3225; Raha.

Rafiki yangu mpendwa,
Raha huwa ina msukumo mkubwa sana kwetu.
Mambo mengi tunayoyafanya ni kwa msukumo wa raha.
Tunayafanya kwa sababu yanatupa raha.

Kufanya mambo kwa sababu ya kupata raha inaweza kuwa kichocheo au kikwazo cha mafanikio yetu.

Raha inakuwa kichocheo cha mafanikio pale mchakato mzima wa mafanikio unapokuwa unatupa raha. Yaani tunakuwa tunapata raha kutoka kwenye mchakato wa mafanikio.
Hilo linatupa msukumo wa kuendelea kukaa kwenye mchakato wa mafanikio bila kuacha.

Raha inakuwa kikwazo cha mafanikio pale unapokuwa na raha nje ya mchakato wa mafanikio. Yaani vitu vinavyokuwa vinakupa raha vinakuwa nje ya mchakato wako wa mafanikio.
Kwa kuwa raha ipo nje ya mchakato, unajikuta ukiharakisha au hata kuahirisha mchakato ili tu kufanya vile vinavyokupa raha, ambavyo ni nje ya mchakato.

Kwa kuwa mafanikio makubwa yanakuwa yanataka umakini wetu wote, kitu chochote kinachotoa umakini huo kwenye mchakato wa mafanikio kinakuwa usumbufu kwetu.
Pale tunapokuwa tunaharakisha au kuahirisha mchakato ili kwenda kupata raha, huo unakuwa ni usumbufu unaotutoa kwenye mchakato.

Ili kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ufanye mchakato wako wa mafanikio kuwa ndiyo chanzo kikuu cha raha kwako.
Furahia sana kile unachofanya na kuwa na msukumo wa kukifanya mara zote.
Kadiri unavyoweka muda na umakini wako wote kwenye kufanya kitu, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora kabisa, yanayokupa mafanikio makubwa.

Tusiruhusu kingine chochote kuwa kikwazo kwetu kupata mafanikio makubwa tunayoyataka.
Mchakato wetu wa mafanikio unapaswa kuwa ndiyo chanzo kikuu cha raha kwetu.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe