3149; Miaka 100.
Rafiki yangu mpendwa,
Nikiwa mkubwa, nataka kuwa kama Charlie Munger 🤗🤗
Sababu ni 5;
1. Ni bilionea.
Mimi; Nitakuwa bilionea.
2. Ana miaka 99 na anaendelea kufanya kazi.
Mimi; Nitaishi zaidi ya miaka 100 na nitafanya kazi maisha yangu yote.
3. Muda mwingi wa siku yake (asilimia 80) anautumia kusoma.
Mimi; Nasoma angalau kitabu kimoja kila siku.
4. Ni mwekezaji wa kununua na kushikilia badala ya kucheza na soko la hisa.
Mimi; Naendelea kuwa mwekezaji bora bila kuhangaika na soko.
5. Amekuwa rafiki wa karibu wa Warren Buffet tangu mwaka 1959 (miaka 64 sasa) na wamekuwa washirika wa kibiashara na uwekezaji tangu mwaka 1978 (miaka 45 sasa). Katika kipindi chote hicho wamepata mafanikio makubwa (kuwa mabilionea) na hawajawahi kugombana.
Mimi; nitaendelea kuwa rafiki yako na mshirika wako wa karibu kwenye hii safari ya ubilionea, lazima tutoboe pamoja.
Siri ya kuishi maisha marefu na yenye furaha.
Charlie Munger alikuwa anahojiwa na mwandishi wa habari ambaye alimwambia watu wengi wamekuwa wanatafuta siri ya kuishi maisha marefu na yenye furaha.
Kabla hata mwandishi huyo hajamaliza kuuliza swali, Munger alimkatisha akisema hiyo ni rahisi.
Alieleza kwamba amekuwa akifuata sheria hizi sita;
1. Usiwe na wivu.
2. Usiwe na chuki.
3. Usitumie zaidi ya kipato chako.
4. Kuwa mchangamfu (mwenye shauku) hata kama una matatizo.
5. Jihusishe na watu wa kuaminika.
6. Fanya yale unayopaswa kufanya.
Munger anasisitiza kwamba ni vitu vya kawaida kabisa, ila vyenye nguvu kubwa sana.
Ahadi yangu kwenye kutekeleza sheria hizo za kuishi maisha marefu na yenye furaha na mafanikio makubwa;
1. Sitakuwa na wivu kwa mtu yeyote yule. Ninapoona wengine waliopata mafanikio makubwa nitawafurahia na kujifunza kutoka kwao ili na mimi nizidi kufanikiwa.
2. Sitakuwa na chuki kwa mtu yeyote yule. Kama naona mtu hana manufaa kwangu nitamwondoa kwenye maisha yangu. Sitakuwa na muda wa kujenga chuki naye. Na yeyote anayeamua kunichukia kwa sababu yoyote ile, hayo ni matatizo yake binafsi.
3. Sitatumia zaidi ya kipato changu. Hii ndiyo sheria ya kwanza ya mafanikio niliyojifunza, jilipe wewe mwenyewe kwanza. Na sijawahi kuivunja tangu nimejifunza. Imekuwa na manufaa makubwa sana kwangu. Nitaendelea kuizingatia daima.
4. Mara zote nitakuwa mchangamfu (mwenye shauku) hata kama kuna matatizo ninayoyapitia. Sitaruhusu mtu yeyote aone nimevurugwa na kitu chochote kile. Nitavaa uso wa tabasamu mara zote na kuwa na shauku kubwa ya kuyakabili maisha.
5. Nitajihusisha na watu wa kuaminika tu. Nitashirikiana na wale wanaothamini ninachofanya na wanaotekeleza kila wanachoahidi. Wale wanaofanya kile wanachosema watafanya. Na wanakifanya kwa viwango vya juu na kwa msimamo mara zote.
Mtu yeyote anayenipa sababu ya kutokumwamini, nitamwondoa kabisa kwenye maisha yangu.
6. Nitafanya yale ninayopaswa kufanya. Nitatimiza kila ninachoahidi, kwa viwango vikubwa na kwa msimamo. Nitaweka kipaumbele na juhudi kubwa kwenye yale niliyochagua kufanya. Nitayapenda sana na mara zote kwenda hatua ya ziada ili kutoa thamani kubwa zaidi. Nitahakikisha nawapa watu vitu ambavyo hawawezi kuvipata kwa mwingine yeyote ila mimi tu. Nitawafanya watu wanitegemee kwa uhakika kwenye maeneo niliyochagua kufanyia kazi, ambayo ni kusoma, kuandika na kufundisha.
Rafiki, hayo ndiyo mambo sita nitakayohakikisha kwa asilimia 100 nayaishi kila siku bila kuruhusu sababu yoyote kunikwamisha.
Na nina uhakika, bila ya shaka yoyote nitafikia sifa tano ambazo Charlie Munger ameweza kuzifikia kama nilivyoshirikisha hapo juu.
Na Munger hatuachi hivi hivi, bali anatupa ahadi hii;
“Hakikisha kila siku unayoimaliza unakuwa na hekima zaidi ya ulivyokuwa wakati unaamka. Kama utafanya hivyo kila siku bila kuacha na ukaishi maisha marefu, utapata kile unachostahili.” – Charlie Munger.
Kwa nukuu hiyo kuna vitu vitatu vya kuzingatia ili kupata kile unachotaka kwenye maisha;
1. Jifunze kila siku.
2. Weka kwenye matendo yale unayojifunza. (Ndiyo tofauti ya maarifa na hekima.)
3. Usife mapema, yaani hakikisha unaishi maisha marefu zaidi.
Hayo yote yapo ndani ya uwezo wetu, tuyatekeleze.
Rafiki yangu mpendwa, kwenye maoni hapo chini weka ahadi yako ya kuziishi sheria sita za Charlie Munger na jinsi unavyokwenda kuziishi kila siku.
Hilo ni zoezi muhimu kwa kila mmoja wetu kulifanya.
Lifanye sasa, shirikisha na liishi kila siku ya maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitahakikisha Kila siku ninayoimaliza Nakuwa na hekima kuliko nilivyoamka asubuhi.
Nitaendelea kutumia muda wangu kusoma zaidi. Na kuandika.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitakuwa mwaminifu na mwangalifu mara zote kama alivyosema Bilionea Charlie Munger.
Nakata kuishi miaka zaidi ya 100 kama yeye.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitaanza kuziishi sheria hizo sita ili kupata mafanikio katika maisha yangu. Nitajakikisha kila siku inayokwisha nakuwa na hekima zaidi ya vile nilivoamka asubuhi. Nitasoma na kufanyia kazi yale ninayoyapata
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahadi yangu katika kutekeleza sheria hizi sita
1.sitakuwa na wivu na yeyote
-nimechagua kuwapongeza wale walionizidi kwenye maisha yangu na sitakuwa na wivu kwao zaidi ya kujigunza yale mazuei kutoka kwao ili namimi niweze kufanikiwa pia
2.sitakuwa na chuki na mtu yeyote
Kama naona mtu ni mzigo na hana manufaa kwangu sitamchukia bali nitamuondoa kwenye maisha yangu na wala sitagombana nae ili asiwe kikwazo kwenye maisha yangu kwa namna yoyote ile
3.sitatumia zaidi ya kipato changu
Tangia nijifunze kutoka katika kitabu cha elimu ya msingi ya fedha mwaka 2020 nilijifunza njia za kugawa kipato changu kwenye mafungu matano na tangia hapo nimekua naiishi hii nidhamu bila kuacha na nitaendelea hivyo maisha yangu yote na nimeweza kujidhibiti sana kwenye matumizi yangu kwa kujilipa na kuwekeza
4.Mara zote nitakuwa mchangamfu
Shauku inaambukizwa ili niweze kukamilisha makubwa kwenye maisha yangu nimechagua kuwa mchangamfu mara zote hata kama nina shida zangu binafsi sitaruhusu hilo liniondolee uchangamfu na nitakua ivo kwa kila mtu nitakaekutana nae kwa maisha yangu yote
5.Najihusisha na watu wa kuaminika tu
Nikishagundua mtu s mwaminifu nitakaa na e mbali
6.Nitafanya yale niliyopaswa kufanya
Nikishapanga mambo ya kufanya nitayatekeleza hayo bila kuruhusu sababu yoyote ile mana kama ni jambo la msingi bas nitatafuta sababu ya kulifanya na si vinginevyo nje hapo ni umbea na nitatekeleza hili kwa maisha yangu yote.
Asante sana kocha
LikeLike
Hongera sana kwa ahadi hii, itimize kwa ukamilifu.
LikeLike
Jambo la msingi ni kuyaishi maisha haya na kuhakikisha haufi mapema kibiashata
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ntajitahidi kuzingatia yote kwenye makala hii ili kuwa na maisha marefu zaidi..
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Asante kocha ahadi yangu ni nitajifunza kila siku na kuyaweka kwenye matendo yale ninayojifunza nitahakikisha naishi muda mrefu na sitakuwa na wivu AO chuki na MTU yeyote pia nitakuwa mchangamfu nakujihusisha na watu waaminifu tuu nitafanya yale ninayopaswa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kufanya na sita tumia zaidi ya kipato changu
LikeLike
Asante sana Kocha,
Ninaamini kuwa hekima ni mkusanyiko wa maarifa na taarifa sahihi na pale unapoyatumia haya kwa busara katika kuyafikia mafanikio.
Daima nitajifunza na kuyafanyia kazi ninayojifunza kwa bidii na kwa msimamo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii nzuri. Sheria namba 1 hadi 3 nilishaanza kuziishi na hapa nahidi kuziishi zote sita kama zilivyo.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Sana Kocha. Na Mimi nikiwa mkubwa nataka kuwa kama Charlie Munga. Sitakuwa na chuki na sitajihusisha na Wala sitavunja mambo SITA aliyosema Charlie
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nitaepuka kuwa na wivu. Hili nimekuwa nikilifanyia kazi muda mrefu na limenisaidia.
Nitaepuka chuki na visasi. Kwa kujiepusha na kupuuza watu wanaoleta uhasama.
Nitaendelea kuwa na maisha rahisi na kuepuka sifa na majivuno ili nisijiingize kwenye matumizi makubwa nje ya kipato.
Nitaendelea kuboresha uchangamfu na shauku nyakati zote bila kujali nini kinaendelea na hasa kwa kuepuka hofu na mawazo hasi.
Nitaendelea kuwaondoa watu wasio waaminifu kwenye maisha, na tayari nimeshawaondoa wengi hivi karibuni, zoezi hili ni endelevu.
Nitajitahidi zaidi mara zote kufanya yale ninayopaswa kufanya na hata kujisukuma zaidi.
Nitazingatia hayo niweze kuishi maisha marefu na kutimiza ndoto kubwa sana nilizonazo.
LikeLike
Safi sana, kaa humo na utaishangaza dunia.
LikeLike
Hakika kuna mengi sana juu ya charlie Munger kujifunza na kuishi kama yeye.
Nitafanyia kazi na kuishi kama Munger alivyoshauri.Ni maisha mazuri na ya furaha kuishi kwa ushauri huu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mtu yeyote atakaenipa sababu ya kutokumuamini, nitahakikisha namuondoa kwenye maisha yangu
Naishi chini ya kipato changu
Sina wivu mtu
Nitakuwa mchangamfu katika hali zote
Nakaa kwenye mchakato kamili
LikeLike
Safi sana, simamia hayo.
LikeLike
Mimi ni billionea, na kila billionea ana maisha yanayo shahibiana na mabilionea mengine, maisha yangu yana shabihiana na maisha ya Bilionea Charlie Munger na nitayaishi haya, maisha yangu yote maana haya ndio maisha ynagu.
LikeLike
Safi sana, umenena na imekuwa.
LikeLike
Nitajifunza kila siku
Nitaweka kwenye Matendo ninachojifunza
Sitaki kufa mapema
4.Sitatumia zaidi ya kipato ninachopata
Sitamwonea wivu mtu yoyote
Sitakuwa na chuki na yeyote
Nitaendelea kuwekeza kidogo kidogo kwa msimamo na kwa muda mrefu bila kuacha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante hizi sheria zote ambazo munger amekuwa anaziishi nimekuwa na ziishi bila kujua kama zinafanya kazi au la ….lakini kupitia kauli ya munger na kuzitaja kama zinaleta matokeo makubwa ukiziishi sasa nitatia mkazo kuziishi kwenye maisha yangu yote hasa hii ya wivu na chuki
Asante sana
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Naahidi kuyashika mambo hayo Sita kama yalivyo bila kuacha chochote ili kufikia mafanikio makubwa na kusihi maisha marefu.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Ahadi yangu ya kuziishi sheri za Charlie Munger ni kutekeleza yale ninayopaswa kufanya kwa uaminifu mkubwa pasipo kujidanganya. Makala hii inatafakarisha sana.
Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
1.Sitakuwa mvivu,Nitafanya kila nalotakiwa kufanya kwa ukubwa
2.Sitakuwa na chuki na yoyote kwa kuwa na chuki ni kuamua kujichosha mwenyewe
3.Sitatumia zaidi ya kipato changu.
4.Nitakuwa mchangamfu na mwenye shauku bila kujali changamoto ninazopitia kwa wakati huo.
5.Nitajihusisha na watu wa kuaminika pekee
6.Nitafanya yale ninayopaswa kufanya tu ili kuokoa muda na kuongeza tija.
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
AHADI ZANGU SITA AMBAZO NINAKWENDA KUZIISHI NI
1. sintakuwa na wivu kwa mtu yeyote yule.
2. Sinta kuwa na chuki na mtu yeyote
3. Sintatumia zaidi ya kipato changu
5. Nitajifunza kila siku.
6. Nitaweka ktk matendo yote ninayojifunza
Asante Sana kocha kwa miongozo hii Bora kabisa.
LikeLike
Vizuri, zingatia.
LikeLike
Asante kocha,Ninahaidi nitazitekeleza sheria zote ambazo zimeandikwa kwenye hii makara ili nisife mapema.na nitazifanyia kazi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahadi zangu ninhizi
1. Nimeachana wivu kabisa.
2. Nitaiepuka chuki daima.
3. Nitaunguza matumizi na sintatumia zaidi ya kipato changu
4. Nitakuwa mchangamfu (mwenye shauku) hata kama nina changamoto.
5. Nitajitahidi kujihuzisha na watu walio Chanya tu.
6. Nitafanya Yale natakiwa kufanya hasa Yale ya msingi yanayogusa maisha yangu
15Aug2023
LikeLike
Safi sana.
Kaa humo.
LikeLike
Sitatumia zaidi ya kipato changu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahadi yangu kwenye kutekeleza sheria hizo za kuishi maisha marefu na yenye furaha na mafanikio makubwa;
1]Sitakuwa na wivu,ninapoona wengine wamefanikiwa,nitafurahia mafanikio yao,na kujifunza kupitia mafanikio yao kuwa inawezekana.
2 ] nitaepuka kutengeneza chuki na wengine,yeyote mwenye chuki na mimi hiyo inabaki kuwa mizigo yake.
3] Kujilipa mwenyewe kabla ya wengine imekuwa na manufaa makubwa sana kwangu,hii kwangu ni kama sala.
4] matatizo,changamoto ni sehemu ya maisha,sina haja ya kuwa mnyonge ninapopitia hali hizo zaidi ya kufurahia mchakato.
5] Kwanza nitawaamini watu,lakini pale watakaponipa sababu ya kutokuaminika nitawapotezea.
6] Nitafanya yale ninayoona ni sahihi kwangu kufanya,na kama kitu siyo kweli,sitasema.
Nitawafanya watu wanitegemee kwa uhakika kwenye maeneo niliyochagua kufanyia kazi,ambayo ni Biashara na Uwekezaji
LikeLike
Vizuri sana.
Zingatia.
LikeLike
Asante sana kocha,hayo mambo sita nitayaandika na kuwa sehemu ya muongozo wangu binafs.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike