ni muhimu sana, ndiyo maana lina msisitizo mkubwa.
LikeLike
Asante kocha,Hapana ndo njia muhimu yakukwepana na usumbufu na kuweka kazi mbele.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitazingatia sana neno la leo juu ya msimu huu wa Hapana
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Asante kocha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nimesoma na kuelewa vizuri dhana hii.Vipi kwa wale walio kwenye ajira?
LikeLike
Kwenye kitabu cha Biashara ndani ya ajira nimeelezea dhana ya SIKU MBILI NDANI YA SIKU MOJA.
Kama siku yako ya kazi inaanza saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni, siku yako ya biashara inatakuwa kuanza saa 10 alfajiri mpaka saa 2 asubuhi, halafu tena saa 10 jioni mpaka saa nne usiku.
Hivyo mwajiri unampa masaa yake 8 na wewe unajipa masaa yako yasiyopungua 8.
Kw kifupi kama umeajiriwa na unafanya biashara, muda unaoweka kwenye biashara yako unapaswa kuwa sawa au zaidi ya unaompa mwajiri.
Hiyo ina maana hutakuwa na maisha ya kijamii kabisa na usingizi utakuwa anasa kwako.
Lazima ujisukume sana kuweza kununua uhuru wako.
LikeLike
Asante sana kocha, nitafanyia kazi haya ili kuutumia vizuri muda wangu. Na hili la kutenga siku moja ambayo ni ya kufanya kazi bila kuwa na usumbufu wowote ni zuri sana. Nitatenga siku ambayo nitakuwa sipatikani kwa namna yoyote ile, bali ni kufanya kazi tu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa mwendelezo wa kusema makala za MSIMU WA HAPANA.
LikeLike
Msimu wa HAPANA, umepamba 🔥🔥
LikeLike
Siku ya jmosi kuanzia wiki ijayo ni siku yangu ya kutopatikana na kujifungia kujifunza nakuboresha mfumo Wa biashara na timu.
HAPANA ni sentensi inayojitosheleza.
Nasema HAPANA Kwa mambo yote yasiyo na tija kwenye biashara na NDIO ni Moja tuu Kwa biashara.
LikeLike
Safi sana, kaa humo kwa msimamo.
Haitakuwa rahisi, watu watakuwa vikwazo, lazima ung’ang’ane sana.
LikeLike
Ni msimu wa hapana kwa mambo yote yanayopoteza muda wangu
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Asante sana Kocha nitahakikisha naweka mambo yangu vizuri nakishi maisha yangu sio kwa msimu huu tu wa HAPANA bali ktk maisha yangu yote nitakuwa natumia sentensi hii kamili inayojitosheleza “HAPANA”
LikeLike
HAPANA ni sentensi iliyokamilika kabisa. Kaa humo.
LikeLike
Tukae kwenye mchakato kwenye msimu wa hapana bila kuyumba
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana ni hakika usemavyo
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kusema hapana na kutumia namba katika tathmini huzalisha matokeo. hiki ndicho chombo changu cha kufika ubillionea wa doller.
LikeLike
Hakika,
Kila la kheri.
LikeLike
Nitatenga masaa 10 ya kazi ya uhakika kwenye kila siku yangu. Asante sana kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Bila kujitoa, haya mambo hayawezekani.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mtasema Hapana ili kuepuka mambo yasiyokuwa tija
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimekisoma makala ,na nitaendelea kuisoma Tena.
Ninakubaliana na ninayapokea mapendekezo yako yote
Matano ya kutenga na kupangilia muda WANGU vizuri
Ili niweze kuzalisha matokeo Bora.
Asante Sana kocha
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Kufanya kazi kwenye mazingira tulivu bila ya kusumbuliwa.
LikeLike
Ni muhimu.
LikeLike
Tupitie uhitaji wetu wa watu ili kuwa na tahadhari kwenye kuajiri. Niwakumbushe kuna mstari mwembamba sana kwenye kuajiri ambao ukiuvuka unaishia kuwa na watu wengi na hapo kazi yako kubwa inakuwa kuwasimamia badala ya kuzalisha. Tusiruhusu hilo kutokea, ni bora kuwa na watu wachache hata kama itamaanisha kufanya kwa uchache. Tujenge kampuni yetu taratibu na kwa umakini.
LikeLike
Maneno muhimu na yenye nguvu sana kuzingatia.
LikeLike
Nasema hapana kwa yote yasiyochangia kwenye malengo yangu .
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante sana Kocha.
Nimekuelewa vizuri.
LikeLike
Karibu.
LikeLike