3066; Acha kuongea.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye hii safari ya mafanikio, kuna mafanikio ya aina mbili.
Moja ni mafanikio halisi ambapo ni mtu kupata kile anachotaka, haya huwa yanahitaji mtu kuweka kazi hasa na kwa kipindi cha muda mrefu.
Mbili ni mafanikio yasiyo halisi, ambapo ni mtu kuridhika na ndoto, malengo na mipango anayokuwa nayo, haya huwa yanahitaji zaidi maneno.
Mafanikio halisi ni watu wachache sana ambao huwa wanayapata, kwa sababu yanahitaji mtu kuweka kazi kubwa na kwa juhudi kwa muda mrefu.
Mtu anakutana na vikwazo vya kila namna, lakini kwa kuwa amedhamiria na kujitoa kweli, anapata matokeo bora kabisa.
Watu wengi wamenasa kwenye mafanikio yasiyo halisi.
Hawa ni watu ambao wakipata maarifa na taarifa zozote za mafanikio wanahamasika sana.
Hamasa wanayoipata inawasukuma kuweka malengo makubwa na mpango wa kuyatekeleza.
Inapofika kwenye kutekeleza yale waliyopanga, wanaanza kutekeleza, lakini wanapokutana na ugumu, huwa hawang’ang’anii kufanya kitu hicho.
Badala yake huwa wanatoroka na kwenda kwenye malengo na mipango mingine.
Kitu pekee wanachofanikiwa watu hao ni raha ya muda mfupi wanayoipata kwa kuweka malengo na mipango upya kila wakati.
Wanapanga na kuongea sana, lakini hakuna hatua zozote wanazokuwa wanapiga.
Rafiki, njia pekee ya kuachana na mafanikio yasiyo halisi ili uweze kwenda kwenye mafanikio halisi ni kuacha kuongea.
Kuongea sana ndiyo kitu pekee ambacho watu huwa wanafurahia kufanya kwa sababu kinawafanya wajisikie vizuri wakati hakuna walichofanya.
Watu wengi kwa kueleza ndoto na malengo makubwa waliyonayo wanajisikia vizuri sana.
Lakini habari inaishia hapo, hakuna hatua yoyote kubwa wanayokwenda kuchukua.
Kwenye safari ya mafanikio makubwa, maneno na matendo huwa yanapishana.
Wale wanaoongea sana huwa siyo watendaji wazuri na watendaji wazuri huwa siyo waongeaji sana.
Maneno mengi ni sawa na kujilisha upepo tu kwa kujifurahisha.
Hivyo kuacha kuongea kunapunguza kujidanganya kimafanikio.
Kwenye hii safari kubwa ya mafanikio, maneno hayana nafasi wala mchango wowote.
Kama huna mpango wa kuchukua hatua kwenye jambo, ni bora ukaacha kuliongelea, kwa sababu maneno hayana nguvu yoyote.
Na kama una mpango wa kuchukua hatua kwenye jambo, ni bora pia ukaacha kuliongelea na kuingia kulifanya, kwa sababu kuongea kunapoteza muda ambao ungetumia kufanya.
Kama huna mpango wa kufanya kitu, achana nacho na peleka juhudi zako kwenye kile unachochagua kufanya.
Na kama una mpango wa kufanya kitu, acha kuhangaika na maneno na peleka juhudi kwenye kukifanya.
Kama kuongea ingekuwa ndiyo kufanikiwa, kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa.
Lakini mafanikio pekee yanayopatikana kwenye kuongea ni yasiyo halisi, yaani ya kujifurahisha tu, kama fedha za kuchora.
Unaweza kufurahia umeichora fedha vizuri, lakini jaribu kwenda kununua kitu na fedha uliyochora na hapo ndipo utagundua furaha yako ni ya kujifariji tu, haiendani na uhalisia ulivyo.
Fanikiwa kwenye uhalisia, kupitia kufanya na siyo kwa maneno ambayo hayaendani na uhalisia.
Acha kuongea na ufanye.
Kuna mengi utanufaika nayo kwenye kufanya kuliko kuongea pekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuongea kunapoteza muda ambao ungetumia kufanya.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maneno ni rahisi sana.
LikeLike
Na rahisi haiwezi kuleta mafanikio.
LikeLike
Mafanikio ya kweli yapo kwenye kufanya kazi na si maneno. Asante kocha kwa kutukumbusha hili.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Mtajitahidi kufanya vitendo zaidi katika maisha ili kufikia malengo ya kweli kuepuka kuwa na fedha za kuchora
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Tuna kwama sana kwenye usahili kwa kuwachukua watu wanao jieleza vizuri sana na kutushawishi, wakija kazini wana kwama kufanya kwa videndo. Makala hii imenifundisha kitu kikubwa sana,
LikeLike
Kabisa, tupuuze maneno, tuangalie vitendo.
LikeLike
Kufanya kuna nguvu kubwa kuliko kuongea.
Nakwenda kufanya badala ya kuongea sana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Acha maneno weka kazi.
Asante Kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
ahsante kocha
naenda kufanya na sio kuongea
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Acha kuongea,fanya kazi, kuna wakati mmoja niliwahi kuongea na mtu mmoja akaniambia “huwa hajishughulishi na watu wanaotaka kufanya kitu flani,bali wanaofanya kitu, maana wanao taka ni wengi wanaofanya ni wachache.
LikeLike
Kwa Kiingereza wanawaita Wantrpreneur badala ya Enterpreneur
Kwa maana kwamba wanataka (WANT) kuwa wajasiriamali, ila hawajajitoa kweli.
LikeLike
Kufanya na siyo kuongea ndiyo kunaleta mafanikio halisi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Rafiki, njia pekee ya kuachana na mafanikio yasiyo halisi ili uweze kwenda kwenye mafanikio halisi ni kuacha kuongea.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sawa kabsa. Hata wahenga walisema Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Njia pekee ya kuachana na mafanikio yasiyo halisi ili uweze kwenda kwenye mafanikio halisi ni kuacha kuongea badala yake piga kazi
Asante sana.
LikeLike
Hakuna mbadala wa kazi.
LikeLike
Kuongea hakuleti matokeo halisi,
lakini kufanya kunaleta matokeo na furaha ya kudumu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Naacha kuongea, naendelea kufanya.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Matokeo ya kweli tutayapata kwa njia ya kuweka kazi. Kazi yetu ni wapenzi wafanyakazi na siyo wapenzi wasemaji.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Safi sana, wapenzi wafanyaji na siyo wapenzi wasemaji.
LikeLike
Asante kocha,Nitajikita kwenye kazi zaidi kuliko kuongea tu bila kuweka juhudi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitapambna na kuacha kuongea sana ili kupata mafanikio halisi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mafanikio halisi na mafanikio yasiyo halisi.
LikeLike
Ni muhimu kuweza kutenganisha hivyo ili visikuchanganye.
LikeLike
Mafanikio halisi yanahitaji matendo sio kuongea sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitaacha kuongea, nitaweka vitendo zaidi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuna mafanikio ya aina mbili.
Mafanikio harisi pia mafanikio yasiyo halisi.
Ili kupata mafanikio halisi unapaswa kuweka kazi kwa muda mlefu.
Watu wasiopata mafanio halisi huwa ni wale waongeaji Sana,
Mafanikio harisi wanapata wale watendaji na wasiopenda kupoteza muda kwa kuongea sana
Asante Sana.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kama kuongea ingekuwa ndiyo kufanikiwa, kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa.ASANTE KOCHA✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maneno ni kikwazo cha kufanya, mara zote nitakuwa mfanyaji kuliko mnenaji.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mafanikio yapo katika kutenda na si katika kuongea.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kweli huwezi kununua bidhaa na hela za kuchora badala yake tufanye kazi ili kazi ieleze uwepo wetu
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
maneno mengi hayaleti mafanikio
LikeLike
Kabisa.
LikeLike