3117; Usife.
Rafiki yangu mpendwa,
Bilionea Charlie Munger, mshirika wa karibu wa Warren Buffett huwa anaishi kwa kanuni hii; “Ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa, ili nisiende hapo.”
Anaiita kanuni ya kugeuza, kuanza na matokeo fulani kisha kujiuliza nini kifanyike kwa sasa kuzuia.
Munger ana miaka 99 na ni Bilionea, hivyo hiyo kanuni yake inafanya kazi kwa uhalisia.
Rafiki, kifo ndiyo hali pekee ya kudumu kwenye maisha yetu.
Mtu unaweza kubadili kila kitu kwenye maisha yako isipokuwa kifo.
Unaweza kufanya makosa mengi kwenye maisha yako, lakini yote utaweza kuyasahihisha kama tu utaendelea kuwa hai.
Hivyo basi, kosa kuu na kubwa kwa kila mtu ni kufa.
Na hapa kufa haimaanishi tu kimaisha, bali kwa kila kitu tunachofanya.
Kwa mfano kwenye biashara unaweza kusahihisha makosa mengi unayokuwa umeyafanya, kama tu biashara bado itakuwa hai. Biashara ikishakufa, hakuna namna unaweza kuboresha chochote kile.
Tunapaswa kuhakikisha chochote tunachofanya tunaepuka makosa ambayo yatapelekea kwenye kifo kabisa.
Cheza mchezo wako wa mafanikio kwa kuangalia muda mrefu zaidi.
Kwa muda mrefu, kila aliyedhamiria kitu fulani ameweza kukipata.
Lakini sharti la kwanza ni kuwa hai na kuendelea na mapambano.
Dhana ya usife inakutaka upime kila hatari kabla hujaingia.
Wajibu wako ni kuepuka zile hatari ambazo zinaweza kukupeleka kwenye kifo ili ubaki kwenye mapambano kwa muda mrefu zaidi.
Kama bado upo hai, ni kiashiria kwamba una nafasi ya kubadili yote uliyofanya huko nyuma.
Hivyo badala ya kupoteza muda na nguvu kwenye kujutia uliyofanya huko nyuma, zitumie kuboresha zaidi.
Hitaji rahisi kabisa la kupata ushindi kwenye jambo lolote la maisha yako ni kukaa kwenye jambo hilo kwa muda mrefu zaidi.
Kwani kuna hata hali ya kukutana na bahati nzuri ambazo zinakupa manufaa.
Lakini hayo yote ni kama bado utakuwa kwenye kitu hicho.
Ikiwa umeondoka, unakuwa umefuta fursa zote za mbeleni.
Dhana hii ya usife ni muhimu sana.
Kadiri unavyokaa kwenye kitu chochote kile kwa muda mrefu zaidi, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri na ya uhakika ya kufanikiwa.
Jua ni wapi ukienda au nini ukifanya utakufa ili usiende au kufanya.
Wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha unadumu kwenye mchezo wako wa mafanikio kwa muda mrefu zaidi.
Muda ni silaha nzuri ya ushindi ukiwa upande wako.
Hakikisha muda unakuwa upande wako kwa kuepuka kifo cha aina yoyote ile.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Wajibu wangu mkubwa ni kuangalia ni wapi nikienda nitakufa ili niepuke kwenda sehemu hiyo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, kifo ndiyo mwisho wa mchezo, tuhakikishe hatukiharakishi.
LikeLike
Ni nuhimu kujua kuwa tusiende wapi ili tusife ili tuepuke hapo na kutokwenda hapo lakini kama tunaishi maana yake tunaweza kudumu tena kwenye mafanikio na kupata ubilionea
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Dhana hii ya usife ni muhimu sana.
Kadiri unavyokaa kwenye kitu chochote kile kwa muda mrefu zaidi, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri na ya uhakika ya kufanikiwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaepuka hatari zitakazopelekea kifo na kukaa kwenye mapambano kwa muda mrefu.
Nitadumu kwenye mchezo wangu wa mafanikio kwa muda mrefu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ahsante sana kocha, kama bado nipo hai nina nafasi ya kubadili yotr niliyoyafanya huko nyuma. Nitaweka juhudi na kujituma zaidi ili kufika lengo langu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Muda ni silaha nzuri ya ushindi ukiwa upande wako.
Hakikisha muda unakuwa upande wako kwa kuepuka kifo cha aina yoyote ile.
LikeLike
Tukae upande mzuri wa kuhakikisha ushindi.
LikeLike
Asante kocha,Niwajibu wangu kukaa na kudumu kwenye mchezo wangu kwa mda mrefu na ndo ntaweza kufanikiwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muda ni silaha nzuri ya ushindi ukiwa upande wako.
LikeLike
Tuitumie vizuri.
LikeLike
Sitakufa, nitahakikisha nakaa kwenye mchakato kwa muda mrefu ili nifikie mafanikio makubwa
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Asante kocha hii dhana ya usife ni muhimu sana kwa hiyo wajibu wangu mkubwa nikuangalia ni wapi nikienda nitakufa ili niepuke kwenda sehemu hiyo.
Pia nimejifunza kwamba kukaa kwenye biashara kwa muda murefu zaidi ndivyo ninavyo jiweka kwenye nafasi nzuri na ya uhakika yakufanikiwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muda ni silaha nzuri ya ushindi ukiwa upande wangu.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Wajibu wangu ni kujua wapi nikienda au nini nikifanya nitakufa ili niepuke kwenda huko na niepuke kufanya jambo hilo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitaepuka kifo kwa kuweka umakini
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Tutulie kwenye mchakato matokea yatakuja tu.
LikeLike
Huo ni uhakika.
LikeLike
Nitaepuka ni wapi nikienda nitakufa?? Asante sana strong
LikeLike
Karibu
LikeLike
Jua ni wapi ukiende au Nini ukifanya utakufa ili usiende au kufanya. Wajibu wangu ni kukaa kwenye mchakato
Wa mafanikio kwa muda mlefu.
Asante kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kwa kanuni ya Bilionea Charlie Munger
Hakika “Muda ni siraha nzuri ya ushindi ukiwa upande wangu, nitaendelea kuheshimu hili.
LikeLike
Karibu
LikeLike