Mpendwa mstoa,
Kila mmoja hapa lengo lake ni kufikia ndoto kubwa kabisa ya kuwa BILIONEA. Na kwa sasa tupo kwenye mchakato wa BILIONEA MAFUNZONI.
Ziko sababu nyingi sana za kwa nini wewe uwe BILIONEA na kwenye kitabu cha BILIONEA MAFUNZONI, mwandishi wa kitabu ameelezea sababu kama tano hivi na sababu hizo ni kama ifuatavyo;
Moja, kuweza kufikia na kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Mbili, kutoa thamani kwa watu wengi zaidi.
Tatu ni misaada kwa jamii na wenye uhitaji.
Nne ni kutimiza ndoto binafsi ambazo mtu anakuwa nazo.
Tano ni kuwa mfano mzuri kwa wengine.
Hapa tunaona kwamba utajiri ni kitu kizuri sana. Na aliyekuwa mmoja wa tajiri kuwahi kutokea John D Rockefeller aliwahi kunukuliwa akisema, tunatumia nusu ya maisha yetu kukusanya utajiri na nusu ya maisha yetu kugawa utajiri.
Hapa tunaondoka na somo kubwa kwamba, unapopata unapaswa kurudisha kwa jamii. Na asili ndivyo inavyotaka hivyo.
Asili haipendi ubinafsi, yaani upate ule wewe tu na familia yako. Huo ni ubinafsi.
Na ubinafsi ndiyo kansa inayowamaliza watu wengi. Watu wanajua vitu lakini hawataki kuwapa jamii.
Watu wanapenda kupokea lakini kutoa hawataki. Kwa mfano, Kuna bahari moja iko Africa mashariki na kati inaitwa Dead Sea yaani bahari mfu. Yeyenye inapokea tu lakini haitoi imepelekea maji yake hayafai hata kwa matumizi ya binadamu.
Usipotoa asili inakulaani na kile ulichokikusanya kwa muda mrefu.
Aliyekuwa mtawala wa Roma na Mwanafalsafa wa Ustoa Mwanafalsafa Marcus Aurelius aliwahi kunukuliwa akisema ,
Utajiri pekee ambao utadumu daima, ni ule ambao unaurudisha kwa jamii.
Nukuu; The only wealth which you will keep forever is the wealth you have given away.
Hapa kupitia falsafa ya Ustoa inatufundisha kwamba tuwe na utajiri lakini utoaji ndiyo utafanya utajiri wako udumu daima.
Utajiri wa kweli siyo kukusanya na kumiliki tu mali na fedha tu. Bali pia ni kitendo cha kutoa na kusaidia wengine.
Kuna faida gani ya wewe kufanikiwa sana halafu unakuwa siyo mtu wa msaada kwa wahitaji?
Kwa mfano, Andrew Carnegie alikuwa ni tajiri wa uzalishaji wa chuma kwenye kipindi chake. Kifupi alikuwa yuko vizuri.
Alikuwa na falsafa yake ya utoaji ambayo aliita gospel of wealth yaani injili ya utajiri.
Na alikuwa anasema kwamba wajibu wa utajiri ni kutumia utajiri wake kunufaisha jamii.
Kumiliki utajiri mkubwa peke yake haitoshi lakini kufanya makubwa kwa wengine.
Kwa mfano Andrew Carnegie alitoa utajiri wake mkubwa na kuacha alama duniani mpaka leo na alisema anataka kuacha alama kwenye maarifa, elimu na utamaduni.
Kwa mfano, Andrew Carnegie alianzisha zaidi ya maktaba (libraries) 2500 nchini Marekani na nchi nyingine.
Kupitia falsafa ya leo ya Ustoa, Marcus Aurelius anatufundisha umuhimu wa kutoa.
Kujenga jamii bora kupitia utajiri tunaopata.
Kuacha alama na kumbukumbu.
Kuwekeza kwenye mahusiano kwa kuwasaidia wahitaji.
Hata mfalme selemani alivyobarikiwa naye alitoa kwa jamii utajiri wake. Hakuwa mbinafsi bali aliinufaisha kwa jamii.
Kumbuka watu hawatakukumbuka kwa nyumba nzuri uliyojenga, magari ya kifahari uliyokuwa unayatumia lakini watakukumbuka pale ambapo maisha yako yamegusa maisha yao. Watu hawanufaiki na maisha yako ya ubinafsi bali wananufaika na jinsi wewe unavyotoa kwa wengine.
Ni rahisi muuza chips akakumbukwa mtaani kwako kuliko wewe unayeishi maisha ya ubinafsi na familia yako. Kwa mfano, unapofungua biashara na kuajiri hapo unakuwa mtu wa msaada kwani umerudisha kwa jamii, lakini yule ambaye ana biashara na haajiri anakomaa tu pekee yake ni ubinafsi huo.
Kumbuka, kujitegemea siyo kujitosheleza kwa mfano, Yesu alikuwa anajua na ana nguvu za kutenda miujiza lakini alitafuta watu wakusaidiana naye. Alitafuta watu ili awafundishe kile alichokuwa nacho ili waiendeleze injili mbele. Unapotoa ndiyo asili inakurudishia.
Na utajiri unaodumu daima ni ule ambao tunaurudisha kwa jamii.
Hatua ya kuchukua leo; tumia nusu ya maisha yako kujenga utajiri na kutumia nusu ya maisha yako kugawa utajiri huo kwa jamii.
Hakuna kitu ambacho kina raha kama kurudisha kwa jamii ya wenye uhitaji. Fanya kitu kwa jamii yako na hata ukifa utakumbukwa. Tumia utajiri wako kuacha alama isiyofutika kama Andrew Carnegie alijenga maktaba nyingi, vyuo vingi na taasisi za tamaduni.
Nani atakulilia ukifa?
Rafiki na mstoa mwenzako
Mstoa Mwl. Deogratius Kessy
Asante sana mstoa Mwl.Deo kessy
LikeLike
Karibu sana Hendry Lema.
LikeLike
Asante mwalimu Kessy kwa falsafa hii nzuri
LikeLike
Karibu sana Kizito Bakwanye
LikeLike
Asante sana mwl Deo somo zuri la Falsafa
LikeLike
Karibu sana Beatus Elias Rwitana
LikeLike
Asante Mwl Deo,
Tujitahidi sana tuwe na utajiri mkubwa, maisha yetu yawe na mguso chanya kwa watu wengine.
LikeLike
Hakika Mzee Mbise
LikeLike