3032; Ua ndoto zao.
Rafiki yangu mpendwa,
Tupo kwenye msimu wa HAPANA, msimu wa kusema hapana kwenye kila kitu isipokuwa kujenga biashara yako kuu na kufanya uwekezaji.
Kitu kimoja kikubwa ambacho utakutana nacho mara kwa mara kwenye msimu huu wa HAPANA ni lawama za watu wengine.
Kwa kuwa ulishawazoesha watu kwa namna fulani huko nyuma, kitendo cha kuwaambia HAPANA kwa mambo ambayo huko nyuma ulikuwa unayakubali, wataona umebadilika.
Hilo litawaumiza sana na hivyo kukupa lawama kwamba hujali au unajiona ni bora zaidi.
Kinachowafanya watu wakulaumu ni ndoto walizonazo kuhusu wewe.
Kila mtu kwenye maisha yako kuna ndoto kubwa aliyonayo kuhusu wewe, ambayo inahusisha yeye kupata manufaa fulani.
Yaani iko hivi, kila mtu anataka uwe vile anavyotaka yeye, ili aweze kujinufaisha kupitia wewe.
Unapokataa kuwa vile wanavyotaka, ndipo unapoibua lawama kwa wale ambao walishajipanga kunufaika kupitia wewe kuishi vile wanavyotaka wao.
Njia pekee ya wewe kufikia ndoto zako kubwa ni kuwa tayari kuua ndoto ambazo wengine wanazo juu yako.
Ndoto ambazo watu wako wa karibu wanazo kuhusu wewe ni zile ambazo zina manufaa fulani kwao wenyewe, bila kujali kama una ndoto nyingine kubwa.
Ni wajibu wako kuua ndoto zote ambazo watu wanazo kwako ili uweze kupigania ndoto yako kuu kwenye maisha yako.
Katika kufanya hayo, lazima uwe na ngozi ngumu sana.
Lazima uwe tayari kupokea lawama nyingi ambazo watu wako wa karibu watazileta kwako.
Ni lazima sana uchague kuwa wewe ili uweze kufikia ndoto kubwa ulizonazo na kuepuka mitego ambayo watu wengine wamekuwekea ili uwanufaishe wao.
Kwenye hii safari ya mafanikio, lawama hazikwepeki.
Mafanikio makubwa unayoyataka yatahitaji mabadiliko makubwa kwenye maisha yako, kuanzia kwenye fikra zako mpaka matendo yako.
Mabadiliko yoyote utakayoyafanya kwenye maisha yako lazima yataibua lawama kwa wengine. Hiyo ni kwa sababu mabadiliko yako yanavuruga manufaa ambayo walikuwa wanayapata.
Watu wanataka uendelee kwenda vile ulivyozoea kwenda, kwa sababu tayari wameshaweka njia za kunufaika na mwenendo wako.
Ni lazima uwe jasiri kuua ndoto za wengine juu yako ili kuruhusu ndoto kubwa ulizonazo ndani yako uweze kuzifikia.
Lawama nyingi utazipata mwanzoni kwa kuwa utakuwa umetikisa maisha ya wengine kwa namna fulani.
Lakini hupaswi kukata tamaa na kurudi nyuma ili kuwafurahisha.
Unapaswa kuendelea na mabadiliko uliyoanzisha, kwa sababu utakapoyapata mafanikio makubwa unayoyapigania, wale waliokuwa wanakulaumu kwa mabadiliko unayofanya watakuwa wa kwanza kukusifia.
Wajibu wako namba moja kwenye maisha yako ni kuijua na kuipambania ndoto kubwa ya maisha yako.
Ndoto nyingine zote ambazo watu wanazo juu yako unapaswa kuziua kwa kuzipuuza.
Hilo haitakuwa rahisi, litaleta kila aina ya ugomvi na lawama.
Hayo yasikutetereshe hata kidogo.
Kuwa imara ili uweze kusimamia na kuzifikia ndoto zako kubwa na hapo utakuwa na fursa ya kuwa na manufaa kwa wengi zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uwa ndoto zao, ni mchakato unaoumiza lakini utakaniweka huru na kunifikisha kwenye ndoto kubwa.
LikeLike
Huwezi kutimiza ndoto za kila mtu, pambania zako.
LikeLike
Ni kweli Kocha kila mtu anataka uwe vile anavyotaka ili kunufaika na wewe ni kazi kubwa sana kutojali ndoto za wengine na kusimamia ndoto zako, msimu huu nasema hapana kwa ndoto za wengine bali kufuatilia ndoto zangu katika kujenga biashara na uwekezaji.
LikeLike
HAPANA ni silaha muhimu sana.
LikeLike
Napambanai ndoto zangu kubwa nilizonazo kwenye maisha yangu bila kujali wengine watanionaje au kunichukuliaje kwa sasa ila nikishafikia hizi ndoto kubwa nilizo nazo watachagua wenyewe kunielewa au kuendelea kutokunielewa
Asante kocha.
LikeLike
Kabla hujatoboa utaonekana ni kichaa tu.
Ila ukishatoboa, kila mtu atajipendekeza.
Utajikuta una ndugu na marafiki hata usiowafahamu.
Tupambanie ndoto zetu.
LikeLike
Asante sana Kocha. Najua ndoto zote za watu juu yangu. Napambania ndoto zangu mpaka nizifikie
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kweli kabisa,,hii kuna watu wengi wanarubuniwa na waajiri wao kwa kuwapa vitu vodogo vidogo ili kuwafurahisha na kusahau ndoto zako.
LikeLike
Kabisa, mtego mkali sana huo.
LikeLike
Asante sana Kocha, ni kweli kabisa kwenye safari ya Mafanikio hasa hii safari yetu ya Ubilionea Lawama hazi kwepeki. Huu ni msimu wa HAPANA.
LikeLike
Ukitaka kuepuka lawama usifanye chochote, na hata hapo bado utalaumiwa.
LikeLike
Nitakuwa jasiri kupambania ndoto zangu na kutoogopa lawama , Asante sana Kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Lawama hazitabadili msimamo Wa HAPANA, HAPANA ni sentensi inayojitosheleza…sihitaji kujieleza sana…
Nitasema HAPANA Kwa ndoto zao kwangu Ili niweze kufikia ndoto yangu Kubwa ninayozipigania kufikia ubilionea
LikeLike
Ndoto za wengine kwako haziwezi kuwa sahihi kwako.
Usiogope kusema HAPANA.
LikeLike
Wajibu wangu No 1.ni kuijua na kuipambania ndoto kubwa ya maisha yangu,za wengine kuhusu mimi napaswa kuziua kwa kuzipuuza.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Wajibu wangu mkubwa kwenye maisha yangu ni kuijua na kuipambania ndoto yangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
nitaziua ndoto zao msimu huu. ahsante
LikeLike
Isisalie hata moja.
LikeLike
Asante sana kocha,nitaziua ndoto zao,na kupambania ndoto zangu kubwa nilizonazo,Neno HAPANA ni neno la msaada wangu mkubwa sana ktk kipindi kwa mambo mengi
LikeLike
HAPANA ni sentensi iliyokamilika.
LikeLike
Wajibi wako namba Moja ni kuzijua ndoto zako na kuzipigania na kuzipambania na kuachana na ndogo nyingine zisizo na mchango Kwenye maendeleo Yako.
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwakuwa nimelijuwa hili nitahakikisha nakuwa na msimamo thabit kupania ndoto zangu
LikeLike
Msimamo ni muhimu.
LikeLike
Una chaguo moja tu ,nalo ni kupambania ndoto yako.
Mengine yote ni sema hapana.
LikeLike
HAPANA bila hofu.
LikeLike
Nilichojifunza hapa ni : Ili niweze kuzifikia ndoto yangu kuu kwenye Maisha , Niwajibu wangu kuua ndoto za wengine walizonazo juu yangu , ndoto ambazo zinamanufaa kwao .
Ni makala Bora, Asante kocha
LikeLike
Hakika, tupambanie ndoto zetu.
LikeLike
Wajibu wangu namba moja ni kupigania ndoto kwa namna yeyote ile kwa hakika itakuwa hivyo
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nakuwa imara Ili niweze kuzifikia ndoto kubwa nilizonazo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nakuwa imara Ili niweze kuzifikia ndoto kubwa nilizonazo kwenye maisha yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Huu ni msimu wa HAPANA kwa yasiyokuwa ya muhimu kwangu. Vipaumbele ni Biashara yangu
Kuna watu weñgi mwanzoni wataumia Ila baadaye watazoea
LikeLike
Watazoea tu.
LikeLike
Hapa nimepata mpya kumbe unaweza kuua ndoto zao kwa kuongeza kazi na kufunga masikio kutokuwasikiliza wao na wewe ukivuka na kutimiza leo utakua msaada kwao lengo libaki kuwa kubwa ndani ya maisha yako ni kweli ni lazima kutikisa maisha yao
LikeLike
Hakika.
LikeLike
kila mtu anataka uwe vile anavyotaka yeye, ili aweze kujinufaisha kupitia wewe.
Unapokataa kuwa vile wanavyotaka, ndipo unapoibua lawama kwa wale ambao walishajipanga kunufaika kupitia wewe kuishi vile wanavyotaka wao.
LikeLike
Hakika,
Lazima kuelewa hilo kwa kina.
LikeLike
Wajibu wako namba moja kwenye maisha yako ni kuijua na kuipambania ndoto kubwa ya maisha yako.
Ndoto nyingine zote ambazo watu wanazo juu yako unapaswa kuziua kwa kuzipuuza.
Hilo haitakuwa rahisi, litaleta kila aina ya ugomvi na lawama.
Hayo yasikutetereshe hata kidogo.
Kuwa imara ili uweze kusimamia na kuzifikia ndoto zako kubwa na hapo utakuwa na fursa ya kuwa na manufaa kwa wengi zaidi.
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Wakome wanaotaka kunichuna.
LikeLike
🤣🤣
LikeLike
Kwangu mimi lawama hazinitishi ili mradi ninaamini kuwa ninachokifanya ni sahihi na kwa maunfaa yangu na pia siyo dhambi kwa Mungu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike