3165; Huruma
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna taratibu mbalimbali ambazo huwa tumejiwekea kwenye kushirikiana na watu wengine.
Kwa taratibu hizo, huwa tuna hatua za kuchukua pale mtu anapokwenda tofauti na anavyopaswa kwenda.
Kuna watu ambao wanakuwa wameenda tofauti kabisa na taratibu ambazo tumeweka.
Lakini inapokuja kwenye kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa, huruma inatuingia.
Tunawaonea watu hao huruma, na kuona tunalazimika kuwapa nafasi nyingine kwa sababu wataweza kufanya vizuri zaidi.
Kama utakuwa ni mdadisi, utakuwa umejionea wazi ya kwamba wale ambao hukufanya maamuzi juu yao kwa sababu ya huruma, ndiyo pia wamekuwa chanzo kikubwa cha changamoto kwako.
Watu hao ndiyo huwa wanayafanya maisha yako kuwa magumu na usiyoyafurahia.
Kwa kifupi watu ambao uliacha kufanya maamuzi kwa sababu ya kuwaonea huruma, ndiyo huwa wanakosa kabisa huruma kwako.
Kumbuka wateja ambao ulivunja utaratibu uliojiwekea kwenye biashara kwa sababu unawaonea huruma, ndiyo hao hao wanaishia kukutesa sana kwenye yale wanayofanya.
Huenda uliwapunguzia bei au hata kuwapa bure kwa huruma uliyokuwa nayo kwao.
Lakini baada ya wao kupata ulichowapa, wanaona wanastahili zaidi hivyo kuanza kukusumbua.
Hapo ndipo wanapokupa mateso makubwa sana ambayo hukuyategemea.
Kadhalika kwa wafanyakazi unaokuwa umewaajiri au watu wengine unaoshirikiana nao, wale ambao hawakidhi vigezo ila ukawaacha kwa sababu ya huruma ndiyo huja kukupa mateso makubwa.
Watu hao ambao wewe uliwaonea huruma, wao wanakosa huruma kabisa.
Unakuwa umewaonea huruma kwamba ukiwaacha hawana pa kwenda.
Lakini wao wanapopata upenyo kidogo tu, huwa wanautumia kikamilifu kuchukua hatua ambazo wewe ulipaswa kuchukua ila ukaingiwa na huruma.
Kwa kifupi, wale unaowaonea huruma ndiyo huwa wanakuwa katili sana kwako.
Ulitegemea wangekuwa wa kwanza kurudisha huruma uliyoonyesha kwao, lakini wanaishia kufanya ukatili ambao unakuumiza sana.
Japo wapo wanaokuwa wanafanya bila kujua, wengi wanakuwa wanajua kabisa kile wanachofanya.
Wanakuwa wanalipa chuki iliyojengeka kwako kwa sababu ya ile huruma unayokuwa umewapa.
Watu huwa hawapendi kujiona hawana nguvu dhidi ya wengine.
Watatumia hata kuwapa wengine hali ya hatia ili tu nao wajione wapo juu.
Na ndiyo maana wale unaokuwa umefanya maamuzi kwa huruma, ndiyo huja kufanya maamuzi yanayokuumiza sana.
Kitu kikubwa cha kuondoka nacho hapa ni kuhakikisha unafuata utaratibu uliojiwekea kwenye kila eneo la maisha yako.
Pale anapopatikana mtu ambaye hajafikia taratibu zilizopo, kamwe usimchague kwa sababu ya huruma.
Badala yake endelea kuwafikia wale watakaokuwa wanakidhi vigezo ulivyoviweka.
Watu sahihi wapo wengi sana.
Kama hujawapata siyo kwa sababu hawapo.
Bali ni kwa sababu hujatafuta vya kutosha.
Unapojaza nafasi na watu ambao hawakidhi vigezo, unajisahau kwenye kutafuta walio sahihi.
Na hao wasio sahihi siyo kwamba watatumia fursa uliyowapa kuhakikisha wanakidhi vigezo.
Badala yake wanakuwa wanatafuta fursa ya wao kukuumiza pia.
Unaweza kuona hayo yote hayajakaa sawa, lakini ndivyo dunia ilivyo, haipo ndani ya uwezo wako kupanga dunia iendeje.
Wewe jiwekee mchakato wako na ufuate mchakato huo mara zote bila kuacha kwa sababu za kihisia.
Maana mara zote pale hisia zinapokuwa juu, fikra huwa zinakuwa chini kabisa na maamuzi yanayofanyika yanakuwa siyo sahihi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
ahsante kocha.
huruma pekee ni kufuata utaratibu
LikeLike
Kabisa, kwenda nje ya utaratibu ni kutafuta shida.
LikeLike
Watu unaowaonea huruma na kujaribu kuwasaidia sio kwamba watatumia nafasi hiyo kujiboresha kuhakikisha wanakidhi vigezo bali, badala yake watakuwa wanatafuta fursa ya wao kukuumiza pia.
LikeLike
Kabisa yani, ni jambo la kushangaza, lakini ndivyo watu walivyo na hakuna tunachoweza kufanya zaidi ya kusisitiza utaratibu ufuatwe.
LikeLike
Ni kweli mara nyingi hao ndiyo wanakuja kuwa hawana tena huruma na wewe wanajiona wameshinda na kukusababishia wewe madhara mskubwa sana
LikeLike
Kabisa, tuwe na tahadhari kubwa.
LikeLike
Mara zote nitafuata mchakato wangu na si kuamua kwa huruma.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha hii naona kama inaongea kuhusu mimi Kwa kweli wasaidizi wangu huwa wananifanyia makosa lakini kwasababu ya huruma badala yakuwafukuza nawaoneaa uruma kumbe kesho tena wanarudilia makosa yaleyale wao hawanisikilii uruma kwa hiyo siongeze tena kumsikilia mutu huruma
LikeLike
Pole, huruma inatuumiza sana, ni vyema kuchukua hatua sahihi mapema.
LikeLike
Huruma hugeuka mateso baadae
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha, watu sahihi wapo, kikubwa ni kuachana na huluma na kufuata utaratibu niliojiwekea kwenye kila eneo la maisha yangu,kwa kweli hizi huruma zinatuponza na hasa naimani kwenye biashara zetu hazifai kabisa.
LikeLike
Ndiyo, kwenye biashara huruma ni hatari mno.
LikeLike
Nitafuata utaratibu wangu badala ya huruma.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Unapotaka kuchukua hatua kwa mtu ambaye analeta zengwe za kushindwa kutekeleza majukumu yake, hisia za huruma zinapaswa kuwekwa pembeni.
Asante sana Kocha
LikeLike
Kabisa, la sivyo hisia hizo zitakuvuruga vibaya.
LikeLike
Ahsante sana kocha, hii imeendana kabisa na maamuzi ambayo huwa nayafanya kwa watu hasa ambao wapo kwenye dozi wakati wameanza dozi inafika muda hawana hela lakini nikiwaambia walipoe kidogo nyingine watamalizia huwa wanapotea jumla hadi najilaumu kwanini niliwaonea huruma. Nitaondoa huruma zote zinazoweza kuniumiza
LikeLike
Ndivyo inavyokuwa, unaona wanastahili huruma, lakini mwishowe wanakuumiza.
LikeLike
Huruma haina nafasi kwenye uraratibu niliojiwekea.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha kweli hili litaihitaji kulichulia hatua maana watu hata wale WA nyumbani unaowasaidia Sana ndiyo baadaye husema wewe ni mzembe ulipata pesa hukutumia vizuri wakati wao ndiyo walitumia. Kumbe wewe uliwasomesha na baadaye wanakuacha hata kama wewe Una shida zinakuwa ni zako mwenyewe Tu.
LikeLike
Kabisa, watu huwa wanajisahaulisha sana. Huruma zinabaki kuwa mzigo na maumivu kwetu.
LikeLike
Kwa kifupi wale watu unaowaonea huruma ndio wanakuwa makatili sana kwako
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajitahidi kutafuta watu sahihi,maana ninapojaza nafasi na watu wasio sahihi ,ina maana nimeziba nafasi ya watu sahihi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante kocha,Nitajiwekea mchakato wangu na kuufata mchakato mara zote bila kuacha kwa sababu za kihisia.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kweli huruma imewaponza wengi sitaendelea tena na huruma bali ni kufuata utaratibu uliowekwa na kinyume chake ni kuchukua hatua mara moja.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana Kocha. Hakuna huruma, ni au unafuata mchakato wa BM na Chuo Cha mauzo, au upotelee Mbali.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni ukurasa unaotupa kila sababu ya kupuuza hisia na kuheshimu mchakato sahihi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hili ni sahihi kabisa, watu huthamini sana kile ambacho hawawezi kukipata. Lakini kama wanaweza kukipata hukidharau. Hili nimeliona hasa kwenye Kazi zangu. Kuna wateja ambao sikutaka kufanya Kazi zao lakini Kwa kule kuwaonea huruma ndiyo walionisumbua sana
Asante sana kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kabisa uyasemayo tuwape nafasi wenye uwezo na kutokuwaonea huruma wasio na uwezo tuache hisia twende kwenye fikra zaidi
Asante
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni muhimu kuzingatia hili wakati wa kuajiri
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
“watu huthamini sana kile ambacho hawawezi kukipata. Lakini kama wanaweza kukipata hukidharau.” Kamanda, imenitafakarisha Sana hii
HARUMA NI KUFUATA UTARATIBU. Hii Kocha nimejifunza, na masomo ya hapa wiki hii ni MOTO…naendelea kufuatilia masomo haya na muhimu ni KUYAFANYIA KAZI
LikeLike
Kila la kheri kwenye utekelezaji.
LikeLike
Huruma zina rudisha muda mwingine tunajutia maamuzi yetu. Nikuwa na mchakato wa kufata na kutoa ona huruma.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitafanya maamuzi kwa vigezo nilivyojiwekea na sio kwa kuangalia huruma.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kuwa Na huruma Na kuacha utaratibu uliojiwekea kutakupoteza
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Watu hao ambao wewe uliwaonea huruma, wao wanakosa huruma kabisa kwako.
LikeLike
Ndivyo wanaohitaji huruma walivyo.
LikeLike
Watu sahihi wapo, kazi ni kwangu kuweka juhudi zaidi kuwatafuta,
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Huruma ni kufuata utaratibu uliosahihi pekee.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni kweli kabisa. Watu tunaowaonea huruma Mara nyingi hawanaga huruma na sisi. Nitafuata utaratibu niliojiwekea kuliko kuonea Msaidizi huruma.
Asante
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Sana KOCHA ni kweli Tunawapenda huruma Watu ambap wao hawana huruma nasisi. Baadaye wanakuwa miiba kwetu na kutusumbua.
LikeLike
Hakika
LikeLike