3063; Kataa kushindwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Kitu kimoja ambacho nimekuwa narudia sana kukisema ni kwamba watu huwa hatupati kile tunachotaka, bali kile tunachokubali, tunachokivumilia.
Na nimekuwa nikitumia mifano rahisi ya miji mikubwa.
Ni vigumu sana ukasikia mtu amekufa kwa njaa kwenye mji wowote mkubwa.
Lakini ndani ya miji hiyo, kuna wengi ambao hawana mahali pa kulala.
Watu hao wasio na pa kulala huwa wanalala popote, hasa nje ya majengo ya biashara au majengo ambayo hayajakamilika kiujenzi.
Watu wa aina hiyo hawatavumilia kulala wakiwa na njaa, lakini watavumilia kulala nje.
Na ndiyo maana hutasikia wamekufa njaa, japo wataendelea kubaki hawana makazi yao.
Kwa sababu wamekataa kufa njaa, pale wanapokosa chakula, watafanya chochote kile ili tu wale. Watafanya kazi yoyote ili waweze kula, wakikosa wataomba na wakikosa watakuwa tayari hata kuiba.
Jambo muhimu kwao ni kula kwanza.
Na wakishashiba, mengine hayana ulazima kwao.
Kitu kikubwa sana tunachojifunza kwenye mfano huo ni kwenye maisha hatupati kile tunachotaka, bali tunachokubali au kupokea.
Wasio na makazi lazima watakuwa wanataka sana kupata makazi.
Lakini wanapokosa makazi, wanakuwa tayari kulala popote.
Wangekuwa wamekataa kabisa kulala popote, wangepambana kwa kila namna kupata makazi.
Kama ambavyo wamekataa kufa njaa, wanakuwa tayari kufanya chochote ili kupata chakula.
Kuna somo kubwa sana hapa kuhusu safari yetu ya mafanikio.
Mafanikio yako kwenye maisha yanategemea zaidi wewe kukataa kushindwa kuliko kutaka kufanikiwa.
Angalia, kila mtu anataka kufanikiwa, lakini ni watu wangapi wanaofanikiwa kweli? Ni wachache mno.
Wengi hawafanikiwi kwa sababu wanakubali, kupokea na kuvumilia kushindwa.
Pale wanaposhindwa kupata kile wanachotaka, wanakubali kupokea chochote kinachopatikana.
Kamwe huwezi kufanikiwa kwa kuwa na ulaini wa kiasi hicho.
Lazima ukatae kata kata kupokea na kukubali chochote ambacho ni chini ya kile unachotaka.
Lazima ujiwekee viwango vya juu kabisa vya mafanikio ambapo hutapokea chochote chini ya hapo.
Ni lazima upambane kwa kila namna, kufa na kupona ili ufanikiwe.
Mara ya kwanza namjua Kocha wa mafanikio Dan Pena niliona video kwenye mtandao wa YouTube ikiwa imeandikwa; Ni heri nife kuliko kuishi masikini (I will rather die than being poor).
Mara moja nikajiambia huyu ndiye mtu ninayetaka kumsikiliza.
Maana nakumbuka nikiwa mdogo, niliwahi kumwambia Mama yangu maneno makali sana ambayo mpaka leo huwa ananikumbusha.
Tulikuwa shamba na akawa ananiambia wewe hupendi kulima, maisha yako yatakuwa magumu.
Na hapo nikamjibu kwenye maisha yangu lazima nitakuwa tajiri, iwe kwa njia halali au zisizokuwa halali.
Sijui hata hiyo kauli niliitoa wapi, lakini tangu nikiwa mdogo nilichagua kuukataa umasikini.
Sasa nimekua na nimejua kuna njia halali nyingi za kupata mafanikio na utajiri, nimeondoa hilo la njia zisizo halali.
Kwenye safari yetu ya ubilionea tumetangaza vita na umasikini.
Tumeukataa umasikini kwa kila namna, hatutaki kujihusisha nao kwa namna yoyote ile.
Tunauchukia sana umasikini kiasi kwamba hatutaki hata kuutamka, hatutaki hilo neno lituzoee.
Tumemkataa huyo masikini na washirika wake wote ambao ni ujinga, uvivu, uzembe, kufuata mkumbo na kuridhika na vitu vidogo.
Kila mtu anataka utajiri,
Lakini ni watu wachache sana ambao wameukataa kabisa umasikini.
Unataka ushahidi?
Ni wangapi ambao wanadhibiti matumizi yasizidi kipato?
Ni wangapi ambao wanajilipa wenyewe kwanza, kwa kuweka akiba kwenye kila kipato kabla hata hawajakitumia?
Wangapi ambao wanafanya uwekezaji kwenye akiba wanazoweka?
Wangapi wanakazana kuongeza kipato chao?
Kama unataka utajiri na hufanyi hivyo vitu hapo juu, hakuna namna utaupata utajiri.
Kwa sababu unakuwa hujaukataa kweli umasikini.
Bado unaendelea kukumbatia tabia za kimasikini.
Kutaka ushindi kunaweza kukupa hamasa ya kuupambania huo ushindi, lakini ni kukataa kabisa kushindwa ndiko kunakufanya uwe mtu hatari.
Pale unapoondoa chaguo la kushindwa kwenye maisha yako, ndipo unapopambana kufa na kupona ili ufanikiwe.
Kataa kabisa kukubali na kupokea chochote ambacho siyo unachotaka hasa.
Fanya kila linalohitajika (siyo kila unaloweza) ili upate kile unachotaka.
Kwa sababu hata asili itakuwa tayari kukupa kile unachotaka, kama utakataa chochote chini ya hapo.
Sikutaka kuandika mengi kwenye ukurasa huu, ila kuna hili wazo limenijia hapa ambalo naona nisipolitaja sitakuwa nimetenda haki.
Watu wengi ambao wanasema hawana muda, siyo kweli kwamba hawana muda, ni kwamba tu kitu wanachosema hawana muda nacho siyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwao.
Iweje mtu apate muda wa kula mara tatu kila siku, kuoga, kujisaidia, halafu akose muda wa kusoma kitabu?
Unaipata picha?
Basi, tuishie hapo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kutaka utajiri ni kitu kimoja lakini kukataa umaskini kuna nguvu zaidi.
LikeLike
Kabisa, tuchukie kabisa kile tusichotaka.
LikeLike
Sihitaji hata kutaja hilo neno lenyewe, nitapambana kwa kila namba kufikia mafanikio makubwa sana.
LikeLike
Tumwite tu ADUI MKUU na yupambane naye kwa kila namna.
LikeLike
Nataka kufanikiwa sana na kufikia viwango vya utajiri mkubwa,ili lanibidi nikatae kushindwa iwe sambamba na matamanio yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nakataa umasikini, kupaombele Changu cha kwanza ni kuwa Bilionea .
Nitaweka akiba kwa kulipa kwanza.
Nitawekeza kwa msimamo.
Nitafanya biashara ili kufikia mafanikio ninayoyataka.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Lazima nijiwekee viwango vya mafanikio vilivyo juu sana vyengine vyo sitafanikiwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kutaka ushindi kunaweza kukupa hamasa ya kuupambania huo ushindi, lakini ni kukataa kabisa kushindwa ndiko kunakufanya uwe mtu hatari.
Pale unapoondoa chaguo la kushindwa kwenye maisha yako, ndipo unapopambana kufa na kupona ili ufanikiwe.
Asante sana
LikeLike
Kabisa, ni sawa na kuweka mgongo kwenye ukuta, huna pa kukimbilia.
LikeLike
Hata mimi niliwahi mwambia maneno makali sana
LikeLike
Vizuri sana,
Karibu utushirikishe maneno hayo na namna gani yamekusukuma kwenye maisha.
LikeLike
Kila siku nitapambana na huyu adui mkuu katika maisha yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nakataa umaskini kwa kujilipa kwanza, kuwekeza, kuhakikisha matumizi yangu yanakuwa chini ya kipato na kun’gang’ana kuongoza kipato.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ninauchukia sana umasikini kiasi kwamba siutaki hata kuutamka, na silitaki hilo neno linizoee. Huu ndio msingi muhimu sana kwangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwenye maisha,,
Hatupati kile tunachotaka bali tunachokubali au kupokea.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,nitaukataa umasikini siku zote na kutafuta utajiri kwa kuweka vipaombele muhimu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Naukataa umasikini
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Pale unapoondoa chaguo la kushindwa kwenye maisha yako, ndipo unapopambana kufa na kupona ili ufanikiwe.
Hilo neno nimeshaliondoa, asante Sana Kocha.
LikeLike
Safi sana, kila la kheri.
LikeLike
Naukata umaskini Kwa vitendo
LikeLike
Onyesha wazi wazi vitendo hivyo.
LikeLike
Nitaukataa umasikini na tabia zake zote!
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ninaweka viwango vya juu kabisa vya mafanikio na kukataa kupokea vilivyo chini ya hapo.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nakataa umasikini ni kauli inayokupa nguvu ya kupambana, kwa mfano nakumbuka kwa mara ya kwanza nilienda Moshi kijijini kwa Babu mwaka 2007 mara baada ya baba kufariki na kwenda kumzika.
Niliona mazingira ya wachaga mtu ukiwa huna fedha unavyodharaulika na kutumwa tumwa hovyo.
Nilijiambia nitakuwa tajiri kama baba mdogo ili kuepuka dharau.
Kiukweli umasikini ni laana.
Kama kitu hukitaki kweli utakipambania kisiingie kwenye maisha yako, huwezi kukubali kwa namna yoyote ile
LikeLike
Safi sana kwa hasira hiyo,
Lazima kupambana sana.
LikeLike
nakataa na kuchukia sana umaskini
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Neno Umasikini kwenye kichwa changu sijawahi kulipa nafasi,na ndio kitu kinanifanya nipambane kufa na kupona.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Umasikini haipo kabsa katika machaguo yangu, sina sababu yeyote ya kuwa masikini nimeubwa kuwa tajiri na katika uzao kizazi changu umasikini umeishia pale ambapo nilizaliwa.
LikeLike
Safi sana, pambania hilo.
LikeLike
Naukataa umasikini na washirika wake wote
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
nakata umasikini
LikeLike
Kataa kabisa.
LikeLike
Ni wangapi ambao wanadhibiti matumizi yasizidi kipato?
Ni wangapi ambao wanajilipa wenyewe kwanza, kwa kuweka akiba kwenye kila kipato kabla hata hawajakitumia?
Wangapi ambao wanafanya uwekezaji kwenye akiba wanazoweka?
Wangapi wanakazana kuongeza kipato chao?
LikeLike
Ukianza kuangalia hapo utaona wazi kwa nini wengi wanashindwa.
LikeLike
Nakataa kushindwa,naenda na kocha Dr Amani Makririta na D Pena,ni kheri nife kuliko kufa masikini,ni kheri kufukuzwa kazi niliyoajiriwa,kuliko kushindwa kufanya kazi zangu zenye tija na mwelekeo wa mabadiliko ya maisha yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike