3234; Hamasa na Nidhamu.
Rafiki yangu mpendwa,
Hamasa na nidhamu ni viungo muhimu sana kwenye mafanikio yoyote makubwa kwenye maisha.
Hivi visipokuwepo, ni vigumu sana mtu kuweza kuvuka vikwazo mbalimbali vilivyopo kwenye safari ya mafanikio.
Lakini kwa bahati mbaya sana, hivyo pia ni vitu ambavyo haviwezi kufundishwa, kuuziwa wala kulazimishwa.
Hivi ni vitu ambavyo vinakuwa na nguvu kama vitaanzia ndani ya mtu mwenyewe.
Lakini vinapotoka nje ya mtu, kwa namna yoyote ile vitafanya kazi kwa muda mfupi, lakini baada ya hapo vitakwama.
Unaweza kulipa kufundishwa hamasa na nidhamu, lakini kama hivyo havitakuwa msingi wa maisha yako, havitadumu.
Utapata matokeo mazuri kwa muda unaokuwa navyo, lakini baada ya hapo utakwama.
Tumekuwa tunaona hili kila mara kwa watu wengi.
Wanakuwa na uhitaji wa kitu fulani, au wanaanzia chini kabisa, hilo linawapa hamasa na nidhamu kubwa ya kufanya.
Lakini wanapopata kile walichokuwa wanataka, hamasa inashuka na nidhamu inapotea kabisa.
Matokeo yake ni ule ukuaji waliokuwa nao unapungua na hata kuanza kuanguka.
Kiasili, hamasa na nidhamu ni vitu ambavyo vinapaswa kuwa ndani ya mtu au kitu.
Ng’ombe hahitaji hamasa na nidhamu kutoa maziwa.
Kuku hahitaji hamasa na nidhamu kutaga.
Ukiwa na njaa hahitaji hamasa na nidhamu kula.
Ukikutana na mbwa mkali na anayetaka kukung’ata huhitaji hamasa na nidhamu kukimbia.
Nadhani kwa hiyo mifano unapata picha.
Kwamba hamasa na nidhamu ni vitu ambavyo vinapaswa kuwepo tayari, kinachoendelea ni vitu hivyo kutumika tu.
Pale unapovitegemea vitoke nje yako, huwa vinafanya kazi kwa muda kisha vinakwama.
Uzuri ni kwamba, kila mtu kwenye maisha yake, kuna vitu ambavyo hahitaji hamasa wala nidhamu kuvifanya.
Yeye anavifanya tu, kwa sababu ni sehemu ya maisha yake.
Anapoona wengine wanakwama kuvifanya, anashangaa kabisa wanakwamaje.
Hapo ndipo mafanikio makubwa ya mtu yalipo.
Rafiki, je wewe ni maeneo gani au vitu gani kwenye maisha yako ambavyo unavifanya mara zote bila kuhitaji hamasa na nidhamu?
Je umeshafanya vitu hivyo kuwa ndiyo kazi yako kuu ambapo unayajenga mafanikio yako makubwa?
Karibu ushirikishe majibu yako kwenye maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kukaa kwenye mchakato wa Mauzo, kusoma na kuandika navifanya bila kuhitaji hamasa na nidhamu.
LikeLike
Safi sana, hakuna kitakachoweza kukuzuia kwa ngazi hiyo uliyofikia.
LikeLike
Kutoa elimu shirikishi,kufwatilia wateja.
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
Asante Kocha,
Afya yangu na kujifunza zaidi kwenye kile nilichoamua kukifanya ni maeneo nisiyohitaji hamasa na nidhamu.
Ninaamini afya bora ni utajiri namba moja ambao nikiutunza kwa kiwango cha juu, utajiri namba mbili Uhuru wa kipato (fedha) ni swala la muda tu.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kujifunza, kudadisi, kuwa na mashaka, kutake risk, kujifanyia tathmini ya nilipo, ari ya kutaka kwenda hatua ya juu zaidi, kuwaza jinsi ya kutengeneza pesa(kila siku mchana na usiku)….haya sihitaji hamasa kuyafanya.
LikeLike
Safi sana, yaishi hayo mara zote.
LikeLike
Vitu ambavyo ninavifanya mara zote bila kuhitaji hamasa na nidhamu ni Kuweka akiba na kuwekeza, kuamka asubuhi na mapema kusoma na kuandika.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kutafta maarifa sahihi na kujituma haya maeneo sihitaji hamasa+nidhamu kuyafanya.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kusoma vitabu, Kufuatilia mifumo, kukaa katika michakato mbalimbali sihitaji hamasa toka nje ,tayari ninayo. Hata Kama ninachelewa kutoa MAONI huwa tayari nimeitekeleza na ninaendelea kuichakata
Asante Sana.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Kufanya na kufuatilia mchakato wa mauzo na kujifunza
LikeLike
Safi, kaa humo.
LikeLike