3222; Haya matatu yanakushindaje ukiwa hai?
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna mambo mengi unayowajibika nayo kwenye maisha yako.
Mambo hayo ni mengi na yote yanakutegemea wewe moja kwa moja bila kujali wingi na ukubwa wake.
Katika hayo mengi, kuna mambo matatu ambayo kwa namna yoyote ile hupaswi kukubali yakakushinda.
Mambo hayo matatu unapaswa kuyafikia kwa viwango vya juu kabisa bila kuruhusu chochote kuwa kikwazo kwako.
Jambo la kwanza ni afya.
Una wajibu wa kuwa mtu mwenye afya bora kabisa kipindi chote cha maisha yako.
Hilo linawezekana na linakutegemea wewe moja kwa moja.
Inapokuja kwenye afya, wewe ndiye mwenye uwezo wa kila kitu.
Kwa sababu inahusisha ulaji wako, ufanyaji wa mazoezi na kujikinga na hatari mbalimbali.
Unapaswa kuwa mtaalamu wa mwili wako, kuzingatia yote yanayohitajika ili kuwa na afya bora kabisa.
Jambo la pili ni utajiri.
Una wajibu wa kuwa na utajiri mkubwa kwenye kipindi chote cha maisha yako.
Wewe ndiye mwenye ufunguo wa utajiri mkubwa kwenye maisha yako.
Kwani unachohitaji ni kila mara kuhakikisha unaongeza kipato chako huku ukidhibiti matumizi yako.
Tofauti ya mapato na matumizi unaweka akiba na kuwekeza, mara zote, kwa msimamo bila kuacha.
Hupaswi kukubali wala kuruhusu umasikini kuwa sehemu ya maisha yako.
Jambo la tatu ni hekima.
Una wajibu wa kuwa mtu mwenye hekima kwenye kipindi chote cha maisha yako.
Hekima ni zao la kujifunza na kuchukua hatua kwenye yale unayojifunza ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Hili ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako, maana fursa za kujifunza zipo nyingi na za wazi na kuchukua hatua ipo ndani ya uwezo wako.
Hakikisha kila mara kuna mambo mapya unayojifunza na hatua unazochukua ili kuyafanya maisha yako kubwa bora zaidi.
Kuna mambo mengine yanaweza kukusumbua kwenye maisha yako, lakini kamwe hayapaswi kuwa haya matatu.
Haya yanapaswa kuwa vizuri mara zote, kwa sababu yanakutegemea wewe moja kwa moja.
Huna wa kumlaumu kama utakuwa na afya mbovu, masikini na mpumbavu.
Dhamiria kuwa vizuri kwenye maeneo hayo matatu ya maisha yako na utaweza kuwa na maisha bora kabisa kadiri unavyotaka wewe mwenyewe.
Kamwe usikubali mambo hayo matatu kukushinda unapokuwa hai.
Yapambanie kwa kila namna mpaka kuyafikia, hayo ndiyo yanayojenga maisha yako kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Tunaposikia kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe ni pamoja na haya matatu
LikeLike
ahahaha kweli kabisa umenena vyema mzee
LikeLike
Hakika
LikeLike
Afya, utajiri na hekima.
LikeLike
Tuyapambanie hayo kwa kila namna.
LikeLike
Afya, utajiri, Hekima ni moja ya misingi muhimu kusimamia ktk safari ya mafanikio yangu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Afya,utajiri na hekima
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Asante Kocha kwa mambo haya matatu muhimu
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kamwe sitokubali mambo haya 3 kunishinda :-
Afya, utajiri na hekima
LikeLike
Vizuri, yapambanie.
LikeLike
Nitayapambania mambo haya matatu na kamwe yasiweze kunishinda Kwa uwezo wa mwenyenzi Mungu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kutunza afya yangu na kupigana na umasikini na upumbavu ili niweze kujenga maisha yangu kwa uhakika.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mala zote nitajisukuma kuyapa kipaumbele Mambo hayo matatu. Afya, utajiri,hekima
Asante Sana.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Mambo matatu hayapaswi kunishinda kwenye maisha yangu nayo ni,
1. Afya, natakiwa niujue mwili wangu na nidhibiti afya yangu.
2. Utajiri. Nitaweka akiba na kuwekeza kwenye maisha yangu yote. Pia nitadhibiti matumizi yangu.
3. Hekima. Nitakuwa mtu wa hekima siku zote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Afya, ytajiri na hekima katika haya mimi ni mbobebu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante kocha huu ndiyo msingi ambao nilijiwekea yaani afya, Utajiri,na hekima
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Hivyo ni vitu ambavyo napambania kila siku Afya, Utajiri na HEKIMA. Nimekuelewa sana hapa kwenye makala
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Huna wa kumlaumu kama utakuwa na afya mbovu, masikini na mpumbavu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Afya utajiri na hekima ndio mambo muhimu tunayotakiwa kuyafanyiia kazi katika maisha yetu
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hapa umenena, Nitazingatia yafuatayo:-
1. Afya – ulaji, mazoezi na kujikinga na hatari
2. Utajiri – Kuongeza kipato huku nikidhibiti matumizi, kuweka akiba na kuwekeza kwa msimamo mara kwa mara bila kuacha.
3. Hekima – Kujifunza mambo mapya na kuchukuwa hatua.
LikeLike
Imekamilika hiyo.
LikeLike
Asante sana kocha kwa mambo haya matatu
LikeLike
Karibu
LikeLike
Always nitasimami afya, utajiri na Hekima katika Marshall yangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Afya utajiri na hekima. Nitayapambania haya matatu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha kila wakati nimekuwa nazingatia na kufanyia kazi mambo hayo. Na ndio msingi wa utajiri ulipo
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike