3099; Usinywe tu, bali ogelea kabisa.
Rafiki yangu mpendwa,
Safari yetu ya mafanikio ni kama vita.
Unapokuwa vitani, chochote kinachoweza kukusaidia kupambana na adui kinatumika vizuri kabisa.
Iwe ni silaha, watu, taarifa, mazingira au hata hali ya hewa.
Na kadiri kitu kinavyokuwa na manufaa, ndivyo kinavyotumika kwa wingi na ukubwa.
Kwenye hii safari ya mafanikio, moja ya silaha muhimu tunazohitaji ni hamasa.
Ugumu na changamoto za hii safari vinafanya kukata tamaa kuwe rahisi sana.
Inahitajika hamasa kubwa sana kuweza kuvuka yote hayo na kubaki imara.
Kuna njia mbalimbali za kupata hamasa, ya nje na ya ndani.
Hamasa ya nje huwa inaamsha hamasa ya ndani na kumpa mtu nguvu ya kuendelea na mapambano.
Watu wengi hutania na kubeza hamasa ya nje kama dawa ya miti shamba ambayo mtu anakunywa, yenye ahadi ya kutimu mengi lakini isiyokuwa na uhakika.
Kama tutaamua kuchukulia hamasa hiyo ya nje kama dawa, wewe hupaswi tu kuinywa, bali unapaswa kuogelea ndani yake kabisa.
Yaani unapaswa kuipata kwa wingi sana ili ikupe nguvu kubwa ya kupambana.
Zungukwa na yale yanayokupa hamasa hiyo ya nje kwa wingi na mara zote.
Tumia yale yote yanayokupa hamasa ya nje ili kuchochea hamasa ya ndani na uweze kujisukuma kwa zaidi ya ilivyo kawaida.
Kama kuna vitu unasoma, kusikiliza, kuangalia au kufanya na vinakupa hamasa, fanya hivyo kwa wingi.
Kama kuna watu ukiwa nao au kuna mahali ukikaa unapata hamasa fanya hivyo.
Usijione kama una mapungufu kwa kuhitaji kupata hamasa mara kwa mara.
Kadiri safari ya mafanikio inavyokuwa kubwa, kadiri malengo yanavyokuwa makubwa, changamoto pia zinakuwa nyingi na kubwa na hivyo unahitaji hamasa kubwa zaidi.
Na kama tulivyoona hapo juu, ukiwa vitani, chochote kinachokusaidia kupambana na adui kinapaswa kutumika kwa wingi na uhakika.
Kwenye vita yako ya mafanikio, usiache kutumia silaha ya hamasa kwa wingi na uhakika.
Chochote kinachokupa hamasa, kitumie kwa wingi na ukubwa mno.
Kila unapokutana na kitu chochote ambacho kinafanya kazi, unapaswa kukitumia vizuri kwa manufaa ya hali ya juu.
Usiache kitu kwa sababu umekitumia sana na kukichoka.
Badala yake endelea kukitumia kwa uhakika kadiri kinavyoendelea kukupa matokeo mazuri.
Usikitumie kwa udogo (kunywa) bali kitumie kwa wingi sana (kuogelea) ili kiweze kukupa matokeo makubwa sana.
Unaweka juhudi ili upate matokeo.
Unapopata chochote kinachowezesha juhudi zako kuleta matokeo makubwa na mazuri, unapaswa kukitumia vyema.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsnate sana kocha, nitatafuta kila chanzo cha hamasa kinachonifanya niweke juhudi zaidi
LikeLike
Kila kitu kitumike, hiyo hamasa ni muhimu sana.
LikeLike
Chochote kinachokupa hamasa kitumie kwa wingi.Hamasa inahitajika sana kwenye safari hii ngumu tunayoiendea.
LikeLike
Hamasa tunaiihitaji kwa wingi sana, sana yaani.
LikeLike
Unapokuwa vitani, chochote kinachokuwezesha kupambana na adui kinatumika vizuri.
LikeLike
Hakuna kuchezea matirio.
LikeLike
Hamasa ndio kichocheo muhimu sitapuuza.
LikeLike
Muhimu sana kuendelea kuichochea.
LikeLike
Unapokutana na kitu ambacho kinafanya kazi kutumia kama hamasa kwa kiwango cha juu.
LikeLike
Tumia vizuri sana.
LikeLike
Chochote ambacho unakitumia na kukupa hamasa kitumie kwa hali ya juu.
Asante sana
LikeLike
Kitumike kwa hali ya juu mno.
LikeLike
Nitatumia yale yote yanayonipa hamasa ya nje ili kuchochea hamasa ya ndani ili niweze kujisukuma zaidi ya ilivyo kawaida. Asante sana kocha.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Hamasa ni silaha muhimu kwenye hii safari ya kusaka mafanikio.
Asante Kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kama kuna vitu unasoma, kusikiliza, kuangalia au kufanya na vinakupa hamasa, fanya hivyo kwa wingi.
Kama kuna watu ukiwa nao au kuna mahali ukikaa unapata hamasa fanya hivyo.
LikeLike
Tunaihitaji mno hamasa.
LikeLike
.
Kwenye vita yako ya mafanikio, usiache kutumia silaha ya hamasa kwa wingi na uhakika.
Chochote kinachokupa hamasa, kitumie kwa wingi na ukubwa mno.
Asante sana
LikeLike
Hamasa inahitajika sana.
LikeLike
Hamasa ni slaa tosha kwenye vita yangu ya kusaka mafanikio,na hasa hapa ambapo nina kocha mwandamizi wa mafanikio.
LikeLike
Safi sana, itumie vyema silaha hiyo.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kweli tumia hamasa ikupe mafanikio
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya kwa nguvu na juhudi kubwa kuleta mafanikio na chochote kile kinachotokana na nguvu zangu kubwa inabidi kukitumia vyema.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Safari ya mafanikio ni Kama vita, ugumu na ChangaMoto
za hii safari zinakatisha tamaa kabisa. Hamasa ya Hali
ya juu inahitajika kuweza kuvuka hayo na kubaki salama.
Zunguukwa na watu au vitu vinavyokupa hamasa
Na endelea kupambana utafanikiwa
Asante Sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Usiache kitu kwasababu umetumia sana na kukichoka
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Chochote kinachokupa hamasa, kitumie kwa wingi na ukubwa mno.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Miziki ya Video za Dansi na Bongofleva huwa inanipa hamasa Sana hasa Christian Bella na Diamond Playnums huwa inanipa hamasa ya kuzonga mbele.
LikeLike
Tumia vizuri hiyo hamasa.
LikeLike
Chochote kinachonipa hamasa, napaswa nikitumie kwa wingi na ukubwa mno.Asante sana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
nitasoma,kumsikiliza, na kuangalia kile kinachonipa hamasa ili niweze kufanikiwa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni muhimu kuwa na silaha ya anasa
LikeLike
Hamasa siyo?
LikeLike
Tumia chochote kinachoweza kuifanya hamasa yako kuwa juu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Unapopata chochote kinachowezesha juhudi zako kuleta matokeo makubwa na mazuri, unapaswa kukitumia vyema.
LikeLike
Kabisa, kitumie hasa.
LikeLike