3070; Mchezo wa milele.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna aina mbili za michezo, ambazo ni michezo yenye mwisho na isiyo na mwisho.
Michezo yenye mwisho huwa inachezwa kwa lengo la kupata ushindi, wakati michezo isiyo na mwisho ikichezwa kwa lengo la kuendelea kucheza.
Michezo yenye mwisho huwa ina sheria kali ambazo lazima zifuatwe na watu wote, maana ndiyo zinaamua nani ameshinda na nani ameshindwa. Michezo isiyo na mwisho haina sheria kali za kufuatwa na kila mtu, kwa sababu haina ushindi wa aina moja.
Michezo yenye mwisho huwa inahusisha kuwashinda watu wengine, wakati isiyo ba mwisho ikihusisha kutumia uwezo mkubwa ulio ndani ya mtu.
Michezo yenye mwisho, ina mwisho mmoja kwa watu wote, wakati isiyo na mwisho ikiwa endelevu ambapo watu wanakuja na kuondoka.
Kwa maelezo hayo ya michezo yenye mwisho na isiyo na mwisho, umejifunza nini kwenye safari yetu ya mafanikio?
Kuna mengi sana unayoweza kujifunza, lakini moja kubwa ni kwamba kama utayachukulia mafanikio kama mchezo wenye mwisho, kamwe huwezi kushinda. Lakini kama utayachukulia mafanikio kama mchezo usio na mwisho, kamwe huwezi kushindwa.
Kwa kuchukulia mafanikio kama mchezo wenye mwisho, utakuwa unapambana kupata kitu fulani. Ukishakipata utaacha kuendelea na safari hiyo na hapo utaanza kupata anguko.
Ndiyo maana kuchukulia mafanikio kama mchezo wenye mwisho kunakupa uhakika wa kushindwa.
Kwa kuchukulia mafanikio kama mchezo usio na mwisho, haijalishi umepata matokeo gani, utaendelea na safari, utaendelea kupambania mafanikio zaidi. Kwa sababu wakati wote unakuwa kwenye safari ya mafanikio, hakuna namna unaweza kushindwa. Maana kushindwa ni pale mtu anapoacha kujaribu.
Kama utaanguka mara saba na kuamka mara ya nane, hujashindwa.
Swali la msingi kabisa kwako ni kwenye safari yako ya mafanikio, upo kwenye mchezo gani?
Usijidanganye kwamba upo kwenye mchezo usio na mwisho, bali angalia sifa ulizonazo.
Kama kuna kitu kimoja unachopambania ambacho unajiambia ukikipata umemaliza, kama unaiga yale wengine wanafanya, upo kwenye mchezo wenye mwisho na mwisho wako ni kushindwa.
Kama umejitoa kukaa kwenye mchakato wa mafanikio bila ukomo, kama unafanya vitu tofauti na vinavyoendana na wewe badala ya kuiga wengine, upobkwenye mchezo usio na mwisho na tayari upo kwenye ushindi.
Kuna mwekezaji mmoja ambaye kabla hajawekeza kwenye kampuni changa huwa anawauliza waanzilishi wakipata bei gani watauza kampuni hiyo?
Hilo huwa ni swali la mtego.
Wakimtajia bei ambayo watauza, huwa hawekezi, maana anajua wanacheza mchezo wenye mwisho na hawawezi kufanikiwa.
Lakini wakimwambia hawatauza kwa bei yoyote ile, anajua wapo kwenye mchezo usio na mwisho, huwa anawekeza, kwa sababu anajua ushindi ni uhakika.
Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuwa kwenye safari yetu ya Ubilionea.
Kama unakaa kwenye mchakato wa safari ya ubilionea ili tu uwe bilionea, kwa maana kwamba ukishakuwa bilionea utaachana na mchakato huo, tayari umeshashindwa.
Nafasi ya kuupata ubilionea itakuwa ndogo sana na hata ukiupata hutaweza kudumu nao.
Kama unakaa kwenye mchakato wa safari ya ubilionea kwa sababu ndiyo mchakato umechagua kwenda nao maisha yako yote bila ukomo, tayari umeshaupata ushindi.
Hiyo ni kwa sababu namna unavyoyaishi maisha yako unakuwa umeridhika nayo.
Rafiki, hatupo kwenye safari hii ya ubilionea kwa ajili ya leo na kesho.
Tupo kwenye safari hii milele, kwa kipindi chote cha maisha yetu.
Kama kuna ahadi ya kweli ya kifo kikutenganishe, basi ni wewe na huu mchakato.
Najua ahadi hiyo imekuwa inavunjwa kwenye maeneo mengine ya maisha, lakini inapokuja kwenye safari yetu ya Ubilionea, usiivunje.
Umechagua kukaa kwenye huu mchakato milele, kwa maisha yako yote, mpaka kifo kikutenganishe.
Hukai kwenye mchakato kwa sababu ya matokeo fulani unayotegemea kupata.
Bali unakaa kwenye mchakato kwa sababu ndiyo maisha uliyochagua, ambayo unayapenda na hakuna namna unaweza kuyaacha.
Hayo ni rahisi kusema, lakini magumu sana kuyaishi.
Ndiyo maana ni wachache sana wanaopata mafanikio makubwa na ya kudumu.
Wengi wanacheza mchezo wenye mwisho, sisi tunacheza mchezo wa milele.
Hakuna namna tunaweza kushindwa, maana hakuna tunayeshindana naye.
Wito wangu kwako wewe rafiki yangu ni kuchagua kukaa kwenye huu mchezo wa milele na kuacha kuhangaika na michezo yenye mwisho.
Kukaa kwenye mchakato wa safari ya ubilionea ndiyo ushindi wenyewe.
Mengine yoyote yanayokuja ni ya ziada, hayatuvurugi kwa namna yoyote ile.
Hivyo ndivyo tunavyokuwa na uhakika wa ushindi kwenye hii safari.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nimechagua kukaa kwenye mchakato bila Kokomo na mchezo wa milele na siyo mchezo ambao una mwisho.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
Na heri ya kuzaliwa rafiki yangu.
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Safari ya ubilionea kwangu ni ya milele. Sio kwamba nimechagua tu kuyaishi haya maisha bali ndio maisha ninayopenda kuyaishi tangu nimeanza kuwa kijana.
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
Kifo ndo kinitoe kwenye mchakato huu wa BM ,Uh Asante sana kocha nimetoa tongo tongo zlizoniganda machoni pangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Wengi wanacheza mchezo wenye mwisho, sisi tunacheza mchezo wa milele.
Hakuna namna tunaweza kushindwa, maana hakuna tunayeshindana naye.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Kudumu kwenye mchakato na siyo kushinda hilo ndiyo linalowaangusha wengi waliopata mafanikio kidogo wanajiona wamefika na kubweteka kumbe ushindi ni kudumu kwwenyee mchakato maisha maana hakuna unayeshindana naye tule game hadi tutenganishwe na kifo s
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kama unakaa kwenye mchakato wa safari ya ubilionea ili tu uwe bilionea, kwa maana kwamba ukishakuwa bilionea utaachana na mchakato huo, tayari umeshashindwa.
Nafasi ya kuupata ubilionea itakuwa ndogo sana na hata ukiupata hutaweza kudumu nao.
Asante sana
LikeLike
Kabisa, kukaa kwenye mchakato ndiyo mafanikio yenyewe.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nipo kwenye mchezo ambao hauna mwisho
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwenye ubilionea nacheza mchezo usio na mwisho…
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Wengi wanacheza mchezo wenye mwisho, sisi tunacheza mchezo wa milele. Hakika nitakuwa hapa kwa kadri ya kibali
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Huu mchezo wangu hauna mwisho. Fainal Ni Kifo hivyo kanuni zake Ni endelevu na ushindi Ni uhakika
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nashindwa tu pale ninapoacha kujaribu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nachagua kukaa kwenye mchezo wa milele kwani huu ndiyo sehemu yangu sahihi kuwemo mingine naachana nayo.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitapambana kucheza mchezo wa milele
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nimeamua kuyachukulia mafanikio kama mchezo usio na mwisho, haijalishi napata matokeo gani, niaendelea na safari na nitaendelea kupambania mafanikio zaidi.
Nacheza mchezo wa milele.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimechagua kucheza mchezo wa maisha yangu yote ya hapa duniani napamba na sipo tayari kufika mwisho Hadi kifo kinitenfanishe
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mafanikio ni mchezo wangu wa milele,
Nimeamua kuucheza bila kujali matokeo na nitaendelea kupambania mafanikio zaidi kwa sababu wakati wote nakuwa kwenye safari ya mafanikio.
Nitakaa humu kwa sababu ndio maisha yangu niliyoyachagua, ninayoyapenda nahakuna namna naweza kuyaacha.
LikeLike
Mchezo wa milele, safi sana.
LikeLike