3183; Nini naweza kupenda kwake?
Rafiki yangu mpendwa,
Wateja tulionao kwenye kile tunachouza ni watu muhimu sana kwetu.
Hao ndiyo wanaotuwezesha kulipa gharama mbalimbali kwenye maisha yetu.
Ni kupitia wao kununua kwetu ndiyo tunapata fedha za kuyaendesha maisha yetu.
Wateja wanaonunua kwetu ni watu muhimu sana kwetu.
Swali ni je tunawafanyaje ili waweze kujiona ni muhimu kabisa kwetu?
Njia kuu ya kuwafanya watu waoje jinsi walivyo na umuhimu kwetu ni kuwapenda kweli kutoka ndani ya mioyo yetu.
Kwa wateja wetu, tunapaswa kuwapenda kweli na siyo kwa sababu wanatuletea fedha.
Fedha zinapohusika kwenye jambo lolote lile, huwa ni vigumu kujua kama mapenzi yanayokuwepo ni ya kweli au ya fedha.
Kwa wateja wetu na umuhimu walionao kwetu, tunapaswa kuwa na mapenzi ya kweli kwao ambayo hayaangalii tu fedha.
Hiyo ni kwa sababu wateja hao licha ya kuwa na uhuru wa kununua kwa wengi wanaouza kile tunachouza, wamechagua kununua kwetu kwa kila manunuzi yao.
Ni wajibu wetu kuwaonyesha wateja hao kwamba wamefanya maamuzi sahihi kutuchagua sisi.
Hivyo basi, zoezi la kuwa na mapenzi ya dhati na wateja wetu halikwepeki.
Swali linalofuata ni je nini unaweza kupenda kwa wateja wako?
Hili ni swali ambalo huwezi kujibia kwa kundi, bali unaweza kujibu vizuri kwa mtu mmoja mmoja.
Ili kuweza kukamilisha zoezi la kuwapenda wateja wako, jiulize swali hili kwa kila mteja; ni kitu gani ninachoweza kupenda kuhusu yeye?
Hili ni swali ambalo linakupa sababu halisi za kumpenda mtu.
Kwa kulijibu swali hilo vizuri unakuwa na uelewa mkubwa kwa kila mteja wako na kuwa na sababu sahihi za kumpenda.
Kwenye kulijibu swali hilo, lazima utaje kitu halisi kutoka kwa kila mteja.
Usiwe na majibu ya jumla kwako, mfano kusema nampenda fulani kwa sababu ananunua kwangu.
Majibu ya aina hiyo hayatakuwa na msaada kwako.
Badala yake chagua tabia na sifa mahsusi anazokuwa nazo mtu na ambazo zina manufaa makubwa kwako.
Japokuwa hatuwezi kuvuka maslahi yetu binafsi kwamba kitu cha kwanza kinachotusukuma kuwapenda ni manunuzi wanayofanya kwetu, bado kwa kuwa na sababu nyingine za msingi zinazotusukuma kuwapenda wateja zinachangia kwenye kuboresha mahusiano yetu na wateja wetu.
Ni kitu gani unachoweza kupenda kutoka kwa kila mteja anayenunua kwako ni swali muhimu kuwa na majibu nalo kwa kila mteja.
Majibu hayo yanakuwa na nguvu ya kuimarisha mahusiano yako na wateja hao.
Kwa mahusiano imara, wateja wanaendelea kurudi kununua kwako.
Wanaporudi kununua wanapata thamani kubwa na kushawishika kununua zaidi ya walivyopanga.
Lakini zaidi wanakuwa tayari kuwaleta wateja wengine kwenye biashara yako.
Kazi yako kuu kwenye maisha kama muuzaji ni kujenga na kuboresha mahusiano na wateja wa aina hiyo wengi.
Kadiri unavyokuwa na wateja wa aina hiyo wengi, ndivyo unavyoweza kuwa na maisha bora na yenye uhuru mkubwa.
Unakuwa unayafanya maisha yao kuwa bora kwa thamani kubwa unayowapa ambayo hawawezi kuipata pengine.
Na wao wanayafanya maisha yako kuwa bora kwa kukupa fedha za kuyaendesha maisha yako.
Kwa kuwapenda kweli wateja wako kutoka ndani ya moyo wako, hasa kwa kuwa una sababu ya kumpenda kila mmoja, unakuwa umeufungua moyo wako kwa wateja wako na wao kujiachia zaidi kwako.
Pamoja na wateja wengi unaoweza kuwa unawauzia, ni wajibu wako kumfanya kila mmteja kujiona wa kipekee kabisa kwako.
Hilo linawezekana pale unapokuwa na mapenzi ya kweli kwa kila mmteja mmoja mmoja.
Hiyo inaweza kuonekana ni kazi kubwa.
Ya nini ujisumbue kutaka kumpenda kila mteja wakati tayari wananunua kwako?
Na jibu ni rahisi, unachotaka ni kila mteja kuwa wako milele.
Asiwe tu mteja wako kwa kununua kwako.
Bali pia awe shabiki wa ukweli kwenye biashara yako.
Kwa kuipambania kuhakikisha inawafikia wengi kama yeye.
Hivyo basi, kama tukiacha uvivu na kuufungua mioyo yetu kwa wateja wetu, tunakwenda kupata manufaa makubwa sana.
Tuwapende wateja wetu kwa sababu maalumu kwa kila mmoja na tutaweza kujenga mahusiano bora na wateja hao na kudumu nao milele.
Mapenzi yana nguvu,
Mapenzi yanaendesha dubia,
Na mapenzi yanaweza kutupa chochote tunachotaka.
Tuwe na mapenzi ya kweli kwa wateja wetu na tutaweza kupata chochote tunachotaka kwenye maisha yetu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mapenzi ya kweli kwa wateja huku Yukons na sababu ya kipekee kwa kila mteja yanatupa nafasi ya kupata chochote.
Inatubidi kuongeza ukaribu zaidi kwa wateja wetu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukimpenda kwa dhati toka moyoni pia huwezi kumpunja na pia huwezi kumpa kitu kibaya na pia utamkumbuka pale kitu kipya kinapokuja na siyo hiyo tu utajua unamjulia hali mara kwa mara kwa jua ni rafiki yako na akipata shida ya kijamii unaweka biashara pembeni na kumfuata ili kumfariji na kushirikiana naye kwenye matukio ya kijamii
LikeLike
Kabisa, ukaribu unakuwa mkubwa na mahusiano yanakuwa bora.
LikeLike
Mapenzi yanaendesha dunia. Tukiwapenda watu, nao watatupenda na kupenda biashara zetu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Tukiweza kuwapenda wateja wetu basi tutaweza kupata chochote tunachokitaka kwenye maisha yetu.
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
Tuwapende wateja wetu kwasababu maalum ya kili mmoja tutaweza kujenga mahusiano bora na wateja hao na kudumu nao milele
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Mapenzi ya dhati kabisa yana ushawishi mkubwa si tu uteja bali ushabiki pia. Mteja anajisikia umiliki wa biashara na kuwa tayari kuitangaza vyema hivyo kuvutia wengine kuja kweye biashara na kufanya manunuzi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nini ninachopenda kwake? Swali muhimu nitakaloendele kujiuliza kwa kila mteja ninayemhudumia.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mapenzi yanaiendesha dunia hivyo basi tukiwapenda wateja wetu na watakuwa tayari kutupenda nakupenda biashara zetu nakuwa tayari kutuletea wengine wateja wengi Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Tuwapende wateja wetu na kuwathamini na tutapata tunachotaka
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wajari wateja wako, pia wathamini na kuwapenda na wao wataijari na kuipenda biashara yako.
Asante kocha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mapenzi yanatupa chochote tunachotaka
LikeLike
Kweli
LikeLike
Nitawapenda wateja wangu ili niweze kupata chochote nachotaka kwao.
LikeLike
Vizuri
LikeLike