3226; Biashara ambayo upo.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye harakati zetu za kupata mafanikio tunayoyataka, huwa tunahangaika na mambo mengi sana.
Kwa sababu tunakuwa tunayataka sana matokeo na kwa haraka, huwa tunaona kama tumechelewa sana.
Hivyo tunakazana kuharakisha kwa kuhangaika na mambo mengi.
Kila fursa ambayo tunaiona au kuisikia tunaiendea kwa kuona hiyo ndiyo yenye matokeo tunayokuwa tunayataka sana.
Kwa haraka tunayokuwa nayo ya kupata matokeo, tunaishia kupoteza muda na nguvu na kuishia kuchelewa.
Tunahangaika na mambo mengi kwa lengo la kuharakisha safari, lakini matokeo yake ni kuchelewa zaidi.
Dawa ya hili ni moja tu, fokasi.
Kuweka umakini wako wote kwenye kile ambacho unakifanya mpaka kikupe kile hasa unachotaka.
Kuna kauli huwa inasema jali biashara yako (mind your business).
Kauli hii ina maana kubwa sana kama itafanyiwa kazi.
Unaifanyia kazi kauli hiyo kwa kujua biashara ambayo upo kisha kuipa hiyo umakini wako wote.
Mengine yote unayapuuza na kupambania hilo moja pekee.
Unakaa kwenye kile ambacho unajua ndiyo unachofanya.
Kila unachofanya, kinakuwa kinahusisha hicho kikuu moja kwa moja na siyo nje ya hapo.
Huhangaiki na kila kinachokuja mbele yako, hata kama ni rahisi kiasi gani.
Nguvu na umakini utakaoutawanya kwenye mambo mengi, ukikusanya kwenye biashara yako kuu moja, utazalisha matokeo makubwa na ya tofauti kabisa.
Unazo fursa za kufanya kwa mitindo tofauti.
Unaanza na wingi, ambapo unaongeza kiwango chako cha ufanyaji. Kwa mfano kufanya mara kumi ya ulivyozoea kufanya.
Kisha unaenda kwenye kufanya kwa ubora, ambapo unaboresha zaidi vile unavyofanya.
Na mwisho ndiyo kufanya kwa upya.
Wengi huwa wanakimbilia kuboresha kabla ya kufanya kwa wingi.
Wanaishia kushindwa na kukosa kujifunza pia.
Kwa sababu wanakuwa hawajui nini kimepelekea washindwe, kiwango chs ufanyaji au ubora.
Kabla hujafanya kitu chochote tofauti au kipya, hebu fanya hicho hicho kwa ukubwa zaidi.
Fanya angalau mara 10 ya unavyofanya sasa kwa muda mrefu.
Kisha angalia matokeo unayopata.
Jua biashara ambayo upo na itendee kwanza haki kabla hujahangaika na mambo mengine.
Kuna hazina kubwa unayoiacha hapo ulipo sasa na kukimbilia vitu vipya.
Achana na hilo kwa sasa na kaa kwenye biashara ambayo upo kwanza.
Kila wakati jikumbushe kujali biashara yako na kufanya yale unayofanya kwa wingi kwanza kabla ya kubadili chochote.
Mara nyingi unakwama kutokana na kufanya kwa udogo kile ambacho tayari unakifanya.
Ukiongeza tu wingi, unajiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo makubwa na bora.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Fanya angalau mara 10 ya unavyofanya sasa kwa muda mrefu.
LikeLike
Hapo ndipo unaweza kujua kama kitu kinafanya kazi au la.
LikeLike
Focus Mind your business times Ten
LikeLike
Yes
LikeLike
Nakwenda kuichukua hatua yakufanya kwa uwingi kile ninacho fanya
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwenye biashara ambayo nipo Nita FOKASI na KUWEKA umakini wangu Wote nitaikuza mara Kumi na naamini nitapata matokeo bora kabisa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kaa kwenye biashara Moja weka nguvu zako zote fanya Kwa wingi ubora na upya
Asante sana
LikeLike
Ndiyom
LikeLike
Hakika tunahitaji kuwa na focus kubwa kwenye kile tunachofanya kwa umakini zaidi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Ninakataa kabisa kwamba Mimi ni wa kawaida.
na pia ninakaa kwenye kile ambacho najua ninakifanya.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Anza na Wingi wa kile unachofanya,halafu ubora unafuata,kwa mtindo huu utafanikiwa sana. ✍️
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kupitia fokasi tunaweza kufanya makubwa.Nitafanya kwa wingi zaidi yale ninayopaswa kufanya kwenye biashara ili kuikuza zaidi(100).
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike