3199; Mauzo ya Kibabe.
Rafiki yangu mpendwa,
Niwe mkweli kwamba huwa napenda sana mambo ya kibabe.
Hasa pale ubabe huo unapomwezesha mtu kuvuka hofu na kuchukua hatua.
Naamini bila ya shaka yoyote kwamba kwenye hii dunia bila ubabe wa aina fulani, huwezi kupata makubwa unayotaka.
Maana kila kitu ni cha kupambania na hakuna nafasi ya walio wanyonge.
Maana hata vitabu vya dini vimeeleza wanyonge hawana nafasi.
Nilikuwa nasoma habari ya mtu mmoja aliyekuwa mwandishi na mhariri kwenye jarida fulani na hakuwa anaingiza kipato kikubwa.
Mtu huyo alienda kwa mmiliki wa jarida hilo akitaka amwongeze mshahara kwa sababu kazi anayofanya ni kubwa na malipo anayopata ni kidogo.
Mmiliki huyo alimsikiliza kwa makini mpaka alipomaliza kujieleza, kisha akamwambia hataweza kumwongezea kipato kwa sababu kazi yake siyo bora kama anavyodhani.
Mtu huyo aliposikia maneno hayo alikasirishwa sana, iweje mmiliki huyo wa jarida amdharau kiasi hicho wakati yeye ni mwandishi na mhariri mzoefu.
Mmiliki huyo wa jarida alimwambia kwa upole; “Sikiliza, sijifanyi najua chochote kuhusu uandishi au uhariri, lakini najua sana kuhusu biashara. Kitu cha kwanza na muhimu kabisa kwenye biashara ni mauzo. Na kila mtu kwenye biashara anatakiwa kutimiza majukumu yake kwa namna ambavyo yatakuza mauzo.”
Mwandishi akamuuliza; “Unamaanisha nini?”
Mmiliki akamjibu; “Wacha nikupe maana rahisi ya uandishi na uhariri bora; ni ule unaoleta mauzo makubwa zaidi. Huwezi kulipwa kiasi kikubwa kama uandishi wako hauchangii mauzo makubwa.”
Mwandishi alitafakari hilo kwa kina na akaona ni sahihi.
Na hapo alifanya maamuzi kwamba ataacha ukiritimba wa kiuandishi na kuangalia jinsi gani kila andiko analoandaa linachangia kwenye kuongeza mauzo.
Mmiliki wa jarida lile alipoona mhariri wake anataka kuongeza kipato zaidi, akawa anazidi kumjenga kimauzo.
Mara kwa mara alikuwa anampa kauli zinazomwongoza kwenye kutekeleza majukumu yake.
Kwa mfano;
“Acha wasomaji wako wakuongoze nini cha kuandika.”
“Usijifanye una akili kushinda soko.”
“Kama hujui cha kufanya kwenye biashara, jiulize swali hili; nini kitakachoingiza fedha zaidi?”
Mmiliki huyo wa jarida alikuwa pia akiongozana na mhariri huyo kwenye mikutano mbalimbali aliyohudhuria na kumtaka abebe majarida ya kutosha.
Kwenye mkutano, mmiliki wa jarida alitumia kila fursa kusalimiana na watu wote mahimu, kwa kujitambulisha yeye mwenyewe na mhariri wake, kisha alimwambia mhariri ampe mtu huyo jarida. Baada ya kumpa jarida, mmiliki alimwambia mtu waliyesalimiana naye; “Ofisi yako inapaswa kujiandikisha kwenye jarida hili.”
Na aliendelea kusisitiza hivyo mpaka alipopata jibu alilotaka.
Alikuwa king’ang’anizi hasa na ndivyo alivyopata mafanikio aliyokuwa nayo.
Kuna kipindi mhariri huyo aliharibu injini ya gari kwa kuendesha bila oil, mmiliki alimtaka apigie wazalishaji wa gari hiyo wawape injini nyingine, japo hawakuwa na waranti.
Alipiga simu zaidi ya mara 500 na majibu yalikuwa ni hawawezi kupewa injini nyingine.
Lakini mmiliki alimtaka aendelee kupiga simu bila kuacha.
Alipigiwa simu mpaka na makamu wa raisi wa kampuni ya magari kuambiwa kwamba hawawezi kupewa injini nyingine bure.
Lakini mmiliki alimtaka aendelee kupiga simu bila kuchoka.
Na mwisho walipewa injini ya bure.
Mhariri alijifunza mengi kupitia mmiliki wa jarida na kugundua kwa nini alikuwa na mafanikio aliyokuwa nayo.
Na tangu hapo alianza kuangalia kila anachofanya kwa mtazamo wa mauzo.
Haikuchukua muda alibadili mwelekeo wa mauzo wa jarida na akaanza kulipwa vizuri.
Tukiwa hapo hapo kwenye kauli za kibabe kuhusu uandishi na mauzo, ipo habari ya Warren Buffett ambaye alinunua gazeti lililokuwa la miaka mingi.
Katika kuchukua hatua za kutaka gazeti hilo lifanye mauzo zaidi, alibadili mpango wa kulichapa gazeti na kuwa gazeti la kila siku ya wiki tofauti na awali.
Waandishi hawakufurahishwa na hilo, hivyo wakaakua kuanzisha mgomo kumshinikiza Warren kurudisha utararibu ambao walishauzoea.
Warren aliwapa siku saba za kurudi kazini na kama hawatafanya hivyo basi atawafukuza wote. Alimalizia kwa msisitizo akisema; “Hakuna chochote kinachofanyika ndani ya chumba cha habari kinachoathiri mauzo ya gazeti hilo.”
Baada ya kuona msimamo wa Warren, waandishi hao waliacha mgomo wao na kurudi kazini.
Kwenye mifano tuliyojifunza hapa, tumeona jinsi ambavyo mauzo yametumika kama kigezo cha kufanya maanuzi yote muhimu kwenye biashara.
Hivyo ndivyo tunavyopaswa kwenda na maamuzi yote ya biashara zetu, tuangalie kile kinachoathiri mauzo kisha kufanya hicho.
Mauzo ndiyo kipaumbele cha kwanza kwenye biashara yoyote ile.
Tuhakikishe maamuzi yoyote tunayoyafanya yana mchango mkubwa kwenye mauzo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika ni sahihi sana mauzo ndio hubeba kila kitu kwenye biashara yetu ukiwa na mauzo mazuri kila kitu kinawezekana.
LikeLike
Tuuze. Hakuna mbadala wa hilo.
LikeLike
Mauzo ndio kipaumbele cha kwanza kwenye biashara yoyote ile. Tunapaswa kuhakikisha kila tunachofanya kinapelekea kuuza zaidi.
LikeLike
Cha kwanza ni mauzo, kabla ya mengine yote.
LikeLike
Asante kocha kocha mauzo ndiyo kipaumbele cha kwanza kwenye biashara zetu
LikeLike
Tuzingatie hilo.
LikeLike
Bila mauzo hakuna biashara.Maamuzi yote yanapaswa kuangalia mauzo.
LikeLike
Mauzo ndiyo yatakayoamua, kila mtu lazima awe anachangia kwenye mauzo la sivyo ni mzigo.
LikeLike
Mauzo ndio kitu cha Kwanza kwenye biashara, kama huuuzi basi hujaweka nguvu kwenye biashara hiyo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha, kwenye mauzo ndiyo kitu,Jana nikiwa kazini nilimpigia msaidizi Wangu simu kutaka kujua kinachoendelea na kujua waliotakiwa kupigiwa simu kama anewapigia,mmoja wa muhimu alikuwa amempigia mara mbili,nikamwambia nataka kusikia umeongea naye sio hapatikani,na wakati huo alikuwa hajauza vizuri,baadae jioni tunaona alikuwa ana uso wa furaha,anatabasamu,alimpata na kuja kufanya manunuzi mazuri kabisa, nikamwambia hatuhitaji kukata tamaa au kukubali kushindwa.
Nikamwambia ni Mimi muda wote nawaza kuuza na kuangalia namba zetu za mauzo.
Asante kwa somo zuri,lenye mifano mizuri
LikeLike
Safi sana,
Yaani muda wote wa siku, masaa 24 tunapaswa kufikiria kitu cha kwanza kama kipaumbele ambacho ni mauzo.
Hupaswi kufikiria mengine kabla hujajua umeuza kiasi gani na unafanya nini ili kuuza zaidi.
LikeLike
Tuangalie kinachoathiri mauzo na kukifanya hicho ili kuongeza mauzo na siyo kuona kuwa sisi ni wauzaji bora ubora wetu upi kwenye kuuza zaidi na siyo ubabe
Pia mmiliki unapaswa kuwa mbunifu mnganganizi na kuweza kuwaelekeza watu wako wafuate kile unachotaka ili kuongeza mauzo
Tena tunapaswa kuwa na msimamo mkali pele tunapoamua kitu siyo tuongozwae na wafanyakazi bali wao wafuate maelekezo au walete maoni nini tufanye ili tuweze kuongeza mauzo
Pia tuwasikilize wateja wanataka nini
LikeLike
Kabisa, cha msingi mauzo yawe kipaumbele cha kwanza.
Kingine chochote kabla ya mauzo ni usumbufu, mauzo yawe ya uhakika kwanza.
LikeLike
Mauzo ndio kipaumbele cha kwanza kwenye Biashara yeyote ile
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha,maamuzi yoyote nitakayoyafanya lazima niangalie je yana tija kwenye mauzo,mauzo ndo kitu cha kwanza kwenye biashara.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha ni kweli mauzo ni ya muhimu sana kwenye biashara.
LikeLike
Tuyape kipaumbele sahihi.
LikeLike
Hili linanihusu,Nimekuwa mhanga kwa muda sasa. Naenda kulifanyia kazi kwa kiwango cha Kibabe.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mauzo ndio mpango mzima kwenye biashara yafanyike Kwa ung’ang’anizi zaidi ili yalete matokeo zaidi
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza mauzo ni kigezo cha kufanya maamuzi muhimu kwenye biashara.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Tunatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kibabe na kuchukua hatua kwa msimamo ili kufikia lengo. Bora kuchukua hatua isiyosahihi kuliko kutochukua hatua kbsa.
LikeLike
Kabisa, hatua yoyote ni bora kuliko kutokuchukua hatua kabisa.
LikeLike
Mauzo ndio kipaumbele cha kwanza kwenye biashara yoyote ile. Maamuzi yo yote tunayofanya ya we na mchango Mkubwa kwenye mauzo.
LikeLike
Kila mtu anapaswa kuchangia kwenye mauzo.
LikeLike
Mauzo yanaleta Raha kwenye biashara.
Kila mtu achangie mauzo kwenye biashara.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mauzo ndio kipaumbele cha kwanza kwenye biashara yeyote ile.
LikeLike
Namba moja kabisa pale.
LikeLike
Mauzo ndio kila kitu kwenye biashara, asante sana
LikeLike
Hakika, tuuze.
LikeLike
Bila mauzo hakuna biashara
LikeLike
Hakika
LikeLike