3152; Umajinuni na ulazima.
Rafiki yangu mpendwa,
Wakati nipo shule ya udaktari, kwenye kitengo cha magonjwa ya akili tulijifunza magonjwa mengi na sifa zake.
Tulikuwa na tabia ya kutaniana ukiambiwa lazima upate ugonjwa mmoja wa akili mtu utachagua upo?
Magonjwa ya akili yapo mengi kitabibu. Lakini kimazoea watu mpaka waone mtu anaokota makopo ndiyo wanasema ana ugonjwa wa akili, au kama wanavyoita kichaa.
Magonjwa mengi ya akili huwa hayaonekani kwa nje, bali huwa yapo ndani ya mtu. Mtu anakuwa na ugonjwa wa akili pale anaposhindwa kudhibiti akili yake mwenyewe.
Moja ya magonjwa ya akili ambayo huwa siyo rahisi kuonekana kwa nje, hasa kwenye hatua za awali ni magonjwa yanahohusisha hisia (mood)
Na hayo huwa yana pande mbili (bipolar).
Upande mmoja ni hisia za huzuni sana ambazo zinapelekea ugonjwa wa sonona (depression).
Na upande wa pili ni hisia za furaha sana ambazo zinapelekea ugonjwa wa mtu kuwa na msukumo wa kufanya zaidi (mania).
Sasa basi, tukirudi kwenye utani wa hapo juu, nilikuwa nasema kama nitaambiwa lazima niwe na ugonjwa mmoja wa akili, basi nitachagua huo wa mania.
Kwani watu wenye ugonjwa huo huwa wanakuwa na mawazo mengi, wanafanya mambo mengi na hawazuiliki.
Japo kuna hatua inafika huo msukumo unakuwa na madhara kwao, mfano kukosa usingizi na hatimaye kurudi kwenye upande wa pili wa sonona.
Nilichoendelea kujifunza ni kwamba watu wengi waliopata mafanikio makubwa, huwa wana kiwango kidogo cha hayo magonjwa ya akili, hasa huo wa mania.
Kwa jinsi mafanikio makubwa yalivyo magumu, mtu mwenye akili timamu hawezi kuhangaika nayo, au hata kuyavumilia.
Kabla hatujaendelea nikuhakikishie hapa kuna namna sisi tuliopo hapa akili zetu hazipo sawa kwa vipimo vya watu wa kawaida.
Kama akili zetu zingekuwa zinafikiri kama wengi wanavyofikiri, tusingejitesa kwa namna hii.
Kuna namna tuna ukichaa mdogo na hilo ni sawa kabisa.
Hivyo pale wengine wanaposikia mipango yako na kuangalia hatua unazochukua na kukuambia umechanganyikiwa, unaweza kuwajibu wamechelewa sana kung’amua hilo.
Hapa kuna ugonjwa mwingine wa akili ambao ninataka ujitengenezee na kuudhibiti ili uweze kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Ugonjwa huo unaitwa Obsessive and Compulsive Disorder (OCD).
Ugonjwa huo una dalili za mtu kuwa na mapenzi makali juu ya kitu (Obsession) au umajinuni na msukumo wa kuchukua hatua pale kitu hakijakaa sawa (Compulsion) au ulazima.
Nikupe mfano ili tuelewane vizuri. Kila mtu anamjua mtu ambaye anaweza kufunga mlango na kutoka, kisha akafika njiani na kujiuliza kama amefunga au la. Anashindwa kuendelea na safari yake mpaka arudi kuhakikisha amefunga mlango. Hiyo ni ngazi ya chini ya ulazima (Compulsion), unakuwa ugonjw ambaya pale mtu anapotoka na bado akarudi tena kuhakikisha kama amefunga, hata baada ya kuhakikisha, bado atarudi tena. Yaani mtu anaweza kushindwa kuendelea na kitu kingine kwa sababu ya hilo.
Mfano wa pili ni mtu anayekuwa amepanga vitu vyake kwa namna fulani, ukienda kubadilisha anakasirika na kurudisha kama alivyokuwa amepanga. Yaani hata ukisogeza kitu kidogo tu, hatakaa sawa mpaka amerudisha kama ilivyokuwa. Hivyo ndivyo umajinuni (Obsession) inavyokuwa.
Umajinuni (Obsession) ni kuwa na mapenzi makubwa sana juu ya kitu kiasi kwamba huwezi kujizuia katika kukifanya. Unakuwa kama umeingiwa na pepo juu ya kitu hicho. Unaweza kukifuatilia na kukifanya kwa muda mrefu bila kuchoka.
Unaweza hata kusahau kula pale unapokuwa unafanya kitu hicho.
Hakuna starehe yoyote inayoweza kukuondoa kwenye kufanya kitu hicho.
Ulazima (Compulsion) ni msukumo wa kuchukua hatua juu ya kitu kwa wakati huo huo bila kusubiri. Ulazima ndiyo unaokusukuma kuchukua hatua haraka kwenye mambo muhimu bila kuahirisha.
Unapokuwa na ulazima kwenye kitu, huwezi kabisa kuahirisha. Hupati utulivu ndani yako mpaka umekamilisha kufanya.
Sehemu ambayo nataka wote tuwe na huu ugonjwa ni kwenye mchakato wa Bilionea Mafunzoni.
Nataka tuwe na umajinuni (Obsession) kwenye huu mchakato. Tuupende na kuukubali sana kuliko kitu kingine chochote. Uwe kipaumbele cha kwanza kwetu na kusiwe na kitu au mtu yeyote anayeweza kututoa kwenye mchakato huu.
Kisha tuwe na ulazima (Compulsion) kwenye kuchukua hatua za mchakato huu wa Bilionea Mafunzoni. Tusukumwe sana kuchukua hatua kiasi cha kukosa kabisa utulivu kama hatujachukua hatua. Isiwe rahisi kwetu kuahirisha kuchukua hatua ambazo tumepanga.
Hata pale tunapokutana na changamoto na vikwazo mbalimbali, bado hatukubali kuacha kutekeleza mchakato wetu. Kwa sababu msukumo ulio ndani yetu hauwezi kutulizwa na chochote.
Umajinuni (Obsession) na Ulazima (Compulsion) ni vitu viwili ambavyo ukiwa navyo unakuwa mtu hatari sana kuweza kujenga mafanikio makubwa ambayo wengi hawawezi hata kuyaota.
Wengi wanachukulia hayo mawili kama ugonjwa kwa sababu wanashindwa kuyadhibiti. Lakini wewe ukiweza kuyadhibiti, yatakuwa baraka kubwa sana kwako.
Kuwa na mapenzi makubwa (Obsession) juu ya kitu kiasi cha kukifikiria muda wote na kuwa na msukumo (Compulsion) wa kufanya kitu hicho bila kukubali kuahirisha kwa namna yoyote ile. Hivyo ndivyo unavyoweza kujenga mafanikio yoyote makubwa unayotaka kuwa nayo kwenye maisha yako.
Na kama watu watakuambia umechanganyikiwa, wacheke, kwa sababu hakuna mwenye akili timamu aliyeweza kufanya mambo makubwa hapa duniani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Umajinuni na ulazima.
Kweli, hakuna mwenye akili timamu aliyewahi kufanya makubwa hapa duniani.
Kweli, wakati mwingine watu huhisi wewe ni kichaa lakini mara nyingi hawakwambii kwa sababu wanaogopa utawashutumu wanakutukana.
LikeLike
Ni kitu cha kufikirisha
LikeLike
Hiyo ndiyo hali halisi.
Tuitumie vyema kufanya makubwa sana.
LikeLike
Hakika kocha mafanikio makubwa hayatokani na akili timamu. Kuna kipindi nilikuwa nawaambia watu kuwa hata viongozi wa kisiasa ni vichaa. Maana Kwa akili timamu ni vigumu kuongoza watu. Ninachokijua watu wenye akili timamu hujificha linapokuja swala la kufanya jambo kubwa.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli, huwezi kuwa na akili timamu ukajitesa.
LikeLike
Nakuwa na mapenzi makubwa juu ya biashara niliyochagua kuifanya kwa kuifanya kwa muda wote na kwa msukumo mkubwa bila kukubali kuahirisha kwa namna yoyote ile na ninakaa kwenye mchakato hadi nitakapokabidhiwa ushindi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Binafsi naona mchakato unaingia damuni.Inapotokea nimeshindwa kutekeleza kitu ki ukweli najikuta naumia.Nafurahia mchakato.
LikeLike
Safi sana,
Kaa humo.
LikeLike
Ni kweli hakuna mwenye akili timamu anayeweza fanya makubwa hapa duniani. Nimesoma hapa nikakumbuka Elon musk siku moja nilikuwa namsikiliza akielezea artificial intelligence robot Zake nikaona kweli anaweza kuwa Hana akili timamu. Pale anapo kiss na robot.
Na sisi kweli tujisukume zaidi kiasi cha kutokuwa na akili timamu ili tufanye zaidi na kuona ni ya lazima
LikeLike
Hakika, mfano uliotoa ni dhahiri kabisa.
LikeLike
Nitakua na mapenzi makubwa na mchakato bila kuzuiwa na mtu yeyote
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mapenzi yangu makubwa nitayaweka kwenye mchakato, na kupitia mchakato huu, nitaweza kupata chochote ninachotaka. Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Kumbe namimi nina kakichaa kadogo 😂.nitakuwa na mapenzi makubwa na bm zamani nilikua naona mateso ila saiv nisipofanya siku yangu haiwi sawa.
Nitahakikisha nakuwa kwenye mchaksto mara zote.
LikeLike
Safi sana, hapo ngoma imeingia kwenye damu. Kaa humo.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, nitajisukuma na kuchukua hatua hadi nikose utulivu kama sijachukua hatua.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hakuna mtu mwenye akili timamu aliyeweza kufanya mambo Makubwa hapa duniani.
Nitakuwa mgonjwa wa Umajinuni na Ulazima.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni bora kuwa kichaa halafu unapata kila unachokitaka kuliko kuwa na akili timamu halafu unakosa hata mahitaji ya msingi kwa maisha yako.
LikeLike
Neno la msingi sana umeshirikisha hapa.
LikeLike
Nina mapenzi makubwa (Obsession) juu ya kitu kiasi cha kukifikiria muda wote na kuwa na msukumo (Compulsion) wa kufanya kitu hicho bila kukubali kuahirisha kwa namna yoyote ile.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Habari njema ni kwamba Nina ugonjwa wa wale wale wenye mafanikio makubwa:
Mapenzi makubwa
Umajinuna
Ulazima 💪🏾
LikeLike
Safi sana, utumie vyema.
LikeLike
Obsession and compulsion tukae hapo
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Umajinuni na ulazima daima ili kuyafikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nitaendelea kuwa na mapenzi makubwa bila kuhofia chochote.
LikeLike
Vizuri sanam
LikeLike
Hakuna mwenye akili timamu anaweza kufanya makubwa hapa duniani, natumia ukichaa kukaa kwenye mchakato bila kuyumba, ni lazima siwezi kuwa sawa bila kutimiza.
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Umajinuni na ulazima ndo mpango mzima wa kupambana na mafanikio kwangu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kuwa na mapenzi makubwa (Obsession) juu ya kitu kiasi cha kukifikiria muda wote na kuwa na msukumo (Compulsion) wa kufanya kitu hicho bila kukubali kuahirisha kwa namna yoyote ile. Hivyo ndivyo unavyoweza kujenga mafanikio yoyote makubwa unayotaka kuwa nayo kwenye maisha yako.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kufanya makubwa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuwa na mapenzi makubwa (Obsession) juu ya kitu kiasi cha kukifikiria muda wote na kuwa na msukumo (Compulsion) wa kufanya kitu hicho bila kukubali kuahirisha kwa namna yoyote ile. Hivyo ndivyo unavyoweza kujenga mafanikio yoyote makubwa unayotaka kuwa nayo kwenye maisha yako.
Hiyo ndiyo hatua ninayokwenda kuichukua kuanzia sasa.
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
UMAJINUNI ni kuwa na mapenzi makubwa sana juu ya kitu kiasi kwamba huwezi kujizuia katika kukifanya.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nina obsession katika upangaji wa vitu Sitaki mtu abadirishe vile nimepanga.
LikeLike
😂😂
Vizuri, sasa hamishia kwenye mchakato wa BM.
LikeLike
Ni kweli hakuna mwenye akili timamu aliyefanya makubwa Bali ni Walelioonekana kuwa vichaa ndio waliofanya makubwa.
Nitakaa kwenye Mchakato huu kama kichaa bila Shaka nitafanikiwa. Hapa tu nilipo wanaonifuatilia wanasema hawanielewi elewi.
LikeLike
😂😂 Ukiona unaeleweka jua umeshapotea.
LikeLike
Umajinuni (Obsession) na Ulazima (Compulsion) ni vitu viwili ambavyo ukiwa navyo unakuwa mtu hatari sana kuweza kujenga mafanikio makubwa ambayo wengi hawawezi hata kuyaota.Asante sana Kocha.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asanste sana Kocha,
Kama umajinuni na ulazima ni ugonjwa basi ni ugonjwa mzuri. Nitaujenga msukumu huu mkubwa kwa ajili ya kupiga hatua kubwa. Lakini kama ukawaida ni uzima basia utakuwa ni uzima wa kushindwa, na sihitaji kueleweka kwa sababu ni wa kawaida.
LikeLike
Vizuri sana, kila la kheri.
LikeLike