3131; Subiri.
Rafiki yangu mpendwa,
Kadiri ninavyojifunza, kufuatilia na kuishi maisha ya kujenga mafanikio makubwa, ndivyo ninavyozidi kuona jinsi ambavyo kushindwa kwa walio wengi kunatokana na kukosa subira.
Kabla sijaendelea kutetea hilo na kukushawishi uwe na subira zaidi, tuangalie mfano wa asili kabisa kwenye hilo.
Ili mti uote, unahitaji vitu vinne; ardhi yenye rutuba, maji, hewa ya oksijeni na mwanga wa jua.
Mimea huwa inatumia mwanga wa jua kuzalisha chakula chake yenyewe, hivyo basi, mwanga huo wa jua huwa ni hitaji muhimu zaidi kwenye ukuaji.
Sasa basi, hapo ndipo penye mtego mkali sana. Miti inayopata mwanga mwingi wakati wa uchanga, huwa inakua kwa haraka sana, lakini mazao yake huwa ni dhaifu. Kwa mfano mbao itakayotokana na miti iliyokua kwa haraka huwa siyo imara, zinaliwa kwa urahisi na wadudu na haziwezi kutengeneza kitu chochote imara.
Miti inayoota chini ya kivuli cha miti mingine mikubwa, huwa haipati mwanga mwingi, hivyo uzalishaji wake wa chakula hauwi mkubwa na hilo kupelekea ukuaji wake kuwa wa tararibu sana. Lakini mazao yake huwa imara sana. Mbao inayotokana na miti ya aina hii huwa imara, haiharibiwi kirahisi na wadudu na inatengeneza vitu imara.
Hapo asili inatupa somo kubwa sana kuhusu kusubiri.
Chochote kinachokua haraka, huwa pia kinaharibika haraka.
Na kwa kuwa kanuni za asili huwa zinafanya kazi kila eneo bila kushindwa, hivyo ndivyo pia inavyokuwa kwenye safari ya mafanikio.
Mafanikio yoyote yanayopatikana kwa haraka, huwa yanapotea kwa haraka pia.
Na hilo lina ushahidi mwingi ambao ni wa wazi kabisa, kwa wale waliopata mafanikio ya haraka na kuishia kwenye anguko kubwa.
Kuna vitu viwili vikubwa ninavyotaka tuondoke navyo hapa na kwenda kuvifanyia kazi kwenye safari yetu ya mafanikio.
Moja ni pale unapokuwa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka, lakini hupati matokeo iliyokuwa unategemea kupata, kuwa na subira.
Mara nyingi sana watu huwa wanakimbilia kufanya vitu vya tofauti kabla hawajaweka muda wa kutosha kwenye vile walivyoanza navyo.
Pamoja na juhudi kubwa unazoweza kuweka, kuna vitu inabidi uvipe muda ndiyo viweze kukupa matokeo unayotaka.
Sehemu kubwa sana ya safari ya kujenga mafanikio makubwa ni kuwa na subira.
Na wengi wanaoshindwa siyo kwa sababu hawajui wanachotaka, au hawajui nini wanapaswa kufanya, bali wanakuwa wamekosa subira.
Mbili ni kuna wakati unahitaji kukataa fursa nzuri za ukuaji wa kasi kwa sababu unakuwa hujajenga misingi imara ya kuhimili ukuaji huo.
Hili ni gumu sana kuelewa na kukubali, lakini lina nguvu kubwa sana.
Ndiyo, unajifunza na kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo makubwa.
Halafu unakutana na fursa kubwa ya kukupa matokeo makubwa na kwa haraka, ila kwa uwezo wako wa sasa, huwezi kuhimili fursa hiyo.
Wengi hukimbilia kukubali fursa hiyo na kupata mafanikio ya haraka ambayo yanaleta anguko kubwa.
Kwa walio wengi wanaona kusema hapana kwenye fursa ni kuikosa milele. Ambacho hawajui ni kwamba kusema hapana kwenye fursa fulani, kunakujenga kuweza kunufaika na fursa kubwa zaidi.
Pale unapokutana na fursa nzuri lakini ni kubwa kuliko uwezo wako wa kuihimili, epuka tamaa ya kuipokea kwa sababu unataka ukuaji wa haraka.
Badala yake jijengee kwanza uwezo wa kuhimili fursa kubwa ili uweze kuzitumia kwa manufaa.
Ukishafanya kilicho sahihi, kinachofuata ni wewe kusubiri.
Endelea kufanya kilicho sahihi na endelea kusubiri.
Endelea kujifunza na kuwa bora na endelea kusubiri.
Endelea kufanya kwa ubora zaidi na endelea kusubiri.
Rudia kufanya hayo yote kwa msimamo bila kuacha na endelea kusubiri.
Kwa mwenendo huo, utajenga msingi imara sana ambao unaweza kuhimili kiwango chochote cha mafanikio utakachokipata.
Inahitaji uwe na msimamo mkubwa kuwa na subira kwenye zama hizi ambazo kila mtu anaonekana kufanikiwa haraka kuliko wewe.
Lakini pia ukiangalia jinsi wengi wanavyoanguka na kupotea, unazidi kuona jinsi subira ilivyo muhimu kwenye hii safari.
Fanya yaliyo sahihi na kuwa na subira. Hapo ndipo penye nguvu kubwa mno ya kukupa mafanikio yoyote unayoyataka.
##NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha Kwa ujumbe huu wa Leo
Nikweli subira ni Kila kitu kwenye mafanikio.
Ni kweli asili Huwa inatufundisha sana kuhusu kuwa na subira .huwezi kupanda mti Leo na kesho ukabeba msumeno kutaka kuupasua mbao.
Ni juzi juzi tuu kupitia huku kujitangaza kwenye mitandao nilipigiwa simu na mtu akinipa fursa kubwa ya ujenzi wa nyumba 30 Dodoma. Kigezo niwe na kampuni inayojiendasha na yenye vifaa. Ni kweli ningeweza kufosi Ili kuipata Kazi hiyo Kwa ujanja ujanja lakini nafikiri ingeweza kuwa na matokeo mabaya kwangu, hasa maswala ya mtaji na uendeshaji.
LikeLike
Vizuri na asante kwa kushirikisha hili. Kweli kabisa, ukubwa huo wa kazi kwa ngazi uliyopo ungekutikisa sana na kuharibu kuliko kujenga mafanikio yako.
Lakini hilo likupe msukumo wa kuwa na maandalizi makubwa ili baadaye uwe na uwezo wa kupokea fursa za aina hiyo. Maana kuweza kuzipata sasa ni kiashiria kwamba zinapatikana na zinaweza kuja kwako pia.
LikeLike
Nitafanya yaliyo sahihi na kuwa na subira. Kila kitu kinahitaji subira kwenye maisha yetu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Mafanikio yoyote yanayopatikana kwa haraka huwa yanapotea kwa haraka pia.
Subira ni sifa muhimu ya kuyaendea mafanikio makubwa na yatakayodumu.
Niliona hata Robert Greene anawakosoa vijana wanaotafuta mafanikio ya haraka kwa ajili ya “show off” lakini kwa gharama ya kujiingiza kwenye matatizo makubwa kwa kushindwa kujenga msingi.
Anasema ujanja sio kuwa na mafanikio ya haraka bali ujanja ni kuwa na mafanikio yanayodumu.
LikeLike
Ujanja ni kuwa na mafanikio yanayodumu 📌📌
LikeLike
Nimechagua kufanya kwa usahihi na kuwa na subira ili kupata mafanikio makubwa,na sitakimbilia fursa kubwa kwa kutaka mafanikio ya haraka bali nakuwa mvumilivu ili kujifunza na kuwa bora ili pale fursa kubwa inapotokea niwe nina uwezo wa kuendana na fursa hiyo na kuifanya kwa usahihi ili iniwezeshe kukuwa zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Tufanye kwa taratibu na kukua kwa taratibu tusikimbilie fursa ambayo ni kubwa kuliko uwezp wetu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Sana Kocha kwa SoMo hili la Subira. Nitakuwa na Subira kwenye maisha yangu. Nitafata utaratibu na kuacha kukurupuka na fursa za mhemko.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika kocha Makirita
SUBIRA inatuepesha na mambo mengi mabaya kwenye mafanikio yetu hasa zile fursa za kitapeli ambazo huwa zinakuja kwa haraka na kutunyima muda wa kufikiria kwa kina.
Ila kukipatikana SUBIRA utapeli hubainika.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Mara zote mafanikio ya haraka ambayo hayajajengwa katika misingi sahihi huishia kuwa anguko kubwa kwa walio wengi. Ili tujenge mafanikio ya muda mrefu tunapaswa kuwa na subira kwenye kila hatua tunazochukua.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha: nitafanya yaliyo sahihi na kuwa na Subira,
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Subira ni kitu muhimu kwa wakati huu tulip nao
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli kabisa subira ni muhimu sana kwangu. Kila kitu kina kanuni Zake za ukuwaji. Makala hii ya Leo imenikumbusha kuweka juhudi na kusimamia mchakato huku nikiaubiri Kwa imani kupiga hatua.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, subira subira subira! Nitakuwa na subira na siyo kukimbilia fursa ambazo zinaonekana ni za kufanikiwa haraka zaidi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana, Subira nikitu muhimu sana maishani nimejifunza kuwa na subira kwa kila jambo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo hili la subira. Ni kweli kabisa kuwa subira yavuta heri. Kuna mteja wangu mmoja tarajiwa huwa namfuatilia kila mara na kwa muda mrefu bila mafanikio lakini jana amekubali kuja kununua katika biashara yetu. Nitaendelea kufanya yaliyo sahihi na kuwa na subira daima.
LikeLike
Hongera sana.
LikeLike
Asante sana kocha nitakuwa na subira hata wengine waonekane kufanikiwa haraka kuliko mimi nitawaacha wafanikiwe cha msingi ni mimi kufanya yaliyo sahihi nakuwa na subira
LikeLike
Vizuri
LikeLike
👉Kufanya kilicho sahihi na endelae kusubiri.
👉Kujifunza na kuwa bora na endelae kusubiri
👉Kufanya kwa ubora zaidi na endelae kusubiri
Mambo matatu muhimu nayafanyia kazi ili kutimiza kusudi labkuwepo duniani.
Asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Asante kocha nitakuwa na subira hata kama wengine wataonekana kufanikiwa haraka kuliko mimi nitawaacha wafanikiwe cha msingi ni mimi kufanya yaliyo sahihi nakuwa na subira
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Subira yavuta heri, tuwe na subira katika kupata mafanikio makubwa tuendelea kuwekeza ndani yetu bila kuangalia tunchopata
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwenye swala la subira nafikiri kuna mtego mkubwa sana, usipokuwa na subira na focus unapata usumbufu mkubwa sana na kwa Dunia ya sasa kila dakika na kila sekrnde kuna kutu kinawezakukufikia, lengo ni ubobezi na ubobezi unaletwa na kufanya kwa msimamo na kufanya kwa msimammo ni kukubali kuwa kuna mambo mengine mengi yatakayo kupita.
amua unacho taka kufanya na kukifanya kwa ubora kila siku na kwa muda mrefu mpaka pale uatakapoweza kukifanya kwa ubora wa hali ya juu.
LikeLike
Hapo ndipo neno HAPANA linapokuwa na uhitaji mkubwa.
LikeLike
Nafanya yaliyo sahihi kwa subira
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaanya yaliyo sahihi ili niweze kuwa Na subra
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Fanya yaliyo sahihi na kuwa na subira.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya yaliyobora na kuwa na subila.a
LikeLike
Vizuri
LikeLike
_mafanikio yanayopatikana haraka pia hupotea haraka.
_unapokua kwenye mchakato sahihi kuwa na SUBIRA pia.
_ nitajenga msingi imara wa kuhimili ukuaji wa Kasi wa
mafanikio yangu.
Asante Sana kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitafanya yaliyosahihi na kuwa na subira ili kupata mafanikio makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
kuna wakati unahitaji kukataa fursa nzuri za ukuaji wa kasi kwa sababu unakuwa hujajenga misingi imara ya kuhimili ukuaji huo
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Subira ni jambo muhimu sana kwa wakati wote ana husaidia kuwa imara katika kile ambacho una kifanya
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kaa kwenye Mchakato sahihi Kisha kuwa na Subira ya kile unavyofanyia kazi.
Mchakato sahihi
Subira ya kutosha kupata matokeo
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
CHOCHOTE KINACHOKUA HARAKA HUWA KINAHARIBIKA HARAKA
LikeLike
Hakika
LikeLike