Kila mmoja wetu huwa anajua tarehe ya kuzaliwa kwake, lakini tarehe ya kufa huwa haijulikani kwa mtu yeyote yule huwa tunapenda kuvuka madaraja kabla hata hatujayafikia kwa sababu ya kuishi wakati ujao, badala ya kuishi wakati uliopo.

Zoezi la kulala ni kama vile kifo, hujui hata utaamkaje. Lakini unajikuta tu umeamka salama, wengine hawaamki.

Mwanafalsa Seneca anatushirikisha jinsi ya kumaliza siku zetu, hatupaswi kuzimaliza siku zetu kama vile mbuzi, bali tunapaswa kuzimaliza siku zetu kama vile binadamu ambaye anaishi misingi ya falsafa ya Ustoa.

Kila siku ni zawadi, na tunapaswa kuitumia zawadi hiyo vizuri kiasi kwamba hutakuja kujutia, pata picha ukiambiwa leo ndiyo siku yako ya mwisho kuishi hapa duniani, utapata muda wa kujisumbua na yale ambayo siyo muhimu?

Nukuu;
Glad and cheerful, let us say, as we go to our rest: ‘I have finished living; I have run the course that fortune set for me’. If God gives us another day, let us receive it with joy. The happiest person, who owns himself more fully, is the one who waits for the next day without anxiety. Anyone who can say, ‘I have had my life’ rises with a bonus, receiving one more day. – Seneca,

Seneca anasema,
Kila unapoimaliza siku yako jiambie kwa furaha na uchangamfu nimemaliza kuishi, nimemaliza mwendo ambao asili imenitengenezea. Kama Mungu atanipa tena siku nyingine, nitaipokea kwa furaha. Mtu mwenye furaha anajimiliki yeye kwa ujumla, anaisubiri siku nyingine bila ya wasiwasi. Yeyote anayejiambia nimeyamaliza maisha yangu, anapata zawadi ya siku nyingine tena ya kuishi.

Kila siku unapaswa kuishi maisha yako kama mwanafalsa Seneca, kabla hujaingia kitandani jiambie kwa furaha na uchangamfu mkubwa nimemaliza kuishi. Nimemaliza mwendo ambao asili imenitengenezea.

Usiwe na uhakika wa siku nyingine, kuwa na uhakika na sasa , kama unaweza kufanya kile unachopaswa kufanya , kifanye tu kwa sababu hatuna uhakika na kesho.

Hatuna uhakika wa kesho lakini pale tunapopewa zawadi ya kuendelea kuishi, tunaishukuru asili na kuendelea kuishi.

Kila siku unapoamka asubuhi kama Mungu atakupa tena siku nyingine, utaipokea kwa furaha kwa sababu ni zawadi ya kipekee ambayo inakusaidia kuendelea kutimiza malengo uliyojiwekea.

Hatua ya kuchukua leo; kila siku kabla hujalala, jiambie nimemaliza kuishi na kama Mungu atakupa tena siku nyingine siku nyingine.

Kwenye maisha unapaswa kuwa na shukrani, kuwa mnyenyekevu kwa kila siku yako na pale unapoimaliza siku yako, jiambie nimemaliza kuishi maisha yangu, na kama nikipata zawadi nyingine ten ya kuishi.

Rafiki na mstoa mwenzako
Mwl Deogratius Kessy