3059; Ahadi yangu kwako.
Rafiki yangu mpendwa,
Tangu nilipoanzisha huduma ya ukocha ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2014, sikuwa naichukulia huduma hii kama biashara, kwa maana ya kuwaangalia washiriki kama wateja.
Badala yake nimekuwa naichukulia kama huduma ninayoijenga na washiriki nimekuwa nawachukulia kama bidhaa ambayo ipo ndani ya huduma.
Ndiyo maana gharama za huduma hii zimekuwa chini mara zote, ili zisiwe kikwazo kwa wale wanaoihitaji kweli.
Mpango ukiwa ni kupitia washiriki waliopo sasa, tujenge sifa bora kabisa ya huduma hii na sifa hiyo bora iweze kuiuza huduma kwa wengi na kwa gharama kubwa zaidi.
Sasa nakwenda kubadili hilo, kwa kuifanya huduma kuwa biashara kamili na washiriki siyo tena bidhaa, bali ni wabia wa kibiashara.
Nimeacha mambo mengi sana kwenye maisha yangu kwa ajili ya kuijenga hii huduma.
Hivyo basi, kila anayeshiriki kwenye huduma hii, ninakuwa mbia wake kwenye biashara anayoijenga.
Hiyo ni kuhakikisha kwamba kila anayeshiriki huduma hii anapata manufaa makubwa na kufikia malengo makubwa aliyonayo.
Na kwa sasa lengo letu kuu ni kufikia ubilionea mwaka 2030, nitahakikisha kila mtu anajisukuma kweli kufikia lengo hilo.
Ahadi yangu kwako wewe kama mshiriki wa huduma hii ni kama ifuatavyo; KAA KWENYE MCHAKATO KAMILI WA HII HUDUMA KWA KIPINDI CHOTE TUNACHOFANYIA KAZI LENGO KUU.
NA KAMA UTASHINDWA KULIFIKIA LENGO PEKE YAKO, BASI NITAKUPA FURSA BORA ZAIDI YA KULIFIKIA LENGO KWA UHAKIKA.
Ninachosema ni kwamba, wajibu wako wewe ni kukaa kwenye huu mchakato wetu kwa msimamo na uhakika.
Na kama kwa sababu zozote zile umeshindwa kulifikia lengo la ubilionea, utapata fursa ya kuingia kwenye biashara za wengine ambazo zimeweza kufanya vizuri na kukuwezesha kulifikia lengo.
Iko hivi rafiki, tuna biashara nyingi sana na za tofauti zinazofanyika na washiriki wa huduma hii.
Kwa kanuni tu ya wastani, kuna biashara ambazo zitafanya vizuri sana na baadhi hazitafanya vizuri.
Zile ambazo zitafanya vizuri zitahitaji zaidi watu ili kuendelea kukua na kuleta manufaa makubwa.
Na hapo ndipo patakapokuwa na fursa nzuri kwa wale ambao tayari wapo kwenye huduma hii na wanauelewa vizuri mchakato kamili.
Hilo ndiyo ninalokuahidi kama mshirika na mbia wako wa kibiashara. Kaa kwenye mchakato kwa msimamo na uhakika kwa kipindi chote na kama biashara yako haitaweza kukufikisha kwenye lengo, utapata nafasi kwenye biashara nyingine zenye fursa ya kukufikisha kwenye lengo.
Rafiki, ili ushirika na ubia wowote uweze kufanya kazi, lazima ujengwe kwenye msingi mkuu wa uaminifu.
Ni lazima tuaminiane sana, kwa kusimamia misingi sahihi na kukaa kwenye mchakato muda wote.
Kwa kuwa safari ina vikwazo mbalimbali, lazima tuwe na imani kwamba vikwazo anavyopitia mtu ni vya kimazingira au kiuchumi na siyo vinasababishwa na uvivu na uzembe wa mtu mwenyewe.
Ahadi yangu itakuwa sahihi na ambayo lazima niitimize kama tu utakamilisha sehemu yako ya ahadi hii, ambayo ni kuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato.
Kama utashindwa na wakati huo huo hukai kwenye mchakato na wala huna uaminifu, unakuwa umeivunja ahadi mwenyewe.
Kama umeshindwa kwa sababu ya uvivu na uzembe wako mwenyewe, sitaweza kukupeleka mahali pengine napo ukaue biashara ambayo mwenzako amepambana sana kuijenga.
Eneo hili la uaminifu na kukaa kwenye mchakato ni nyeti sana.
Kama kutakuwa na mazingira yoyote yanayotilia shaka juu ya uaminifu wako na ukaaji wako kwenye mchakato, unakuwa umeivunja ahadi yetu.
Kama utaonyesha viashiria vya kukosa uaminifu na kutokukaa kwenye mchakato mapema, hutapata nafasi ya kuendelea na huduma hii.
Hilo ni eneo ambalo nimekuwa nalisimamia kwa ukali na umakini mkubwa, kwa sababu bila ya hivyo hakuna kitu tutakachoweza kujenga.
Tutaishia kudanganyana kwa kupeana matumaini hewa.
Hii safari ya ubilionea ni ngumu kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yako.
Inakutaka ujitoe sana, uwe tayari kuteseka na kutengwa na wengine.
Huku pia ukiwa huna uhakika sana wa kulifikia lengo.
Lakini kupitia huduma hii, nakwenda kukupa uhakika wa kulifikia lengo.
Kwani kama utalishindwa peke yako, kama utakuwa mwaminifu na mkaaji kwenye mchakato bila shaka yoyote, utapata fursa nzuri kwenye biashara zitakazofanikiwa.
Watu wengi hudhani ubilionea ni mpaka ujenge biashara yako mwenyewe.
Ni kweli kujenga biashara ni hitaji muhimu, lakini siyo lazima iwe yako mwenyewe.
Mabilionea wengi duniani ni zao la ubia wa kibiashara au kupata nafasi za juu kwenye biashara kama kuwa mkurugenzi mkuu.
Hicho ndicho ninachokuahidi hapa.
Kama utakaa kwenye huu mchakato kwa uaminifu mkubwa, kama biashara yako itashindwa, ufapata nafasi ya kuwa mbia au kufanya kazi kwenye nafasi za juu kwenye biashara ambazo zitafanya vizuri ndani ya hii huduma.
Kwa sababu kama ambavyo tunaendelea kuona, kupata watu sahihi ni changamoto kubwa sana kwenye kujenga timu ya kibiashara.
Kwa wewe kuwa mtu sahihi, utaweza kufanyia kazi kwa ubora fursa ya kuwa nafasi za juu kwenye biashara za watu wengine.
Wajibu wako mkubwa kwenye haya makubaliano yetu ni kukaa kwenye mchakato kwa ukamilifu na msimamo bila kuyumba.
Iishi misingi yetu yote kwa uaminifu mkubwa.
Jifunze kila wakati.
Jenga biashara.
Fanya uwekezaji.
Weka fokasi kwenye haya mambo muhimu.
Kama utatimiza hayo, kwa matendo yanayojionyesha na siyo tu maneno, nakuhakikishia utalifikia lengo lako kuu la ubilionea.
Kama utashindwa kulifikia peke yako, utapata fursa ya kulifikia kwa kushirikiana na wengine.
Kama utashindwa kukaa kwenye mchakato au utakosa uaminifu, huo ndiyo unakuwa mwisho wa ubia na ushirika wetu.
Hatutahitaji kuwa na mazungumzo yoyote ya mapatano, ushahidi ulio wazi wa kukosa uaminifu au kutokukaa kwenye mchakato ndiyo yatakuwa maamuzi ya mwisho.
Naamini sana kwenye huu mchakato kiasi kwamba naweza kuwa tayari kumlipa mtu aliyekaa kwenye mchakato huu kwa uhakika na asipate matokeo.
Ninajipa uhakika kwenye hilo kwa sababu najua mchakato huu unafanya kazi, kama utafanyiwa kazi.
Ndiyo maana nipo tayari kukudhamini kwa namna yoyote ile kama kweli utastahili dhamana, kwa kuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato kwa uhakika na msimamo.
Karibu twende pamoja kwenye hii safari rafiki yangu.
Nimejitoa hasa kuhakikisha unapata maarifa na miongozo yoyote unayohitaji.
Nimejitoa kukusukuma zaidi ya ulivyozoea.
Na nimejitoa kukuwajibisha hasa pale unapoyumba kwenye mchakato.
Wajibu wako ni kuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato.
Mengine yote yatakwenda sawa.
Na ubilionea utaufikia kwa uhakika.
Haya siyo matumaini hewa ninakupa.
Hii ni fursa ya wewe kupambana mpaka tone la mwisho ili kulifikia lengo.
Na kama utapambana kweli, nakuhakikishia utalifikia lengo, kama siyo peke yako, basi kwa kushirikiana na wengine.
Pambana uwezavyo uendelee kubaki ndani ya huduma hii.
Kwani mazuri na makubwa sana yapo mbele yetu kwa uhakika.
Usijinyime hayo kwa kukosa uaminifu na kushindwa kukaa kwenye mchakato kwa uhakika na msimamo.
Nimalizie kwa kusema;
Wewe siyo mteja wangu,
Wewe siyo bidhaa yangu,
Wewe ni mshirika na mbia wangu kwenye hii safari ya kujenga ubilionea.
Kamilisha sehemu yako na mimi nikamilishe sehemu yangu na kwa uhakika tutalifikia lengo hili kubwa.
Karibu sana tuendelee kuwa pamoja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha, Uaminifu na Ukaaji kwenye mchakato ndiyo tiketi ya kuwa mbia na mshirika. Naahidi kuwa mwaminifu na mkaaji kwenye mchakato kwa msimamo na uhakika.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Uaminifu na kukaa kwenye mchakato.Binafsi Nina imani kubwa sana kwenye haya.Ni swala la muda tu.Naona pia nafasi kama mabilionea kuwekeza kwenye sekta ya benki na bima kwa kuanzisha kampuni kwenye maeneo hayo.
LikeLike
Umesema vyema sana.
Sekta ya afya, kuanzia benki, bima na uwekezaji mkubwa wa kibiashara (kununua na kuuza biashara) ni eneo lenye fursa kubwa sana ambayo lazima tuifanyie kazi.
Maana sisi wenyewe tayari ni wateja wakubwa kwenye maeneo hayo.
LikeLike
Asante sana kocha, muhimu kwangu ni kukaa kwenye mchakato na kufanya yanayotakiwa, Asante sana
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitakaa kwenye mchakato na kuwa mwaminifu siku zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitapambana kuendelea kukaa kwenye mchakato ili kufikisha melengo ya Ubilionea kama klabu kwa pamoja
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha.
Mambo niliyoondoka nayo hapa,
1. Kuwa muaminifu
2. Kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Vizuri sana,
Yafanyie kazi.
LikeLike
Wajibu wangu mkubwa:
1-Kukaa kwenye mchakato kwa ukamilifu na msimamo bila kuyumba.
2-Kuishi misingi yetu kwa uaminifu mkubwa.
#Kwa kujifunza kila wakati.
#kujenga biashara.na
#kufanya uwekezaji.
Asante Kocha. 🙏🙏
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani. Nakupongeza sana kwa kuwa mbia wa biashara zetu hapa na ahsante sana. Uaminifu na kukaa kwenye mchakato kwa msimamo hakika si jambo rahisi lakini lazima yafanyike haya mawili Kwa msimamo.
Nipo tayari kuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato mara zote kama ahadi yangu ya kukaa hapa
✅🔥🤝
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante sana Kocha, msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale ni UAMINIFU. Kukaa kwenye mchakato bila kuyumba ni njia sahihi kabisa ya kufikia malengo.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante sana Kocha, msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale ni UAMINIFU.
Kukaa kwenye mchakato bila kuyumba ni njia sahihi kabisa ya kufikia malengo.
LikeLike
Asante sana Kocha, msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale ni UAMINIFU.
LikeLike
Msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale ni UAMINIFU.
LikeLike
Nitapamba niwezavyo kukaa kwenye mchakato. Kitakacho bakia ni muda tu kufikia Ubilionea
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kwa nafasi hii ya kuwa mbia na siyo bidhaa wala mteja.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Nitakaa kwenye mchakato mara zote.
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Umeni fungua sna kocha hapa na kunioendolea wasiwasi kuwa hata kama sijafanikiwa kwenye wazo langu binafsi basi kwa uzoefu ua ujuzi nitakaoujenga kupitia program ya Bilionea mafunzoni kwa kukaa kwenye mchakato bila kuyumba, nitaufikia ubilionea kwa kuwa mbia kwenye baishara za mabilionea wenzangu.
Hili limenipa hamasa na uhakika zaidi wa kukaa kwenye mchakato na kuondoa kabisa mawazo ya kukata tamaa yanayonijia.
Kama Tunavyojua Binadamu tunapenda uhakika.
LikeLike
Karibu sana tupambanie hili, ni letu sote.
LikeLike
Asante sana kocha wangu, naamini sana huu mchakato WA kuifikia Ubilionea. Kadri ya muda unavyokwenda najikuta nikiendelea kujifunza na kukua. Niishukuru sana klabu yangu ambayo pia inao watu wanaonipa hasira ya kuzidi kupambana.
LikeLike
Vizuri sana, kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha.
Nitakuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato Kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante,
Umeweka wazi nia yako ya huduma.umeshaweka mchakato wazi kazi yangu ni kufanya yale yanayonihusu kwenye mchakato huu.Karibu sana,naahidi uaminifu wa hali ya juu kwenye huduma hii na wanakisima wenzangu kuwa mwaminifu kwao kwa chochote nachoweza kushirikiana nao.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Nimalizie kwa kusema;
Wewe siyo mteja wangu,
Wewe siyo bidhaa yangu,
Wewe ni mshirika na mbia wangu kwenye hii safari ya kujenga ubilionea.
Kamilisha sehemu yako na mimi nikamilishe sehemu yangu na kwa uhakika tutalifikia lengo hili kubwa.
Karibu sana tuendelee kuwa pamoja.
Asante sana tupo pamoja
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante Kocha, Siri ya kufikia ubilionea ni kukaa kwenye mchakato huu Kwa uaminifu na msimamo bila kuyumba.
Kwa kukubali kujitesa,kutengwa na jamii na kuishi na wasiwasi Wa kushindwa
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha, nitakaa kwenye mchakato wa bilionea mafunzoni bila kuacha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nimeipenda hii na naahidi kuwa maaminifu kwa kutekeleza majukumu yangu na kuufanya ile sehemu yangu hadi tone la mwisho
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante sana nafanyia kazi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha nitakua mwaminifu na kukaa kwenye mchakato mpaka kielewe.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha muhimu kwangu ni kukaa kwenye mchakato kwa uaminifu bila kuyumba asanteni sana
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Nitakuwa mwaminifu kwa wakati wote na nitakaa kwenye Mchakato kwa wakati wote..
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,ntakaa kwenye mchakato siku zote na kuwa mwaminifu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mimi ni mbia sasa mimi sio mteja tena.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kudumu kwenye mchakato ndio silaha pekee ya kufanikiwa. Shukrani sana.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Neno mchakato na uaminifu limerudiwa mara nyingi sana huu ndiyo msisitizo mkubwa. Nitakaa kwenye mchakato kwa uaminifu.
Asante Kocha kwa kujitoa
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Asante sana kocha kwa ahadi yako kwetu. Nami naahidi kutimiza sehemu yangu kwa kuwa mwaminifu na kukaa kwenye mchakato siku zote ili hii fursa ya kufikia ubilionea kupitia ubia isinipite.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Nitajifunza kila mara.
nitakuwa mwekezaji mzuri wa mara kwa mara,
nitajenga biashara yangu ili niendelee Kuwekeza.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitakaa kwenye mchakato kwa uaminifu na msimamo,kujenga biashara na kuwekeza.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
asante sana kocha nahidi nitaka kwenye mchakato na nitakuwa muaminifu
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Asante sana Kocha muhimu kwangu ni Kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Asante Sana kocha kwa ahadi yako.
Nidhamu na kukaa ktk mchakato ndio msingi wa mafanikio yetu. Asante Sana tupo pamoja.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Asante sana kocha Kwa makala hii ya kutukumbusha wajibu wet
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
safari ya ubiione inahitaji kuwek kazi sana kuvunjsa miiko sana
na kuwa uhuru kwa kwa chochote
asante koccha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
UAMINIFU unakwenda sambamba na Mafanikio.
“Iishi misingi yetu yote kwa uaminifu mkubwa.
Jifunze kila wakati.
Jenga biashara.
Fanya uwekezaji.
Weka fokasi kwenye haya mambo muhimu.”
Nilipata Kujifunza mahali maana ya neno FOKASI ambayo ilisema kuwa ni uwezo wa kusema HAPANA kwa Yale yote yasiyokuwa na mchango kwenye malengo yako ya Sasa .
Katika msimu wetu huu wa KUSEMA HAPANA ni MSIMU WA KUFOKASI kwenye lengo letu kuu la ubilionea, na KUSEMA HAPANA kwa yale yote yanayopingana na mchakatako wetu wa BM &KISIMA CHA MAARIFA na HAPANA kwa yale yote yasiyokuwa na mchango wowote katika kulifikia lengo letu la kuwa MABILIONEA
Asante Sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kukaa katkamchakato kikamilifu kuna lipa, kwan mchakato unafanya kazi na una fursa zaidi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nina ahidi kukaa kwenye mchakato na kua mwaminifu kwenye hii safari hadi nione matokeo.
LikeLike
Vizuri na karibu sana.
LikeLike
Nitakaa kwenye mchakato bila kuchoka. Nitahakikisha nakuwa mwaminifu wa bila kutiliwa mashaka. Nitakubali kuwajibika pale nilipokengeuka na nitaweka nidhamu kali
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Nitakuwa mwaminifu na nitakaa kwenye mchakato kikamilifu.Haya tu ni tiketi ya mimi kufikia mafanikio makubwa
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato kwa uaminifu.
LikeLike
Maono yako ni makubwa mno Kocha, tukiwa kama ambavyo unaamini, kuwa Billionaires inawezekana bila shaka yoyote. Uaminifu ndio kila kitu.
LikeLike
Asante sana, ni kazi kubwa, na tutaifanya kwa uhakika.
LikeLike
Kama utashindwa kukaa kwenye mchakato au utakosa uaminifu, huo ndiyo unakuwa mwisho wa ubia na ushirika wetu.
Tukae kwenye mchakato mara zote
Asante sana
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike