3207; Simu ziite sasa.
Rafiki yangu mpendwa,
Nimekuwa naona watu wakiweka picha za bidhaa mbalimbali wanazouza kwenye mtandao (wasap status) pamoja na bei zake.
Kisha wanaweka maelezo; simu ziite sasa.
Nimekuwa nachukulia kauli hiyo kama utani tu na kuona hakuna muuzaji aliye makini anayekuwa anategemea kweli kwamba simu zitaita.
Siku moja nilikuwa namfanyia usaili mtu wa mauzo na kwenye kujibu maswali ya awali alieleza amewahi kufanya kazi ya mauzo kwenye kampuni fulani.
Maswali yangu mengi yaliegemea kwenye hiyo kazi ya mauzo, nikitaka kujua alikuwa anaifanyaje na nini kilimfanya aiache.
Alinieleza jinsi alivyokuwa anafanya ni hivyo, kuposti picha za bidhaa na kusubiri simu ziite.
Nilipomuuliza kwa nini aliacha hiyo kazi, alijibu biashara haikuwa nzuri, maana alikuwa analipwa kwa kamisheni na hivyo hakuweza kuwa anafanya mauzo ya kutosha.
Nilimuuliza kama kuna kitu cha ziada alikuwa anafanya zaidi ya kuposti hizo bidhaa, akajibu hakuna.
Hapo ndipo niligundua kumbe ‘simu ziite sasa’ ni mkakati kamili ambao watu wanautegemea kwenye mauzo.
Nimekuwa pia nakutana na watu ambao mkakati wao mkuu wa mauzo ni kutuma jumbe kwa watu kwa njia mbalimbali. Wakiamini kwa kutuma jumbe nyingi wataweza kuuza kwa ukubwa.
Sikiliza rafiki, watu wanaweza kuzunguka kwa namna wanavyotaka, lakini mkakati sahihi wa mauzo ni ule unaohusisha kuzungumza na mtu kumshawishi anunue.
Na mazungumzo yanaweza kuwa ya ana kwa ana (ambayo yana ushawishi mkubwa ila huwezi kuyafanya kwa wingi) au kwa njia ya simu (ambayo yana ushawishi mdogo ila unaweza kuyafanya kwa wingi).
Vitu vingine vyote unavyofanya kwenye mauzo ni vya ziada tu, vyenye lengo la kuelekea kwenye mkakati wa mazungumzo.
Hivyo vitu vingine ni kama kurusha jiwe gizani, ukisikia mtu amelia kwamba jiwe limempata, unamwambia apite mbele, huyo ni wa kuuzia.
Kwa lugha nyingine ni hayo mengine unayokuwa unayafanya lengo lake ni kumtaka mtu anyooshe mkono kwamba na mimi nataka.
Na hapo sasa wewe ndiye wa kufanya naye mazungumzo kumshawishi anunue.
Sasa kwa sababu watu wengi wamevurugwa na mambo mengi waliyonayo ya kufanya huku muda wao ukiwa mchache, kuwasubiri wakupigie au kukutafuta ni kujipoteza mwenyewe.
Ni lazima wewe uwatafute, kuhakikisha wanajua unachouza na kuchukua hatua ili kupata hicho unachouza.
Hivyo unaweza kupost kila mahali unakotaka kupost, ukatuma ujumbe kila mahali unakotaka kutuma, lakini lazima uanzishe mazungumzo na watu, tena wengi na siyo wachache.
Ongea na watu kuwashawishi wanunue, hayo ndiyo mauzo. Vingine vyote ni vya ziada tu.
Ni kiburi cha hali ya juu sana kuweka bidhaa/huduma zako mtandaoni kisha kusema; simu ziite sasa na ukaona umeshakamilisha kazi.
Unakuwa unajikuta wewe ni nani au una nini hasa cha kuwafanya watu waache yote wanayofanya na kuanza kukutafuta?
Kuna wabishi watasema huwa tunapost na watu wananunua.
Wacha nikuambia, kila kitu kinachofanyika huwa kinafanya kazi, hata kama ni kwa kubahatisha.
Tunachozungumzia hapa ni jinsi ya kuufanya mchakato uwe wa uhakika kwako badala ya kubahatisha.
Turudi kwenye kanuni ya soko kubwa;
Ni asilimia 3 tu ya soko ndiyo wapo kwenye hitaji la kununua sasa.
Na asilimia hiyo 3 ndiyo inalengwa na watu wote wanaotangaza biashara zao kwa njia mbalimbali.
Hawa ndiyo mara moja moja watakutana na ulichopost na wakapiga simu kweli kupata unachouza.
Na wewe ukaona njia yako ya kupost na kusubiri inafanya kazi, hivyo kuendelea nayo.
Lakini haitakuchukua muda utasema biashara ni mbaya, kwa sababu simu haziiti.
Kuna asilimia 17 ya watu kwenye soko ambao wanakusanya taarifa kuhusu kitu wanachotaka kununua. Wanataka kununua, ila hawana haraka ya kufanya hivyo.
Hawa ndiyo watakutana na kitu ulichopost na wakajiambia wakiwa tayari watakutafuta.
Lakini unajua maisha huwa yanaingilia katikati hapo, anakuja kujikuta ameshanunua anachotaka na kusahau kabisa kuhusu wewe.
Sitaendelea na makundi ya chini hapo, kwa sababu nina imani picha umeipata.
Fanya kila unachoamini kitafanya kazi kwa upande wako wa mauzo, halafu jumlisha na mazungumzo ya kutosha na watu.
Post vile utakavyo, tuma jumbe nyingi uwezavyo, fanya chochote ambacho kinakupa amani.
Halafu sasa, wakati unasubiri simu ziite, na wewe unakuwa unazipiga kwa wingi.
Kwa zama tunazoishi sasa, kama mambo hayaendi unatakiwa uyalazimishe kwenda.
Wakati unasubiri simu ziite na wewe endelea kuzipiga.
Usiwe mvivu na mzembe.
Ongea na watu.
Wengi iwezekanavyo.
Hayo ndiyo mauzo.
Huenda unayajua yote haya, lakini bado kuchukua hatua zilizo sahihi inakuwa vigumu kwako.
Kwenye ukurasa utakaofuata tutaliangalia hilo kwa undani zaidi.
Lakini mpaka wakati huo, usisubiri simu ziite, bali ziitishe wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ongea na watu uvae viatu. Simu ziite SASA.
Asante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, lazima kuongea na watu.
LikeLike
Wakati unasubiri simu ziite na wewe endelea kuzipiga.
LikeLike
Zipigwe kwa wingi hasa.
LikeLike
Si kusubiri simu ziite bali kuzipiga vya kutosha.Mauzo ni kuongea na watu.
LikeLike
Tuongee na watu, hakuna namna nyingine.
LikeLike
Asante Sana kocha , ni ukweli ulio wazi kabisa ,kwa zama tunazoishi Sasa Kama Mambo hayaendi vizuri ninapaswa kuyasukuma ili yaweze kwenda .
Asante
LikeLike
Hakuna kuyasubiri, ni kuyafosi yaende.
LikeLike
Usisubiri simu iite piga simu mwenyewe
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Nitaongea na watu wengi iwezekanavyo na hayo ndo mauzo sintasubili simu ziite,bali nitapiga simu mwenyewe.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni kweli pamoja na kuwatumia waone ni lazima uwape ushawishi na kuwaibulia tamaa na hutaweza tu kwa kupost bali kwa kuendelea na njia zingine wapigie simu omba mwaliko wa kukutana naye ili uweze kumshawishi anunue .kuwa karibu nao
LikeLike
Tusiikwepe hatua hiyo muhimu.
LikeLike
Asante,hakuna kusubiri simu ziite ni kupiga simu tu.
LikeLike
Ndio mpango mzima huo.
LikeLike
Tunatakiwa kupiga simu siyo kusubiri tupigiwe simu. Asante sana kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Usisubiri simu ziito bali ziite wewe
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha mauzo ni kuongea na watu wengi zaidi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli nisisubiri simu ziite bali nizipige mwenyewe na pia ninapaswa kutembelea watu na Kuongea nao uso kwa uso.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sitosubiri simu ziite Bali nitazipiga kwa kutosha.
Na Mimi nilikuwa nakosea kwa kuamini nikipost na kutoma jumbe simu zitaita ila siyo kweli
LikeLike
Tusijipe matumaini hewa, tuweke juhudi na tutapata matokeo.
LikeLike
ONAWAWEI=ONGEA NA WATU WENGI IWEZEKANAVYO.
Asante sana kocha kwa makala hii ya leo. Kiukweli kazi kubwa hapa ni kuhakikisha kwamba napiga simu nyingi kadiri uwezavyo.
LikeLike
Nimependa sana hiki kifupisho.
ONAWAWEI.
Mauzo ni kuongea na watu.
Hivyo basi,
ONGEA NA WATU WENGI IWEZEKANAVYO.
Kabla hujalalamika huuzi, anza kujiuliza hapo; umeongea na wangapi?
Na siyo kwa kusubiri wakutafute, bali wewe kuwatafuta.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza mkakati sahihi wa mauzo ni kuzungumza na watu kuwashawishi wanunue.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
ahsante kocha.
nusu ya mauzo ninayofanya kwa siku yanategemea mimi na team kupiga simu.
na simu ninazopiga ni 20 na ninazopigiwa ni 4 wastani kwa siku.
kwa hiyo lazima uzipige nyingi kuliko unazo pigiwa.
LikeLike
Asante kwa kutushirikisha uhalisia huu kwa upande wako.
Sasa zidisha simu unazopiga mara 10, na matokeo yatakuja zaidi ya mara mbili.
Utazidishaje mara 10, najua unajua hilo. Lifanye.
LikeLike
Usisibiri watu wakutafute bali weka Juhudi kuwatafuta.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni lazima simu ziite zaidi ndio ufanye mauzo makubwa kama simu haziiti ni ngumu sana kufanya mauzo..
LikeLike
Na ziite kwa sisi kuzipiga, siyo kusubiri kupigiwa.
LikeLike
Usisubili simu ziite wafuatae wateja walipo na ongea nao Kwa Nia ya kuwashawishi ili kununua
Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo mpango mzima.
LikeLike
Usisubiri simu ziite bali ziitishe wewe.
Asante
LikeLike
Tupige simu, kwa wingi sana.
LikeLike
safi sana,,,,biashara si kama mtu anavyofikiri ni kuweka matangazo status na kukaa ndani hiyo siyo mauzo ni maonyesho
LikeLike
Mauzo yangekuwa rahisi hivyo kila mtu angekuwa ameshatoboa.
LikeLike
Dawa ni kupiga simu, vingine ni vya ziada.
Nimekuelewa vizuri sana Kocha.
Sasa ni utekelezaji tu.
LikeLike
Simu zipigwe kwa wingi.
LikeLike
Asante kocha; watu wamevurugwa sana; lazima niwapigie simu na kuwatafuta mimi kwanza
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni kweli kabisa ongea na watu uvae viatu. Nguvu ya mazungumzo ni kubwa Sana kuweza kushawishi wateja kuja kununua
LikeLike
Ndiyo
LikeLike