3129; Ni kodi unayotakiwa kulipa.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha yetu yamekuwa magumu na yenye changamoto mbalimbali kwa sababu ya matarajio yasiyokuwa sahihi ambayo tunakuwa nayo.
Tunataka dunia iende kama tunavyotaka sisi wenyewe, wakati dunia haijui hata kama tupo hai.
Dunia huwa inajiendesha kwa kanuni zake za asili, bila ya kujali nini sisi tunataka au hatutaki.
Kwa mfano kama unataka kufanya kazi zaidi, lakini giza limeingia, unaweza kuvurugwa utakavyo, lakini huna cha kufanya.
Dunia haiwezi ghafla ikaanza kukuangalia wewe ni muda wa mwanga kiasi gani unahitaji ili ikupe. Yenyewe itaendelea kujizungusha kwenye mhimili wake na kuleta usiku na mchana kwa usawa.
Maisha tunayoishi hapa duniani, yana kodi mbalimbali ambazo tunapaswa kuzilipa.
Kujaribu kukwepa kodi hizo ndiko kumekuwa chanzo kikubwa cha changamoto kwa maisha ya wengi.
Hapa sizungumzii kodi ambazo unajua kabisa unatakiwa kulipa, kama vile za nyumba au za serikali.
Bali nazungumzia gharama mbalimbali za aina ya maisha unayochagua kuishi hapa duniani.
Kuoa au kuolewa kunakuja na manufaa yake, lakini pia kunaambatana na gharama za kulipa. Kadhalika kutokuoa au kuolewa, kunakuwa na gharama zake za kulipa.
Kuajiriwa kuna manufaa yake fulani, lakini pia kunaambatana na gharama za kulipa.
Kadhalika kufanya biashara, kuna manufaa na gharama.
Ni uchague kipato kidogo na cha uhakika au kipato kikubwa kisichokuwa cha uhakika.
Kushirikiana na watu wengine kwenye jambo lolote lile kuna manufaa ya kupata mchango wa wengine.
Lakini pia kunakuja na gharama ya kuchelewa kufanya maamuzi kwa sababu wengine lazima pia wahusishwe.
Na hapo bado kuna hali za kutokuelewana baina ya watu.
Kutokufanikiwa kuna gharama ya kudharauliwa na kupuuzwa na wengine. Wakati kufanikiwa kuna gharama ya kuchukiwa na kuwindwa na wengine.
Kabla hujafanikiwa unaweza kuona maisha ni magumu sana kwako na kudhani kwa kufanikiwa utayarahisisha.
Utapambana sana ili ufanikiwe, halafu ndiyo unagundua mafanikio nayo yanakuja na gharama zake pia.
Huwa nacheka sana pale mtu anaponiambia lengo lake ni kumaliza kabisa changamoto anazopitia kwenye maisha.
Najiambia huyu hajui anachopanga, utatuzi wa changamoto moja ni uzao wa changamoto nyingine.
Ndivyo maisha yanavyokwenda, huwezi kukwepa hilo.
Hivyo basi, badala ya kukwepa kila aina ya changamoto, ni vyema kujiandaa kuzikabili changamoto kubwa zaidi.
Badala ya kuangalia maisha yasiyokuwa na gharama, ni vyema kujiandaa kulipa gharama kubwa zaidi.
Kila maisha yanapoleta changamoto kwako, usichukie wala kulalamika, badala yake furahia, kwa sababu ni ishara kwamba unakua.
Kama changamoto ulizonazo ni zile zile ambazo umekuwa nazo mara zote, haimaanishi kwamba wewe ni mjanja sana, bali inamaanisha unabaki pale pale, hukui.
Kwa mfano, unapoanzisha biashara yako, ambayo unakuwa peke yako, unakuwa na udhibiti mkubwa wa biashara hiyo. Lakini unakuwa na changamoto kubwa sana za uchovu wa kufanya kila kitu peke yako na huo unakuzuia kukua.
Unapoamua kuajiri wafanyakazi kwenye biashara hiyo ili utatue changamoto yako ya uchovu, utaitatua, lakini utakuwa umezalisha changamoto nyingine mpya, ambayo ni ya usimamizi wa watu.
Watu wana tabia zao mbalimbali ambazo ni tofauti kabisa na za kwako.
Ungetamani wakupe tu kazi unayotaka na waweke tabia zao pembeni, lakini kwa bahati mbaya wanaambatana na hizo tabia, kama boga na ua lake.
Hivyo unakuja kukuta tabia binafsi za wafanyakazi wako kwenye biashara, zinaiathiri biashara pia.
Na hapo unakuwa na gharama za ziada za kusimamia tabia hizo binafsi zisiathiri biashara unayojenga.
Hivyo ndivyo maisha yanavyokwenda hapa duniani.
Hakuna kitu cha bure.
Huidai dunia chochote.
Inakupa hifadhi.
Kuna gharama lazima uzilipe.
Unaweza kuchagua kuzilipa na kukua zaidi.
Au ukazilalamikia na ukabaki pale ulipo.
Maisha ni yako na uchaguzi ni wako.
Malalamiko yoyote unayoweza kuwa nayo, hayamwathiri mtu mwingine yeyote isipokuwa wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha Kwa ujumbe huu. Changamoto zetu ni kipimo Cha ukuaji. Kama unafanya utalipa, na Hata kama hafanyi utalipa. Ni lazima Dunia itakuletea kitu ambacho hukijui upambane nacho.
Maisha ni mfululizo wa kuendelea kujifunza na kutatua changamoto.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hakuna kitu cha bure.
Huidai dunia chochote.
Inakupa hifadhi.
Kuna gharama lazima uzilipe
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
ASante Sana kocha nimechagua kupambana mpaka SIKU yangu ya mwsho
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nipo tayari kulipa gharama za asili kwani dunia imenipa tu hifadhi na siidai chochote.
Asante kocha
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Utatutizi wa changamoto moja ni uzao wa changamoto nyingine huo ni ukweli kabisa yena ngumu kuliko uliochagua
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ahsante sana kocha, nilichojifunza hapa utatuzi wa changamoto moja ni uzao wa changamoto nyingine.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Malalamiko yeyote unayokuwa nayo hayamwathiri mtu mwengine isipokua wewe
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Malalamiko yote niliyonayo yananiadhiri Mimi mwenyewe
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Changamoto ni sehemu ya maisha yetu tusikate changamoto maana ndio ukuaji wenyewe kataa changamoto kataa ukuaji
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Changamoto ni sehemu ya maisha yetu tusikate changamoto maana ndio ukuaji wenyewe kataa changamoto kataa ukuaji
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
-Dunia inakwenda kwa kanuni zake.
-hakuna kitu Cha bule hapa duniani
-malalamiko yeyote unayokuwa nayo hayamuathili mtu
Mwingine yeyote ispokua ni wewe mwenyewe.
Hivyo ninapaswa kuukubali ukweli kwamba
Kulipa gharama hakukwepeki
Asante Sana kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kila kitu kwenye maisha kina gharama yake. Kuishi tu ni kodi, tunaalikwa kuwa tayari kulipa kodi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,changamoto hatuwezi kuzikwepa na maisha ni gharama lazima uzigaramikie.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kufanya biashara kuna manufaa na gharama zake.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Unaweza kuchagua kuzilipa na kukua zaidi.
Au ukazilalamikia na ukabaki pale ulipo. Asante Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
utatuzi wa changamoto moja ni uzao wa changamoto nyingine
LikeLike
Hivyo ndivyo ilivyo.
LikeLike
NIMECHAGUA KULIPA GHARAMA KUBWA ILINIFANIKIWE
LikeLike
Vizuri
LikeLike