3175; Muda kama silaha.
Rafiki yangu mpendwa,
Siyo kila tatizo au changamoto unayokutana nayo kwenye maisha unahitaji kuishambulia kwa ukali.
Zipo nyingine ambazo silaha yake sahihi ni muda.
Kwa kuvipa vitu muda, vinajitatua vyenyewe bila ya wewe kupoteza muda kwenye kuvitatua.
Mfano mzuri ni pale watu wanapoiga kile unachofanya.
Ni hali inayoweza kukuumiza.
Kwa sababu unakuwa umekazana kuweka mkakati wako na kuufanyia kazi.
Hivyo unapogundua kuna mwingine anakuiga, inaweza kukuumiza.
Lakini njia sahihi ya kukabiliana na wanaokuiga ni kuwapuuza.
Wape muda na watapotezwa bila ya wewe kupoteza nguvu zako.
Hiyo ni kwa sababu watu wanaokuiga huwa siyo halisi kwao wenyewe na hata kwa wengine.
Hicho ni kiashiria kizuri cha kushindwa.
Hivyo kama utawapa muda, watapotea tu wao wenyewe.
Kadhalika kwa wale wanaoshindana kwa kupunguza bei kwa kiasi ambacho inatengeneza hasara.
Usikimbilie kupunguza bei kama yeye, badala yake jipe muda na watajipoteza wao wenyewe.
Kwa sababu ni swala la muda kuelekea kifo kwa biashara inayojiendesha bila faida.
Na hata pale wateja wako wanapokuambia wamepata mwingine anayeuza kwa bei rahisi zaidi yako, watake wawe na subira kabla hawajakimbilia huko.
Wasihi wasiharibu sifa yao nzuri ambayo walishajijengea kwa kuhangaika na wapita njia, ambao hawataweza kudumu kwa muda mrefu.
Waonyeshe wazi kwa namba ni kwa nini hao wanaoshusha bei hawataweza kudumu kwa muda mrefu.
Ukiweza kuwashawishi wakasubiri, wanaopunguza bei watapotea haraka sana.
Kitu cha mwisho ni muda unaokuwa umekaa kwenye kitu na changamoto unazokuwa umepitia kwenye kipindi chote ambacho umekuwepo.
Unapokaa kwenye kitu chochote kwa muda mrefu, lazima upitie changamoto na magumu mbalimbali.
Yapo yanayokuumiza na kukuachia makovu.
Hizo pia zinakuwa silaha za kukabiliana na mengine yanayokuja.
Kwa muda unaokuwa umekaa kwenye kitu, tegemea kabisa baadhi ya vitu pale vinapotokea.
Kuumizwa, kupoteza na kukatishwa tamaa inakuwa sehemu ya safari yako nzima.
Hivyo unapokutana na hali za aina hiyo, kuwa kabisa umetegemea vitatokea na jinsi ya kuvikabili ni kuendelea kuvipa muda.
Kuna wakati tunahangaika kutumia silaha kali kukabiliana na baadhi ya mambo tunayokuwa tunapitia, wakati silaha sahihi ingepaswa kuwa ni muda, kwa kuwa na subira.
Subira inatatua matatizo mengi sana bila ya wewe kupoteza nguvu zako.
Ukali wa silaha ya muda upo kwenye kutokufanya chochote.
Yaani unapochagua kupuuza, hupotezi nguvu zako kwenye kuhangaika na vitu vingi.
Badala yake unakabiza fokasi yako kwenye yale ambayo ni muhimu.
Huku mengine ukiyapa muda yajitatue yenyewe.
Muda utakupa hadithi na makovu kwenye mambo mengi unayopitia.
Ambazo pia ni silaha zaidi za kukabiliana na mambo mengi unayoyapitia kwenye maisha yako.
Utulivu wako ni muhimu sana kwenye hii safari ya mafanikio.
Ukiitumia vizuri silaha ya muda, utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Muda huwa unatibu mengi yaliyoshindikana.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muda ni tiba.
LikeLike
Sahihi
LikeLike
Muda Haudanganyi ni silaha ya uhakika.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kweli kabisa
Ukali wa silaha ya muda upo kwenye kutokufanya chochote.
Yaani unapochagua kupuuza, hupotezi nguvu zako kwenye kuhangaika na kila fursa inayokuja ila badala yake unaweka fokasi yako kwenye yale ambayo ni muhimu kwa msimamo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukali wa silaha ya muda upo kwenye kutokufanya chochote.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli muda ni silaha tosha sana kukabialiana na wale wanaoshusha vitu bei na kukosa faida lakini pia wale ambap hawawezi kuvumilia kukaa kwenye mchakato muda utawaondoa maana watashindwa lakini pia kutatua yale ambayo yanaweza tatuliwa na swala ka muda tuiachie asili iamue
LikeLike
Sahihi
LikeLike
Unapokaa kwenye kits chochote kwa muda menu, lazima upitie magnums mbali mbali
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
“Subira yavuta Kheri”
Asante sana Kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
”Ni suala la muda”muda ni tiba ya mambo mengi kwenye maisha yetu na tukiweza kuitumia vizuri ni silaha yenye nguvu sana pale tunapofanya kitu/ kupitia changamoto mbalimbali.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha,Muda kama silaha.
•Utulivu wangu ni muhimu sana kwenye hii safari ya mafanikio.
•Nikiitumia vizuri silaha ya muda, nitaweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu.
Ubarikiwe sana kocha!!
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
MUDA Tu changamoto zingine zinahitaji muda TU tuweke muda na zitaondoka zenyewe tusitumie ukali sana
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
muda nimwalimu mzuri,hakuna ktaharuki mambo
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kocha,utulivu wangu ni muhimu sana kwenye hii safari ya mafanikio,kujipa mda ni nguvu kubwa ya kupunguza usumbufu na makovu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kikubwa ni kujipa muda.Muda ni tiba tosha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kweli kabisa. Muda ni suluhisho kwa sababu wenyewe hausubiri unakwenda tu
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitavipa muda baadhi ya vitu viweze kujitatua vyenyewe..
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana, muda nikipimo sahihi Kwa kila jambo hata kwenye mahusiano yawe ya biashara au ya mdoa bado muda unatoa majibu sahihi
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Muda ni silaha pia hata Kwa upande mwingine wa mafanikio. Maana ukiutumia vizuri Sana bila kupoteza muda utapata matokeo Bora na makubwa sana na kufikia lengo. Maana imetumia silaha yako kushinda Jambo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muda ni kitu muhimu kwenye hii safari ya mafanikio
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Muda utakupa hadithi na makovu kwenye mambo mengi unayopitia.
LikeLike
Hakika
LikeLike