3231; Ugumu na ubora.
Rafiki yangu mpendwa,
Ugumu wa kupata kitu na ubora wake ni vitu ambavyo vinaendana.
Kadiri kitu kinavyokuwa kigumu kupatikana ndivyo pia kinavyokuwa bora.
Na kitu ambacho ni rahisi kupatikana, huwa pia siyo bora.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa watu unaojihusisha nao.
Kadiri inavyokuwa rahisi kwa watu kujihusisha na wewe, ndivyo pia wanavyokuwa siyo bora.
Inapokuwa vigumu kwa watu kupata nafasi ya kujihusisha na wewe, ndivyo unavyopata watu walio bora.
Ili kupata watu ambao ni bora, weka ugumu kwenye mchakato wanaopaswa kufuata ili kupata nafasi ya kujihusisha na wewe.
Hilo litapunguza wingi wa watu utakaowapata, lakini litakupatia wale walio bora zaidi.
Lakini pia watu wanaopitia ugumu kupata kitu huwa wanakithamini zaidi kuliko wale ambao wanapata kitu kirahisi.
Hivyo unapokuwa umeweka ugumu wa watu kuvuka ili kujihusisha na wewe, wale wanaovuka ugumu huo wanathamini nafasi wanayokuwa wameipata.
Wakati wale wanaokuwa wameipata nafasi kirahisi, hawaipi uzito mkubwa, hivyo kuwa tayari kuipoteza kirahisi pia.
Ugumu ni chujio zuri sana la kupata ubora.
Unapotumia chujio hili, unapata matokeo ambayo ni mazuri.
Japo utapata idadi ndogo kuliko kama usingetumia ugumu.
Wengi kwa hofu ya kukosa wingi, wamekuwa wanaepuka kutumia ugumu.
Na kweli wanapata wingi, lakini ambao siyo bora.
Matokeo yake yanakuwa ni kupata usumbufu mwingi kwa kuwa na wingi usio bora.
Kamwe usiende kinyume na asili na saikolojia ya binadamu.
Vitu vingi vimebadilika, lakini binadamu amenaki vile vile.
Nenda naye kwa namna sahihi ili uweze kupata kile unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ugumu ni chujio zuri sana la kupata ubora.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tafuta walio Bora achana na wingi ni usumbufu tu
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Vitu vingi vimebadilika, lakini Binadamu amebaki vile vile. Nenda naye kupata unachotaka
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wanaopitia ugumu kupata kitu huwa wanakithamini zaidi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ugumu ni chujio la kupata ubora
Kadiri kitu kinavyokuwa kigumu kupatikana ndivyo pia kinavyokuwa bora.
LikeLike
Kweli
LikeLike
Watu wanao pata kitu kwa ugumu huwa wanakithamini zaidi kuliko wale ambao wanapata kitu kirahisi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha,ugumu ni chujio la kupata kilicho bora.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kamwe usiende kinyume na asili na saikolojia ya binadamu.
Vitu vingi vimebadilika, lakini binadamu amenaki vile vile.
Nenda naye kwa namna sahihi ili uweze kupata kile unachotaka.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Nitakaa kwenye mchakato sahihi hata pale Nina pokumbana na ugumu kwani ndiyo kwenye thamani na ubora.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
ASANTE sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
ugumu unazalisha ubora………. appreceate
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ugumu ni chujio zuri sana la kupata ubora.
LikeLike
Hakika
LikeLike