3242; Hujataka vya kutosha.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama haupo tayari kutoa kafara na kupoteza vitu ulivyonavyo ili kupata kile unachotaka, basi jua hujakitaka vya kutosha.
Na kitu chochote ambacho hujakitaka vya kutosha, huwezi kukipata.
Kwa kitu chochote kile unachokuwa unakitaka, huwa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali kwenye kukipata.
Kama hujajitoa kweli kupata kitu, hutaweza kuvuka vikwazo cha changamoto unazokutana nazo kwenye kukipata.
Dunia ina utele wa mafanikio na rasilimali mbalimbali ambazo watu wanakuwa wanazitaka.
Lakini duniavhuwa haipo tayari kutoa tu kwa kila anayetaka vitu hivyo.
Badala yake huwa inawajaribu na kuwapima watu ili kujua wamejitoa kiasi gani ili kupata kile wanachotaka.
Dunia inawaheshimu wale wanaotaka kitu hasa na kufanya kila wanachopaswa kufanya ili kukipata.
Na inawapuuza wale wanaotamani vitu ila hawajajitoa kweli ili kuvipata.
Kila kitu kwenye maisha huwa kina gharama zake. Na kadiri kitu kinavyokuwa kikubwa, ndivyo gharama yake inakuwa kubwa zaidi.
Dunia haiwapi watu kitu chochote kile bure, bali inawataka wakipambanie ndiyo waweze kukipata.
Kama kweli unakitaka kitu, kuwa tayari kujitoa hasa mpaka kukipata.
Na kama haupo tayari kujitoa hasa kupata kile unachotaka, usijidanganye nacho, jiambie tu wazi kwamba hukihitaji sana kisha endelea na mambo mengine.
Jinsi maisha yalivyo na vikwazo na changamoto, kujidanganya wewe mwenyewe ni kujiongezea mzigo usio na sababu.
Kama unakitaka kitu kweli kiendee kwa kujitoa hasa.
Na kama haupo tayari kujitoa hivyo, usijidanganye kwamba mambo yatatokea kimiujiza.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Dunia haiwapi watu kitu chochote kile bure, bali inataka wakipambanie ndio waweze kukipata.
LikeLike
Lazima kulipa gharama.
LikeLike
Nitazidi kupambania yale yote ninayoyataka katika maisha sababu dunia haitanipa bure.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitazidi kupambana ili kufikia malengo kwa kujitoa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kila kitu kwenye maisha kina gharama zake.
Shukrani kocha.
LikeLike
Lipa gharama.
LikeLike
Niko tayari kutoa gharama kubwa kwa sababu mafanikio ninayoyataka ni makubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kama unataka kitu lipa gharama no free lunch
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha,
Umenikumbusha dunia haiwapi watu kitu chochote kile bure, Bali inawataka wakipambanie ndiyo waweze kuki pata. Niko tayari kuendelea kujitoa hasa kupambania kile ninachokitaka.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
“Dunia haiwapi watu kitu chochote kile bure, bali inawataka wakipambanie ndiyo waweze kukipata. Kama unakitaka kitu kweli kiendee kwa kujitoa hasa”
Nitajitoa kweli kweli ili kupata mafanikio
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwa kitu chochote kile unachokuwa unakitaka, huwa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali kwenye kukipata.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Maisha yamejaa vikwazo na changamoto za kila aina.
Kama Kuna kitu unakitaka, unapaswa kukipambania Hadi ukipate.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kulipa gharama ni muhimu kwa kitu chochote unachokitaka
LikeLike
Hakika
LikeLike